Moto aliodai kuuwasha Reginald Mengi dhidi ya mafisadi ulizima au ulizimwa?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,060
22,755
Ukimya wa Reginald Mengi wa IPP, aliyewahi kuapa hapo nyuma kuwa moto aliouwasha dhidi ya wahujumu na mafisadi wa nchi hii kamwe hautazimika, unatisha. Kwa mbali nakumbuka hotuba ya Jakaya Kikwete kwa wazee wa Dar es Salaam kuwa waliotaka kuleta mdomo wameshashughulikiwa na sasa wako kimya.

Je Reginald Mengi ni moja wa hawa watu walioshughulikiwa kimya kimya na sasa kapoa kama kamwagiwa maji ya friji. Kama hii itakuwa ni kweli, tumweleweje huyu Reginald Mengi, alikuwa ni mpiganaji wa kweli au wa kuchonga kama wale wachumia tumbo waliokuwa wakipayuka bungeni na kujiita wapiganaji ndani ya CCM ?

Wote aliodai amewawashia moto bado wanatamba na kusonga mbele lakini yeye pamoja na magazeti yake kimya. Hii ni sababu kubwa na tosha kwa wazalendo kuutambua ujasiri wa mpiganaji Dr. P. W. Slaa ambaye ameweza kusimama kidete kukabiliana na makombora ya mafisadi na vibaraka vyao ndani ya CCM na serikalini bila kutetereka.

Tumuunge mkono Dr. P. W. Slaa, tuung'oe huu utawala wa kifisadi.

Mengi ameptima maji na akagundua kwenye ile vita alikua pekee, wengi wetu ni wapiga debe tu kwenye mitandao na mitaani... leo tukiambiwa tusimame tupinge ufisadi, tunakua bize

Charity starts at home
 
Mengi hajawahi hata siku moja kuwa serious kuhusu maslahi ya taifa hili zaidi ya maslahi yake binafsi.
Personality ya Mengi ni "umimi" kama watu hawamjui.
 
Moderator ungeweka button ya kum UNTHANK mtu ningeitumia kwa huyu M-mbabe.
 
Huwezi ukawa ndani ya CCM then ukawa mpiganaji wa ufisadi.

Mengi mara amsifie JK bila kutoa sababu za msingi.

Yuko kimaslahi zaidi
 
Nadhani kuna wadau walikanyaga nyaya sasa akawa anakosa mawasiliano. Alipokoroma kidogo walisogea pembeni na mawasiliano yakawa msuano
 
Ukimya wa Reginald Mengi wa IPP, aliyewahi kuapa hapo nyuma kuwa moto aliouwasha dhidi ya wahujumu na mafisadi wa nchi hii kamwe hautazimika, unatisha
Tumuunge mkono Dr. P. W. Slaa, tuung'oe huu utawala wa kifisadi.

Mengi vuvuzela tu, kazeni kamba hakikisheni Slaa anapata kura za kutosha!
 
mag3
mengi aliuwasha moto lakini moto wenyewe ulikuwa hauna wakokeaji
moto wenyewe ulikuwa unamtegemea mengi aukokee

je kuna mtu alimsaidia mengi kuhakikisha moto ule unaendelea kuwaka??????
 
Ukitaka kujua Mengi ni mtu wa aina gani basi angalia jinsi ambavyo TV yake ilivyocover tukio lililotokea Jumamosi. Ufisadi wa habari uliofanywa na vyombo vyake siku ya Jumamosi unazungumza mengi kuhusu Mengi's character. Tuache utani jamani, kama mtu anashindwa kuripoti news hatawezaje kupambana na mafisadi?
 
Mengi ameptima maji na akagundua kwenye ile vita alikua pekee, wengi wetu ni wapiga debe tu kwenye mitandao na mitaani... leo tukiambiwa tusimame tupinge ufisadi, tunakua bize

Charity starts at home
Hakuwa anapigana vita na mafisadi alikuwa anapigana vita ya kibiashara!
 
Mengi ameptima maji na akagundua kwenye ile vita alikua pekee, wengi wetu ni wapiga debe tu kwenye mitandao na mitaani... leo tukiambiwa tusimame tupinge ufisadi, tunakua bize

Charity starts at home

Tuelewe kuwa Dr Slaa pamoja na ujasiri wa kizalendo alionao lakini ana ''immunity''. yeye ni mbunge na ni katibu mkuu kwahiyo kauli zake huwa zipo katika capacity hiyo. Mengi ni raia kama wewe na mimi, lakini tusidharau mchango wa vyombo vyake vya habari. Kuna gazeti lake la kiingereza limetufunua sana macho, lina habari na data zisizopingika, muulizeni Masha.
Tatizo letu tunadhani haya ni mapambano ya wateule fulani, si kweli. leo kila mtu anasubiri Slaa atasema nini, ukweli ni kuwa sisi tuna wajibu na ukaribu mkubwa sana na jamii kuliko Dr peke yake jukwaani. Ni lazima tuwaeleze watu wetu nchi ilipotoka , ilipo na inapokwenda.
Mimi naanza na ninyi, Kila atakayesoma habari hii amueleze ndugu yake kuwa baada ya miaka 50 ya uhuru ifuatayo ni shule ya watoto wetu, huku mtu mmoja akijengewa hekalu la bilioni 2 zaidi ya thamani ya kijiji chote. Tuwaeleze watu kuwa kofia/kanga na vitenge havitawakomboa, bali uthubutu,ujasiri na uamuzi mgumu dhidi ya mazoea ndio jibu litakalo wakwamua.

aisee....
 
Jamani, Ebu tuwe tofauti na wale wanaoliona suala la kushinda au kushindwa katika uchaguzi huu ni la Dr. Slaa kama Slaa na si kama ukombozi wa Wananchi na nchi kwa ujumla. Tunajiweka kando tukingoja matokeo ya kuumia kwa wengine ili tuwahukumu badala ya kushiriki harakati pamoja. Kwa ufupi, shame-upon us all kwa Kushindwa kwa Mengi!
 
Mengi kama mwananchi yeyote Mtanzania alitumia haki yake ya msingi kutoa dukuduku lake juu ya watu aliowaita Mafisadi papa na akawataja kwa majina.Baada ya matamshi hayo,baadhi ya walioshutumiwa waliweza kujitetea kwa kupitia vyombo vya habari na wengine walitishia kufungua mashtaka.Siwezi kujua upande wa serikali walilichukuliaje jambo hilo,ila Mengi alikuwa anawafahamu fika wafanyabiashara hao kama mmoja wa wanachama wa chama cha vigogo wa biashara nchini.Mwamuzi wa tuhuma hizo hakujitokeza,labda Mzee Mengi alijikuta yu pekee yake,ikambidi aachane nayo na kushughulika na mambo mengine.
 
Mengi alivamia vita bila kujua anapaswa kuwa upande gani....hvyo bahati mbaya akaingia upande wa maadui,lakini alipogundua haraka sana akarudi upande wake kabla upande wa maadui haujaangamizwa-ndio maana zile mbwembwe hazipo tena,kasharudi mulemule hivyo hawezi kuangamiza wenzake
 
Back
Top Bottom