BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi limeanza kazi kwa kufanya mapinduzi makubwa kwenye bajeti yake ikiwamo kupunguza matumizi kwenye mambo yasiyo ya lazima huku ikiazimia kuwalipia ada wanafunzi wote wa shule za sekondari za kutwa.
Matumizi yaliyopunguzwa ni yale ya ofisi ya meya kutoka shilingi milioni 16 zilizotengwa kwenye bajeti ya mwaka 2010/11 hadi shilingi milioni 4.7 kwenye bajeti ya mwaka 2011/12.
Katika bajeti hiyo, kiasi kikubwa cha fedha kimepunguzwa kwenye fungu la chai na vitafunwa kutoka shilingi milioni 10.3 mwaka 2010/11 hadi kufikia milioni 1.8 kwa mwaka 2011/12.
Wanafunzi wa sekondari 8,528 watalipiwa ada ya shilingi 20,000 kila mmoja itakayogharimu halmashauri hiyo kiasi cha shilingi milioni 170.5 huku wazazi wao wakitakiwa kulipia michango mingine ya shule ikiwamo kulipia wapishi, walinzi na huduma nyingine zinazotolewa kwenye shule hizo.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa manispaa hiyo Bernadette Kinabo, alipingana na uamuzi wa madiwani hao juu ya kuwalipia ada wanafunzi kwa madai kuwa inapingana na sera ya serikali inayowataka wazazi kuwalipia wanafunzi wao ada ili wajisikie wana uchungu na elimu ya watoto wao.
Je viongozi kama hawa kweli wapo kwa faida ya Taifa? Kama Halmashauri/nchi inakusanya mapato ya kutosha kwa nini wananchi wake wasifaidike na matunda ya kazi yao? Je kumuacha Mzazi apate uchungu na ugumu wa maisha na kuweka budget yote kwenye Chai na vitafunwa ndio halali ya sera za CCM?
Huyu mkurugenzi anawakilisha mtazamo na mawazo ya aliyemteua, Yani RAIS& Waziri Mkuu na sera zao za CCM.
Watanzania tuamke na kuwaondoa hawa wanyonyaji.
Source: Tanzania Daima
Kama ni bogus statement
Hongera Chadema pambaneni hadi watu waone clear differences between the two.
........Hata hivyo, Mkurugenzi wa manispaa hiyo Bernadette Kinabo, alipingana na uamuzi wa madiwani hao juu ya kuwalipia ada wanafunzi kwa madai kuwa inapingana na sera ya serikali inayowataka wazazi kuwalipia wanafunzi wao ada ili wajisikie wana uchungu na elimu ya watoto wao.
Source: Tanzania Daima........
Hongera CDM - Endelea kuonyesha njia.
mambo kama haya ndiyo cdm ilitakiwa at least ifanye toka mwanzo na siyo maandamano yasiyomsaidia mtanzania kwa sasa zaidi ya kuchochea chuki katika jamii. hapo madiwani wameonesha mchango wa mawazo yao na huyo mkurugenzi hatakiwi kupinga tu bila hoja labda yeye naye aseme hapana walipe ada lakini michango ya aina yoyote wao ndio watakao toa, maana wakuu kama mnavyojua shule za misingi ada ilitolewa lakini hiyo michango iliyopo imekuwa ni mara kadhaa ya ile ada waliyokuwa wanachangia. kwahiyo hilo nalo liangaliwe pia. maana isije ikaondolewa ada lakini michango ya wapishi wa chai na vitafunwa na walinzi ikawa mikubwa zaidi.lakini pia hao madiwani mawzo hayo kama yatafanya kazi yafikiriwe hadi ngazi ya A level kwani wasije fika huko wakakuta utaratibu huo wa kulipiwa haupo wazazi wakagoma kutoa ada.
You are absolutely right Mkuu......................kuna sehemu nilisema hawa CDM ni kama sikio la kufa vile..............kuna vitu muhimu sana vinafanywa na CDM vya ku-capitalize na malengo yao..........lakini jamaa utaona wako kimya tu............
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi limeanza kazi kwa kufanya mapinduzi makubwa kwenye bajeti yake ikiwamo kupunguza matumizi kwenye mambo yasiyo ya lazima huku ikiazimia kuwalipia ada wanafunzi wote wa shule za sekondari za kutwa.
Matumizi yaliyopunguzwa ni yale ya ofisi ya meya kutoka shilingi milioni 16 zilizotengwa kwenye bajeti ya mwaka 2010/11 hadi shilingi milioni 4.7 kwenye bajeti ya mwaka 2011/12.
Katika bajeti hiyo, kiasi kikubwa cha fedha kimepunguzwa kwenye fungu la chai na vitafunwa kutoka shilingi milioni 10.3 mwaka 2010/11 hadi kufikia milioni 1.8 kwa mwaka 2011/12.
Wanafunzi wa sekondari 8,528 watalipiwa ada ya shilingi 20,000 kila mmoja itakayogharimu halmashauri hiyo kiasi cha shilingi milioni 170.5 huku wazazi wao wakitakiwa kulipia michango mingine ya shule ikiwamo kulipia wapishi, walinzi na huduma nyingine zinazotolewa kwenye shule hizo.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa manispaa hiyo Bernadette Kinabo, alipingana na uamuzi wa madiwani hao juu ya kuwalipia ada wanafunzi kwa madai kuwa inapingana na sera ya serikali inayowataka wazazi kuwalipia wanafunzi wao ada ili wajisikie wana uchungu na elimu ya watoto wao.
Je viongozi kama hawa kweli wapo kwa faida ya Taifa? Kama Halmashauri/nchi inakusanya mapato ya kutosha kwa nini wananchi wake wasifaidike na matunda ya kazi yao? Je kumuacha Mzazi apate uchungu na ugumu wa maisha na kuweka budget yote kwenye Chai na vitafunwa ndio halali ya sera za CCM?
Huyu mkurugenzi anawakilisha mtazamo na mawazo ya aliyemteua, Yani RAIS& Waziri Mkuu na sera zao za CCM.
Watanzania tuamke na kuwaondoa hawa wanyonyaji.
Source: Tanzania Daima
Aisee budget ya chai ya mil 10.3 kwa mwaka ni sawa na zaidi ya laki 8 kwa mwezi au 42,000/= kwa siku (Ada ya watoto 2). Hiyo Ofisi ina wafanya kazi wangapi ambao hutumia that amount per day?
Hongera CDM; mlistahili kuchukua nchi, now l can see ACTIONS loud and clear, sio maneno ya matumaini ya kila siku ya watu waliokulia kwebye Mipasho!
Kwani lini nilikuwa gamba wenye magamba wanajulikana.Heh leo vipi Quinine, umejivua gamba lini?
1. Hongereni Chadema kwa kuthubutu kupingana na uongozi-kwa-mazoea (business as usual)
2. Pamoja na hayo, kuna ukweli kuwa kutoa elimu bure siyo solution. Inajenga "sense of entitlement", yaani, dhana ya kuwa unastahili kitu kwa kuwa upo tu. Hii ni mbaya sana kwani;
- inapunguza juhudi ya wananchi kujitafutia. Juhudi za kujitafutia ndiyo uchumi wenyewe
- inapunguza thamani ya kitu kinachotolewa bure. Watu wanakichukulia poa
- unazoesha watu tabia mbaya ya utegemezi
Ushauri wangu ni kuwa hizo million 170.5 kwa mwaka, zingetumika kukarabati shule ili Moshi iwe na shule nzuri kuliko miji yote Tanzania ifikapo mwaka 2015. Kila mwaka karabati shule kadhaa.
3. Ukitaka kuona athari za hii dhana ya kustahili angalia viongozi wa sasa na mashangingi yao. Yaani mtu kwa kuwa tu ni mkurugenzi, basi hawezi tena kupanda land-rover. Au eti hawezi kutibiwa Mawenzi hospital ni lazima aende Morningside Hospital Sandton akatibiwe tumbo la kuhara. Siyo kwa sababu amefanya kitu kikubwa sana, la hasha, ni kwa sababu yeye ni yeye tu.
Tusiilete hi dhana kwa wananchi, kwani tupo wengi mno.
The Stig1. Hongereni Chadema kwa kuthubutu kupingana na uongozi-kwa-mazoea (business as usual)

The Stig
Una maana gani unaposema tusiilete hii dhana kwa wananchi hutaki wazazi wapate msaada, kama nchi zinazotupa misaada zingekuwa na mawazo kama yako kuwa zisitoe misaada kwa sababu nchi masikini nyingi budget yetu isingekuwa inatosha hata Quater moja.
Serikali ina budget ya maendeleo, ina pokea msaada chini ya mpango wa MMEM na MMES wa kuendeleza elimu (shule za kata) ikiwemo kuboresha majengo, mbali ya kupokea misaada kwa ajili hiyo Serikali haitimizi wajibu wake. Hadi sasa kwenye huo mpango hakuna sehemu iliyotengwa na serikali kwa ajili ya kulipia wanafunzi, wanachofanya Chadema ni kusaidia sehemu ambayo serikali haina hata wazo, inawasaidia wazazi kulipia ada za watoto wao. Ni kipi cha msingi kumsaidia mzazi au kuisaidia serikali inayotumia vibaya funds za maendeleo ikiwemo kuboresha majengo.
Nashangaa sana watu wenye mawazo kama yako akiwemo huyo mkurugenzi ni kama wivu fulani vile kwa sababu nyie mnauwezo wa kusomesha na kuwalipia watoto wenu nje sasa mkiona wazazi wengine wanawezeshwa ili watoto wao angalau wapate elimu ya msingi hampendi kwa kisingizio cha eti wazazi hawataona uchungu, inawezekana kabisa hata huyo Kinabo alipata elimu ya bure ina maana wazazi wake hawakuwa na uchungu kwa vile serikali ilimsomesha bure, ni mawazo mgando kabisa ndiyo maana nikayaita ni Bogus statement ya mwaka.
Aisee nimekuelewa mtazamo wako!:lying:
Umejikita kwenye hiyo na siyo rahisi kukutoa huko, tutaishia kujibizana tu.
Lakini ushauri wa bure (manake kwa dezo haujambo), NOBODY OWES YOU ANYTHING. Ukiishi unategemea misaada na kuwezeshwa utaishia kuwa mzigo kwa jamii. This country will become strong only when everyone is pulling his own weight and creating value. Wale mnaokaa vibarazani mnasubiri kuwezeshwa na kodi zilizokatwa kwa wenzenu wanaofanya kazi hamsaidii hili taifa.
pesa za halmashauri bado ni za wazazi kwani wao ndio walipa kodi!