Moto aliodai kuuwasha Reginald Mengi dhidi ya mafisadi ulizima au ulizimwa?

Mengi ameptima maji na akagundua kwenye ile vita alikua pekee, wengi wetu ni wapiga debe tu kwenye mitandao na mitaani... leo tukiambiwa tusimame tupinge ufisadi, tunakua bize

Charity starts at home
Two posibilities:
(1)Alikuwa hajui adui yake ni nani, baada ya kumjua kuwa ni yule yule aliyekuwa akimtanguliza kumuunga mkono katika vita (Hope mnamjua) aka freeze,akabanwa,akazibwa mdomo na sasa Vyombo vyake vya habari vinamshabikia adui yake pamoja na washirika wake
(2) Alikuwa mnafiki tu,alikuwa nataka kupata umaarufu na kuleta chuki zake binafsi na wafanya biashara wenzake na kujipendekeza kwa Muungwana ili kuficha UFISADI ALIOUFANYA
 
Tuelewe kuwa Dr Slaa pamoja na ujasiri wa kizalendo alionao lakini ana ''immunity''. yeye ni mbunge na ni katibu mkuu kwahiyo kauli zake huwa zipo katika capacity hiyo. Mengi ni raia kama wewe na mimi, lakini tusidharau mchango wa vyombo vyake vya habari. Kuna gazeti lake la kiingereza limetufunua sana macho, lina habari na data zisizopingika, muulizeni Masha.
Tatizo letu tunadhani haya ni mapambano ya wateule fulani, si kweli. leo kila mtu anasubiri Slaa atasema nini, ukweli ni kuwa sisi tuna wajibu na ukaribu mkubwa sana na jamii kuliko Dr peke yake jukwaani. Ni lazima tuwaeleze watu wetu nchi ilipotoka , ilipo na inapokwenda.
Mimi naanza na ninyi, Kila atakayesoma habari hii amueleze ndugu yake kuwa baada ya miaka 50 ya uhuru ifuatayo ni shule ya watoto wetu, huku mtu mmoja akijengewa hekalu la bilioni 2 zaidi ya thamani ya kijiji chote. Tuwaeleze watu kuwa kofia/kanga na vitenge havitawakomboa, bali uthubutu,ujasiri na uamuzi mgumu dhidi ya mazoea ndio jibu litakalo wakwamua.

Mkuu Nguruvi, kwa kiasi kikubwa nakubaliana na hayo uliyoyaandika hapo juu, na nimekugongea "kasanks".
Lakini nimjuavyo Mengi (nothing personal against him), kila analilofanya lazima kuna clandestine motive nyuma yake. Nasema hili from my personal experince kwenye interactions kadhaa naye.
Kuonekana kuwajali siju walemavu au media campain against akina Mkapa, Masha, nk is a cosmetic gimmick only - anataka watu wamuone he's doing it for the right course wakati deep down kuna ulterior samsing.
 
Unjua ninashangazwa sana na wengi walichangia,kwani wanafikiria ya kuwa mengi ni Saint.Ule moto aliouanzisha haukuziwa bali yeye mwenyewe alichangia kuuzima.inaweza kuwa alikuwa yuko right katika ya yale aliyoyasema,lakini mimi naona kitu pekee kilichosababisha kusema yale siyo kwa uchungu wa nchi yake bali kwa ajili biashara zake.Kwani nina uhakika watu walimkumbusha madudu aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanya.yanamfanya na yeye kuwa miongoni mwa hao mapapa anaowazungumzia.Hivi lile sakata lake la NBC limezimwa vp?na kuna meingine mengi sana ambayo watu walitumia kumnyamazisha.....
 
Tatizo letu tuliowengi ni mahodari wa kukagua kuchambua na kuhakiki michango ya wenzetu pasipo kujihoji kwa uaminifu ni upi mchango wetu kwa maendeleo ya taifa letu? Kabla ya kuangalia nani kafanya nini angalia unatakiwa kufanya nini na ufanye kwa uaminifu na usahihi.
 
Kwa maoni yangu, Mengi ana dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi ila hakuungwa mkono na Watanzania kwa sababu bado wako kwenye usingizi mzito, hawajui kwamba adui mkubwa wa maendeleo yao ni ufisadi unaolelewa na utawala wetu mbovu.
 
Mengi ni mnafiki tu, huwezi kupiga vita ufisadi katika nchi hii na hapohapo unamsifia JK kuwa ni kamanda mzuri katika vita hiyo,il hali JK ndiye anwafuga hao mafisadi na yeye mwenyewe kaingia madarakani kwa njia ya kifisadi.
 
Ukisoma hii thread itakupa picha sisi Watanzania tulivyo WANAFIKI WAKUBWA NA TUNA PENDA UMANGI MEZA. Watu hapa wanamlaumu Mzee Mengi kana kwamba anapokea malipo (kutoka kwenye kodi zetu) lakini hafanyi kazi ya kupiga vita ufisadi kama inavyotakiwa.Vita dhidi ya ufisadi inahitaji ujasiri wa hali ya juu hasara zake ni kubwa hata kupoteza maisha ndiyo maana BABA NA MAMA ZETU WALILIONA HILO NA KUHAMUA KUKAA KIMYA KUJAZA NAFASI. Badala ya kujificha nyuma ya keyboards na kulaumu watu wengine kwa kujaribu kudhubutu, tujiangalie sisi wenyewe na kujiuliza mchango wetu ni upi kwenye kupiga vita ufisasi

Watanzania tunaunga mkono ufisadi lakini hatujui kama tuna fanya hivyo,mfano mzuri ni hii thread,tunadiriki kusema wabunge wapiganaji walikuwa wanaganga njaa.Mwakyembe kwenye ile report ya Richmond alikuwa na uwezo wa kumsafisha Lowassa na wenzake na labda hali ya kisiasa Kyela isingekuwa kama ilivyokuwa,sasa watu kama hawa wakisoma hapa tunajaribu kuwaita mafisadi kwa kujaribu kupiga vita ufisadi bila misingi yoyote ile ,inasikitisha kutia huruma na kukatisha tamaa kwa wale wanaotaka kudhubutu.

Mzee Mengi kutoa msaada kwa walemavu na kusema ana clandestine motive bila ushaidi ni kutaka kuondoa neno MSAADA kwenye kamusi. Bill Gates anapotoa msaada wa nyandarua sijui na yeye ana Motive gani?

Mambo kama haya yatamfanya kila mtu awe fisadi.
 
Ukisoma hii thread itakupa picha sisi Watanzania tulivyo WANAFIKI WAKUBWA NA TUNA PENDA UMANGI MEZA.
Nina wasiwasi kama kweli unaelewa maana ya unafiki - sasa ngoja nikusaidie kwa kukupa mfano - mtu anayelaumu utendaji ndani ya serikali lakini anamsifu kiongozi anayeiteua na kuiongoza serikali hiyo hiyo ni mnafiki, upo ?
Watu hapa wanamlaumu Mzee Mengi kana kwamba anapokea malipo (kutoka kwenye kodi zetu) lakini hafanyi kazi ya kupiga vita ufisadi kama inavyotakiwa.
Hizi tuhuma unazitoa wapi ama umesoma wapi kwamba Mengi analaumiwa kwa kupokea malipo (kutoka kwenye kodi zetu) lakini hafanyi kazi ya kupiga vita ufisadi. Kwanza huyo Mengi alipwe na nani na kwa nini alipwe - haya unayatoa wapi.
Vita dhidi ya ufisadi inahitaji ujasiri wa hali ya juu hasara zake ni kubwa hata kupoteza maisha ndiyo maana BABA NA MAMA ZETU WALILIONA HILO NA KUHAMUA KUKAA KIMYA KUJAZA NAFASI.
Aha, kwa hiyo Mengi moto aliouwasha dhidi ya mafisadi ameuzima kwa kusalimu amri ili asipate hasara na kupoteza maisha. Wahenga husema if you cant fight them, join them na kwa maana hiyo Mengi amebwaga manyanga na sasa anakula nao bila wasi wasi tena. When the going gets tough, the tough keep going mfano wa shujaa Dr. Slaa.
Badala ya kujificha nyuma ya keyboards na kulaumu watu wengine kwa kujaribu kudhubutu, tujiangalie sisi wenyewe na kujiuliza mchango wetu ni upi kwenye kupiga vita ufisasi
Sawa, wengine mchango wetu ni kuwapigia kelele hao mafisadi kwenye jukwaa letu nyuma ya keyboard kama Mengi naye alivyofanya kwa kutumia vyombo vyake. Tofauti ni kuwa sisi tunaendeleza mapambano, yeye mmmh.
Watanzania tunaunga mkono ufisadi lakini hatujui kama tuna fanya hivyo,mfano mzuri ni hii thread,tunadiriki kusema wabunge wapiganaji walikuwa wanaganga njaa.
Nakuomba ukumbuke kuwa ndege wanaofanana huruka pamoja. Itakuwaje watu mlale kitanda kimoja na kujifunika shuka moja halafu ubaki ukimnyooshea kidole mwenzio kuwa ni mchafu huku huondoki ? Ukisikia unafiki na kuganga njaa ndiko huko !!
Mwakyembe kwenye ile report ya Richmond alikuwa na uwezo wa kumsafisha Lowassa na wenzake na labda hali ya kisiasa Kyela isingekuwa kama ilivyokuwa,
Mwakyembe mwenyewe aliutangazia Umma kuwa kamati yake iliisetiri serikali isiwe uchi kwa kutoanika yote. Je na wao walikosa ujasiri na kuogopa hasara pamoja na kupoteza maisha ?
sasa watu kama hawa wakisoma hapa tunajaribu kuwaita mafisadi kwa kujaribu kupiga vita ufisadi bila misingi yoyote ile ,inasikitisha kutia huruma na kukatisha tamaa kwa wale wanaotaka kudhubutu.
Katika vita walivyojaribu kupiga dhidi ya ufisadi wameweza kufanikiwa kwa kiwango gani ? Ninavyojua walioitwa mafisadi wako pale pale na akina Mwakyembe wanaendelea kula na kuishi nao. Sana sana tunaweza kusema ufisadi ndani ya CCM umeshinda kwani makamanda wao bado wamejipanga vile vile walivyokuwa toka mwanzo.
Mzee Mengi kutoa msaada kwa walemavu na kusema ana clandestine motive bila ushaidi ni kutaka kuondoa neno MSAADA kwenye kamusi.
Wewe mwenyewe mwanzoni umedai akina Mzee Mengi wameamua kukaa kimya baada ya kutambua hii vita si lelemama na yahitaji ujasiri mkubwa, sawa ? Je unataka kutuambia kuwa hao unaowatambua kama mafisadi hawatoi misaada ?
Bill Gates anapotoa msaada wa nyandarua sijui na yeye ana Motive gani? Mambo kama haya yatamfanya kila mtu awe fisadi.
Kwa hiyo Bill Gates unamweka kundi moja na Mengi, kaazi kweli kweli !
 
Nina wasiwasi kama kweli unaelewa maana ya unafiki - sasa ngoja nikusaidie kwa kukupa mfano - mtu anayelaumu utendaji ndani ya serikali lakini anamsifu kiongozi anayeiteua na kuiongoza serikali hiyo hiyo ni mnafiki, upo ?
Unafiki ninaongelea hapa, baadhi tunapiga kelele kuhusu ufisadi usiku kucha na upande mwingine tunawapiga vita hao wanaopiga vita ufisadi, huo ndio unafiki ninaosema mimi.Mwakyembe na wenzake wamedhubutu kupiga vita ufisadi,sasa kujaribu kuwaita nao ni mafisadi bila ushaidi wowote, huko ni kujaribu dhoofisha hiyo nguvu ndogo ya kupiga vita ufisadi.

Hizi tuhuma unazitoa wapi ama umesoma wapi kwamba Mengi analaumiwa kwa kupokea malipo (kutoka kwenye kodi zetu) lakini hafanyi kazi ya kupiga vita ufisadi. Kwanza huyo Mengi alipwe na nani na kwa nini alipwe - haya unayatoa wapi.
Tafuta maana ya neno "kana kwamba" au labda umelifumbia macho kupindisha maana.

Aha, kwa hiyo Mengi moto aliouwasha dhidi ya mafisadi ameuzima kwa kusalimu amri ili asipate hasara na kupoteza maisha. Wahenga husema if you cant fight them, join them na kwa maana hiyo Mengi amebwaga manyanga na sasa anakula nao bila wasi wasi tena. When the going gets tough, the tough keep going mfano wa shujaa Dr. Slaa!
Hili ndio tatizo, kujiona kwamba sisi tuna haki ya kukaa kimya na wengine wachache haki yao ni kupambana na mafisadi.
Sawa, wengine mchango wetu ni kuwapigia kelele hao mafisadi kwenye jukwaa letu nyuma ya keyboard kama Mengi naye alivyofanya kwa kutumia vyombo vyake. Tofauti ni kuwa sisi tunaendeleza mapambano, yeye mmmh.!
Kwa nini unafikiria na yeye hayuko nyuma ya keyboard kama wewe au kwa sababu ni Mengi haruhusiwi.

Nakuomba ukumbuke kuwa ndege wanaofanana huruka pamoja. Itakuwaje watu mlale kitanda kimoja na kujifunika shuka moja halafu ubaki ukimnyooshea kidole mwenzio kuwa ni mchafu huku huondoki ? Ukisikia unafiki na kuganga njaa ndiko huko !!
Kwa maana yako, huko mbeleni tunaweza tusiwe na chama.Chama kikishakuwa na mafisadi wale wasiopenda ufisadi wahame na huko wanapohamia ufisadi ukianza wasiopenda wahame na sio kujaribu kukisafisha chama.Kwa wale wanaoona mbali mwisho itakuwa ni kuhama hama.

Wewe mwenyewe mwanzoni umedai akina Mzee Mengi wameamua kukaa kimya baada ya kutambua hii vita si lelemama na yahitaji ujasiri mkubwa, sawa ? Je unataka kutuambia kuwa hao unaowatambua kama mafisadi hawatoi misaada ?
Kwa matazamo wangu, Mengi kaamua kukaa kimya baada ya kugundua hana support

Kwa hiyo Bill Gates unamweka kundi moja na Mengi, kaazi kweli kweli !
Inategemea ni kundi gani unaongelea.Nisome tena,labda utaelewa kwa nini nimemwingiza Bill Gates.
 
Mengi anasubiri mpaka mtu atoke madarakani ndio azungumzie mabaya yake.
 
Unajua hata mimi najitahidi sana kutafakari kila siku kuwa
...endapo fisadi anakuja na vibilion vyake kisha ananiambia kamata hizi ila achana na hiyo palanja-palanja yako kutusakama et all....
walah am still thinking what to do!
Sihongeki wala sinunuliki. Ila nawaza jinsi jamii itakavyoniamini kwamba nimehongwa kunyamaza. (hicho ndo kinachowasibu wapambanaji wengi)
 
Tunaelekea wapi?
Tusiwe vibaraka wa wanaopinga ufisadi au mafisadi wenyewe.
UFISADI NI ADUI NO.1 KWA WATU WENYE AKILI NZURI!
 
Moto wa Mengi waliumwangia...maaa...maji aise! mbulaaaaaaa! ITV saa nyingi kijani na njani humo ati!
 
Mengi ni fisadi kama walivyo kina Rostam, anachofanya ni kutafuta ulaji, kama kweli anapigania maslahi ya watanzania angepigania uhuru wa vyombo vya habari, isitoshe kama kweli yeye ni mzalendo mbona halipi mamailioni ya pesa alizokopa kwenye mabenki yetu. Mengi acha unafiki!!!!!!!!
 
Kuona jinsi vyombo vyake habari – ITV na magazeti yake vinavyokikumbatia chama tawala kwa lengo la kuona kinavigaragaza vyama vya upinzani, ningemshauri mmiliki Mzee Mengi abadilishe msimamo huo na kurejea upande wa haki – upande wa wananchi wengi walio wanyonge.

Huu msimamo alionekana kuwa nao pale alipowatangaza mafisadi papa takriban miaka miwili iliyopita.

Yaliyonisukuma kusema haya ni jinsi vituo vyake vya TV viwili ITV na EATV vilivyoripoti live leo hafla ya mjini Nairobi, Kenya ya utiwaji saini wa Katiba mpya.

Nilijiuliza, hivi Mzee Mengi haoni kwamba kuna umuhimu kwa Watanzania nao kuwa na Katiba mpya? Anatoa mchango gani kupatikana kwa ndoto hii?

Kuhusu vita dhidi ya ufisadi – inaonekana Mzee Mengi kaikimbia kambi na kuwaacha wanyonge aliyokuwa nawasemea kwenye mataa. Sababu yake bado siijui, kwani anaogopa nini? Kwani naye huenda si msafi? Sababu nyingine siioni hapa, labda nijuzwe.

Na ninaposema kurejea kwenye upande wa haki simaananishi kwamba ajisimike upande wa upinzani, la hasha. Angalau achukuwe sehemu ya kati, ingawa kufanya hivyo pia ni kuonekana kuukimbia upande ule anajua haki inaposimama.

Yule muzee, hakuna kitu kabisa, ndio maana alitetemeshwa na mtu mdogo ndani ya ccm kama kirumbe ng'enda!!! Alikua akichochea mgawanyiko ndani ya ccm, na walipomtisha kua hawamtambui kama mwanachama wa ccm alitoa kamasi akam mtoto mdogo... Kwa maneno mengine ni kuwa huyu jamaa haweza kufanya biashara akiwa hana kadi ya ccm!! Hivyo ile kadi kwake ndio mtaji mkubwa zaidi kuliko chochote aliconacho.....
 
Kuona jinsi vyombo vyake habari – ITV na magazeti yake vinavyokikumbatia chama tawala kwa lengo la kuona kinavigaragaza vyama vya upinzani, ningemshauri mmiliki Mzee Mengi abadilishe msimamo huo na kurejea upande wa haki – upande wa wananchi wengi walio wanyonge.

Huu msimamo alionekana kuwa nao pale alipowatangaza mafisadi papa takriban miaka miwili iliyopita.

Yaliyonisukuma kusema haya ni jinsi vituo vyake vya TV viwili ITV na EATV vilivyoripoti live leo hafla ya mjini Nairobi, Kenya ya utiwaji saini wa Katiba mpya.

Nilijiuliza, hivi Mzee Mengi haoni kwamba kuna umuhimu kwa Watanzania nao kuwa na Katiba mpya? Anatoa mchango gani kupatikana kwa ndoto hii?

Kuhusu vita dhidi ya ufisadi – inaonekana Mzee Mengi kaikimbia kambi na kuwaacha wanyonge aliyokuwa nawasemea kwenye mataa. Sababu yake bado siijui, kwani anaogopa nini? Kwani naye huenda si msafi? Sababu nyingine siioni hapa, labda nijuzwe.

Na ninaposema kurejea kwenye upande wa haki simaananishi kwamba ajisimike upande wa upinzani, la hasha. Angalau achukuwe sehemu ya kati, ingawa kufanya hivyo pia ni kuonekana kuukimbia upande ule anajua haki inaposimama.
Nilipoweka nyekundu kwenye post yako na hizo posts hapo chini nilipoweka nyekundu pia zitakupa picha ya jibu lako.Inashangaza na Kusikitisha unaitwa fisadi kwasababu unapigania haki za wanyonge.
Mkuu Nguruvi, kwa kiasi kikubwa nakubaliana na hayo uliyoyaandika hapo juu, na nimekugongea "kasanks".
Lakini nimjuavyo Mengi (nothing personal against him), kila analilofanya lazima kuna clandestine motive nyuma yake. Nasema hili from my personal experince kwenye interactions kadhaa naye.
Kuonekana kuwajali siju walemavu au media campain against akina Mkapa, Masha, nk is a cosmetic gimmick only - anataka watu wamuone he's doing it for the right course wakati deep down kuna ulterior samsing.

Hakuwa anapigana vita na mafisadi alikuwa anapigana vita ya kibiashara!

Back
Top Bottom