Mossad na jaribio la mauaji ya Waziri Mkuu, Golda Meir ndani ya Rome

hao BLACK SEPTEMBER na PLO mbona siku hizi hawafanyi matukio au wote wameuwawa...

makundi hatari yanayosikika ni alshabab, boko haram, IS nayo yamejikita ktk ugaidi na sio ujasusi...
 
Huwa napenda sana kusoma
Mambo kama haya mkuu hakuna
nyingine ushushe tena
Pitia youtube ukiwa na bundle la kutosha utazame mambo ya ajabu juu ya uzalendo wa watu kwa nchi zao. Uzalendo wako utaongezeka maradufu kwa nchi yako mkuu!
 
Mpango huo uliandaliwa na magaidi wa Black September, baada ya kugundua ziara ya Meir kwenda Rome Italia kukutana na Pope Paul VI, January 1973, ziara hiyo ilitayarishwa kwa usiri mkubwa na Serikali ya Israeli. Lakini siri hiyo inashukiwa kuvujishwa na padri wa kipalestina aliyekua kwenye jopo la uongozi ndani ya Vatican.

Kamanda wa Black September aliyejulikana kama Ali Hassan Salameh alipanga kuishambulia ndege ya Waziri Mkuu Meir mara tu baada ya kutua Rome, lengo lake likiwa sio kumuua tu Meir bali mawaziri pamoja na maofisa wa Mossad alioongozana nao.

Wakati huo huo Salameh alikuwa kwenye negotiations na Warusi ili apate sehemu salama ya muda ndani ya Urusi kwa ajili ya hilo shambulizi la Rome, lengo likiwa baada ya shambulizi na wakati Mossad wana recover kutoka kwenye shock wenyewe wangekuwa salama nchini Urusi na mbali ya mikono ya Mossad.

Black September walifanikiwa kuingiza kwa siri baadhi ya shoulder launcher (strela 2 missiles) ndani ya Bahari, Italy, kutokea Dubrovnik, Yugoslavia kwa njia ya boat na baadae zilisafirishwa kwa siri mpaka Rome na kuwekwa pande tofauti katika uwanja wa Fiunicino Airport muda mfupi kabla kuwasili Waziri Mkuu, Golda Meir wa Israel.

Ili kuwachanganya na kuwahamishia akili kwingine, Samaleh alipanga shambulizi la kigaidi kwenye ubalozi wa Israel huko Bangkok, Thailand. Desemba 28, 1972 magaidi wanne wa Black September waliuteka ubalozi huo jijini Bangkok na kushikilia mateka 12 kisha walipandisha bendera ya PLO na kutishia kuua mateka wote endapo madai yao ya kuachiliwa wafungwa 36 wa PLO yasingesikilizwa.

Haraka sana jengo hilo lilizungukwa na askari Jeshi na Polisi wa Thailand, Mpango wa kuwakomboa mateka uliwekwa mezani nchini Israel lakini baadae wakauweka pembeni kwa kuamini kuwa sehemu jengo lilipo ni center na population ni kubwa, kwa Thailand hawatakubali kuwepo kwa kuvamia.

Hata hivyo madai yao hayakukubaliwa na mwisho waliahidiwa kuondoka salama endapo watakubali kuwaachia mateka salama walikubali na walielekea Cairo. Mossad waligundua mpango wa kuuawa Meir January 1973 baada ya mfanyakazi wa simu operator kuwataarifu Mossad kwamba alishughulikia simu zilizopitia kwenye kibanda cha simu cha kulipia(pay phone) katika nyumba ambayo hukaliwa na wanachama wa PLO.

Simu zilikuwa kwa lugha ya kiarabu na ziliongelewa ki msamiati (coded) mpigaji alisema "ni muda wa kuwasilisha mishumaa kwa ajili sherehe ya kuzaliwa" habari hii ilipomfikia mkurugenzi wa Mossad, Zvi Zamir alihisi hilo lilikua ni agizo la siri kwa shambulio lililopangwa kufanywa.

Zamir pia alihisi shambulio la Bangkok lilipangwa kuelekeza attention yao kwingine wakati shambulio likitekelezwa. Hapa aliona mwanga kutokana na magaidi wa Black September wanavyofahamika kwa uwezo wa fedha na mbinu. Alijumlisha moja na moja akatoka na mbili.

Pia ali tafakari kuhusu candles ni aina gari ya silaha baadae akailinganisha na rocket, baada ya tafakari na kuunganisha na tour ya Golda Meir Italy, walikuwa hawana shaka Black September walipanga kuilipua ndege ya Meir pindi itakapotua Rome.

Zamir aliamua kumtuma field officer kwenda Rome, na yeye akachukua team ya Mossad agents na kuelekea Rome. Zamir alikutana na mkuu wa kitengo cha Anti terrorists wa Italy na kumuelezea wasiwasi wake, walielekea kwenye nyumba husika na kuivamia: ile nyumba waliyokuwa wanaishi wanachama wa PLO: waliisachi na walipata menu tu za Kirusi zilizokuwa zinaelekeza jinsi ya kutumia rocket lakini hakukuwa na ushahidi wowote kuhusu mpango unaohusisha mpango wa mauaji ya Meir.

Asubuhi ya kuwasili Meir, Mossad Agents na anti terrorist wa Italy waliuzunguka uwanja wa ndege. Wakati wakiwa kwenye patrol, agent mmoja wa Mossad aliiona fiat van ikiwa imeegeshwa sehemu lakini imeelekezwa kwenye runway ya ndege ndipo alikwenda na kumtaka dereva atoke nje, ghafla mlango wa nyuma ulifunguka na magaidi wawili walitoka na kuanza kumfyatulia risasi agent wa mossad ambae ali side dive na kuwapiga risasi zilizowajeruhi vibaya, wakati huo dereva alichomoka na kukimbia akafukuziwa na agent mwingine, jamaa baada ya kuona hali mbaya akaenda na kusimamisha gari kwa mtutu ili aiteke atokomee, hakujua kwamba alijaribu kuiteka gari ya Mossad iliyokuwa patrol akanaswa kiulaini.

Jamaa alichukuliwa mpaka kwenye lori walilokuwa wanatumia Mossad kama command post yao na kumpa jamaa kipigo heavy mpaka akawaeleza ilipo team ya pili ya missile jamaa waliondoka speed waliiona cafe van sehemu imepaki huku roof yake ikiwa wazi na missile tatu zikionekana kuelekea angani jamaa waliifuata na kuivaa ubavuni na kuipindua na kuwaminya jamaa ndani ya van ili kutoa muelekeo wa missile angani. Dereva na watu waliokuwemo walitolewa wakiwa hawana fahamu, ndipo Italian anti terrorists walipoarifiwa kwamba "kuna ajali ya kuvuta hisia na wangependa kuiona" Zamir alisema baadae kwamba alitaka kuwaua magaidi wote palepale, lakini ingeweka doa kwenye kukutana kati ya Golda Meir na pope paul VI.

Magaidi walipelekwa hospitali, baadae walielekea Libya ndani ya miezi kadhaa wote waliuawa na mossad.
ntarudi baadae.......
 
Hvi hawa israel wanawezaje kusurvive hapo middle east kama kila jirani yao ni adui yao?
waisrael watakuwa wana-apply nadharia iliyomo ktk the law of the jungle:

"when ye fight with a wolf of the pack, ye must fight him alone and afar,
Lest others take part in the quarrel, and the Pack be diminished by war".
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom