Most fascinating people of 2009

Kwame Nkrumah

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
886
376
We have about 2 weeks remaining before the start of the New Year.
This is a list of most fascinating people in Tanzania for 2009. Watu hawa wamebadilisha kwa kiasi fulani mwelekeo wa nchi, au fikra zetu. Ni watu waliojadiliwa sana mwaka huu. Pia kwa namna moja au nyingine wametufurahisha ama wametuudhi , wamechangia kulipeleka taifa letu mbele au wameturudisha nyuma. Na wengine wamefanikiwa sana katika nyanja zao, and therefore have an impact on all of us.

10: JK.
Mwaka huu Mheshimiwa. Alikuwa Rais wa kwanza kutoka Africa kuonana na Rais Obama. Though it is hard to say what we
gained from this meeting, but it is also hard to argue that our President had his fifteen minutes of fame on the global arena from this meeting. Pia kulikuwa na maswali mengi kuhusu afya ya rais wetu , lakini ripoti iliyotelewa na daktari wake baada ya kupoteza fahamu Mwanza inaonyesha kuwa Rais ni mzima na buheri wa afya. JK pia ameendelea kusifiwa kwa kuendeleza uhuru wa kukosoana na uhuru wa vyombo vya habari kuliko ilivyokuwa awamu ya tatu.
Lakini pia picha yake ya kubembea huko Jamaica imekuwa gumzo lisiloisha hasa ikizingatiwa kwamba faida za ziara hiyo kwa walipa kodi hazijawekwa wazi.

9: YOU. Yes, you JF members.
Kwa kuchangia mawazo yako kwa ustaarabu, bila matusi, udini,vitisho wala mikwaruzo. Kuendeleza mapambano ya kuinua jamii yetu,kupashana habari, kuburudisha na hata kupeana nafasi za kazi. Kwa wale ambao waliteleza , najua mwakani watakuwa wanachama wazuri. Tusisahau pia kuchangia JF. Mkono Mtupu haulambwi…lol…

8: ENIGMA:
Who is Ka-nzi? How does he/she do it? Why is Ka nzi not here all the time like some of us? Powerful people in our corridors of power shake in their boots for fear of Enigma. Kwa kuleta uchunguzi ambao unajadiliwa mpaka Bungeni.

7: MATEO QARES:
For finally naming names. Kwa kupeleka lawama sehemu inayostahili. Kutaja wazi kwamba Rais ameshindwa kazi na CCM ichague mwanachama mwingine kugombea mwakani. Watu wengine wote wanasema “rais ana washauri wabovu”. But Hon. Qares had enough courage to put blames on the very top echelons of power where it belongs.

  • SOFIA SIMBA
Kwa kushinda uchaguzi wa UWT. Kuendeleza mipasho katika shughuli za serikali. Kumuita Lowassa “ mwanaume wa shoka” kwenye kikao muhimu kinachoamua mambo muhimu ya kitaifa. Kujibu hoja kwa mipasho.Katibu wake Mkuu wa UWT amemtaja kwa kukwamisha mradi wa kuku hadi apate ten percent Kwa kutajwa kuwa na degree fake na hivyo kutokuwa na sifa za uwaziri.

5: Mh. ANNA KILANGO.
Kwa kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi bila woga hata kutunukiwa tuzo.

4: HASHEEM THABEET.
Whether you are a sports fan or not. Hasheem ameweka Historia katika nchi yetu kwa kuwa the first NBA player from Tanzania. It is hard to predict what impact he is going to have for his team or NBA in general this early, lakini ameifanya Tanzania kujulikana zaidi. Katika mechi zake za College tumeshuhudia mara kadhaa wakionyesha Serengeti, Mt. Kilimanjaro na hata Dar-es-salaam. That was a lot of free publicity for our country.

3: JOHN POMBE MAGUFULI:
Kwa kufanya ambacho hakijawahi kufanywa toka tupate uhuru, protecting our Exclusive Economic Zone.
Meli moja tu imekamatwa na maliasili ya Tshs. 2 billions.Je ni meli ngapi za kiharamia zinaiba maliasili zetu kwa wiki, mwezi, mwaka, miaka na hata miongo kutoka Uhuru???Cha ajabu ni kwamba muda wote uliopita kulikuwa na watu ambao walikuwa na cheo kama cha Magufuli, majukumu yaleyale,na tuliwapa magari, madereva, mishahara minono, nyumba nzuri karibu na beach na hela nyingi tu za semina ili wajifunze kazi na kupanga mipango mizuri…….lakini wapi…….najiuliza walikuwa wanafanya nini kila siku wakienda kazini? Changamoto aliyonayo sasa ni kuhakikisha kwamba maliasili za baharini sasa zinaanza kuchangia katika pato la taifa kwa kiwango cha kuridhisha.


2……



1: VICKY NTETEMA.
Anyone at anytime who is willing to put his/her life on line for the love of his/her country should be applauded by all of us.
Vicky is the ultimate symbol of excellence in journalism. Vicky anaingia katika list hii kwa kufanya uandishi wa uchunguzi uliobobea dhidi ya mauaji ya albino na kuupasha ulimwengu juu ya uovu huu. Alifanya yote haya licha ya vitisho vya kuuwawa na licha ya Waziri mhusika kukana kwamba kuna mauaji yanaendelea. Kwa kiasi kikubwa ni juhudi zake binafsi zilizopekea kupungua kwa mauaji haya na kusukuma serikali kuchukua hatua.


Namba 2 nimekuachieni wadau. Feel free kushauri nani aongezwe kwenye orodha au nani aondolewe, na kwa nini.








 
2. ABEID AMANI KARUME na Maalim SEIF SHARIF HAMAD
.........kwa kukubali kwa njia ya mazungumzo kwamba hakuna kitu kibaya katika maisha ya mwanadamu kama kuchezea amani na umoja katika nchi. wametambua kwamba wote lengo lao moja, kuwaongoza wazanzibari katika misingi ya amani na utulivu.
ALUTA CONTINUA
 
2. ABEID AMANI KARUME na Maalim SEIF SHARIF HAMAD
.........kwa kukubali kwa njia ya mazungumzo kwamba hakuna kitu kibaya katika maisha ya mwanadamu kama kuchezea amani na umoja katika nchi. wametambua kwamba wote lengo lao moja, kuwaongoza wazanzibari katika misingi ya amani na utulivu.
ALUTA CONTINUA

Ni kweli, atleast wameanza kuzungumza, hata hivyo makubaliano bado hayafikiwa, ni mwanzo mzuri hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika uchaguzi mkuu.
 
Back
Top Bottom