BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi limeanza kazi kwa kufanya mapinduzi makubwa kwenye bajeti yake ikiwamo kupunguza matumizi kwenye mambo yasiyo ya lazima huku ikiazimia kuwalipia ada wanafunzi wote wa shule za sekondari za kutwa.
Matumizi yaliyopunguzwa ni yale ya ofisi ya meya kutoka shilingi milioni 16 zilizotengwa kwenye bajeti ya mwaka 2010/11 hadi shilingi milioni 4.7 kwenye bajeti ya mwaka 2011/12.
Katika bajeti hiyo, kiasi kikubwa cha fedha kimepunguzwa kwenye fungu la chai na vitafunwa kutoka shilingi milioni 10.3 mwaka 2010/11 hadi kufikia milioni 1.8 kwa mwaka 2011/12.
Wanafunzi wa sekondari 8,528 watalipiwa ada ya shilingi 20,000 kila mmoja itakayogharimu halmashauri hiyo kiasi cha shilingi milioni 170.5 huku wazazi wao wakitakiwa kulipia michango mingine ya shule ikiwamo kulipia wapishi, walinzi na huduma nyingine zinazotolewa kwenye shule hizo.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa manispaa hiyo Bernadette Kinabo, alipingana na uamuzi wa madiwani hao juu ya kuwalipia ada wanafunzi kwa madai kuwa inapingana na sera ya serikali inayowataka wazazi kuwalipia wanafunzi wao ada ili wajisikie wana uchungu na elimu ya watoto wao.
Je viongozi kama hawa kweli wapo kwa faida ya Taifa? Kama Halmashauri/nchi inakusanya mapato ya kutosha kwa nini wananchi wake wasifaidike na matunda ya kazi yao? Je kumuacha Mzazi apate uchungu na ugumu wa maisha na kuweka budget yote kwenye Chai na vitafunwa ndio halali ya sera za CCM?
Huyu mkurugenzi anawakilisha mtazamo na mawazo ya aliyemteua, Yani RAIS& Waziri Mkuu na sera zao za CCM.
Watanzania tuamke na kuwaondoa hawa wanyonyaji.
Source: Tanzania Daima