Moshi Inatia aibu

Waungwana na wenyeji wa Moshi pamoja na sifa zote nzuri za Mji wenu, tatizo ni hilo tu la usiku mji kuonekana kama kijiji. Kubalini msikubali na kuna haja ya kulitatua hili. Taa zipo barabarani lakini hziwaki kamwe na wale mnaoropoka ropoka hapa, mie sizungunzii moshi vijijini huko, nazungumzia the town Center. Vitaa vinavyowaka ni vya majumbani kwa watu na hata mwanga wa barabarani unatoka kwa asilimia kubwa kwenye nyumba kando kando ya bara bara. Ninavyotambua Moshi si mji mdogo barani Africa. Lakini katika hili la kuuweka katiika mandhari nzuri ya usiku na mchana ni lazima wadau wa Moshi kulifanyia kazi.

Tusipende kuendeshwa na vionjo hata kama ni nyumbani kwenu. Swala la mgao halipo sasa ivi lakini wendawazimu watasingizia mgao wa umeme.

Ndio, Ndesa mbunge wenu kafanya makubwa hususani katika kusimamia barabara zinazoonekana. Sasa ivi CDM inongoza manispaa nadhani hili ni sehemu ya yale wanayoweza kuyafanya na kuacha legacy yao ndani ya mji huu.

Rai yangu, wakazi wa Moshi shirikianeni na viongozi wenu kuendelea kuuboresha mji wenu wa Moshi kwani mandhari ya mji wenyewe ni sehemu ya vivutio vya utalii. Badala ya wazungu kupanda mlimani wakishuka wanapaswa wawe na tamaa ya kuendelea kuspend dolari ndani ya mji huu badala ya kutamani muda ufike akakwee pipa kurea kwao alikotoka.

Nyie wachaga vipi?
 
Kwani kilichowaleta huku ni taa za barabarani?Kwa taarifa yako watalii vitu kama hivyo wameshavichoka huko kwao na ndio maana
huko porini wanapendelea hata kulala kwenye mahema.Kama ni taa si zingefungwa hata huko Serenegeti?Ukweli mimi si mwenyeji wa
moshi lakini Moshi iko juu.
 
Moshi ni mji wenye sifa ya usafi Tanzania. Zaidi ya usafi ni mji wa Mlima Kilimanjaro (The town of Mt Kilimanjaro) hivyo ni mji wa kitalii barani Africa. Pia mji huu uko kwenye mchakato wa kufanywa kuwa jiji na ndio maana umeshaanza kupanuliwa kieneo kwa kuchukua maeneo ya Moshi vijijini kama vile mabogini na Kahe.

Kinachotia aibu ni ifikapo mida ya saa moja usiku mji huu unakua giza totoro mithili ya msitu. Ni aibu kwa wageni wa ndani na nje ya nchi waingiapo ndani ya mji huu wanakumbana na kiza hiki.

Nimefika hapa kwa sherehe za kufunga mwaka na nimeona kuna haja ya CDM wanaoongoza manispaa hii kuufanya mji huu kuwa katika hadhi yake wakatii wa usiku na sio kama ilivyo sasa.

Sasa wewe unataka mwanga ili iweje? Hujaja kwenye sherehe wewe una lako jambo , next time njoo na genereta fal we
 
Mimi kama mwenyeji wa huko nakuunga mkono. Ni kweli kuna haja ya kuboresha kwa kuweka taa za barabarani. Tuangalie nguvu ya hoja ya huyu jamaa.
 
theluji ya kilimanjaro inatosha kutoa mwanga,moshhi sio las-vegas.
 
Wanabodi,

Mleta sredi ametoa changamoto nzuri ingawa ametia chumvi zaidi. Moshi is a "sleepy" town, hakuna activity nyingi pale mjini kati nyakati za usiku. By saa mbili usiku mjini kati hakuna watu pale, wamekwenda Machame, Kibosho, Rau, Njoro, au Pasua na watarudi asubuhi. Taa usiku utamwashia nani? Just sayin'!!.

By the way niwape high five MMC kwa kazi nzuri pale Uhuru Park. Nadhani Moshi inakuwa mji pekee wenye proper and well maintained public park. Ndio bado kazi inahitajika lakini they deserve a clap for that.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom