Moto mkubwa kiwanda cha sigara

majany

JF-Expert Member
Sep 30, 2008
1,223
579
Wakuu nakatiza hapa maeneo ya kiwanda cha sigara(nyerere road) nashuhudia moshi mkubwa sana unatoka kwenye moja ya store zao...wananchi wanaoshangaa ni wengi...mwenye kuwajua fire awape taarifa...
 
Moto unawaka kampuni ya Sigara sasa hivi, fire brigade zote Dar ziko eneo la tukio.
Habari zaidi baadaye
 
duu isije ikawa ndio ile hesabu ya stock taking inaharibiwa hivyo..
 
Sigara wana emergency preparedness and response programme nzuri tu. watakuwa wameshafanya utaratibu, that is, kama hawafanyi mock drill now.
 
Usikute ni mambo ya Insurance!!!!!! Hebu tusikie maana wavuta sigara duniani wanapungua, uhamasishaji umesaidia!!! Nilikuwa na ndungu zangu na marafiki chain smokers wameshacha!!! Upako mwingi so bora kumaliza, walipwe watambae!!! Si uliona kiwanda cha magodoro kule mahali wakati wanataka kuhamishia kiwanda Dar? Mambo ya Paradise Hotel je? Chezea tanzania, kila kitu kinawezekana, jaribu!!
 
Bora kiungue kabisa. Huu ujinga wa taifa kutegemea kodi kwenye vitu haramu utakoma. Kikimalizika hicho moto mkubwa pia uwake kiwanda cha pombe pale karume.
 
Wakuu nipo hapa magomeni zimepita gari za kuzima moto 3 zinatokea hupande wa kinondoni,,,
hatujui wapi kimenuka 2naomba mtupe update wakuu
nawasilisha
 
Bora kiungue kabisa. Huu ujinga wa taifa kutegemea kodi kwenye vitu haramu utakoma. Kikimalizika hicho moto mkubwa pia uwake kiwanda cha pombe pale karume.

Yaan TBL kiwake moto??hahaha...kijana badilisha kauli....
 
Nchi inayotegemea walevi na smokers huku ikiwa na utajiri wa rasilimali kibao, Lazima tuandamani hicho kiwanda kikiungua ndo tunategemea kupata hela za safari za bwana mkubwa hapo
 
Back
Top Bottom