PAKA MAPEPE
Member
- Jul 20, 2012
- 19
- 0
Moto hauzimwi kwa kumwaga petroli.. mwisho wa CHUKUA CHAKO MAPEMA ( CCM ) UMEKARIBIA..
well said kamanda Makene, nimefarijika Moro kupita kwenye hilo Tanuru, wawe STRONG... safi sana poliCCM kwa kuzidi kutukomaza na kututoa woga wa kupigwa mabomu ya machoz. go on poliCCmNi kweli. Polisi wamevuruga maandamano yaliyokuwa yafanyike kwenda eneo la mkutano, Uwanja wa Ndege, hapa Morogoro Mjini. Wamedhalilisha viongozi waliowakamata na sasa wameanza kuomba samahani, yaishe.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Shilogile (mnaojua alihamishwa Dar es Salaam kuja hapa...) amevunja makubaliano yaliyofanyika mara mbili ya kuruhusu maandamano. Tunajua wapo wanasiasa hapa Morogoro ambao hawataki meseji ifike leo kwa wakazi wa Morogoro Mjini.
Inajulikana namna ambavyo CCM wamekuwa shaken big time na operesheni iliyokuwa na mafanikio huko vijijini, itawaumiza zaidi ikifanikiwa hapa mjini. Kwa hiyo lengo hapa si kuvuruga tu maandamano, bali ni kuvuruga mkutano, ili hatimaye watu waogope kuja mkutanoni, ujumbe usifike. Hawatafanikiwa kwa hilo, maana wananchi sasa wanazidi kujikusanya, maeneo kama ya Masika, kwenda eneo la mikutano, kwa maandamano.
Polisi wanachafua mji sasa, polisi wanawapitisha wana-Morogoro kwenye tanuru ambalo watu wa Mwanza, Mbeya, Arusha, Moshi, Musoma, Tarime, Ruaha na kwingineko kwingi, walipita/kupitishwa ili kuwa hapo walipo wakiwa na imani isiyoyumba katika mapambano haya ya kudai na kuwaandaa Watanzania kwa mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala. Chuma hakiwezi kuwa chuma mpaka kipite kwenye tanuru, lakini why doing it unnecessary?
Tutawapatia more updates on the issue?
Nguvu ya umma imeshinda mabomu ya polisi na mabavu ya polisi. Watu wameandamana na tayari wameshakusanyika eneo la mkutano, Uwanja wa Ndege. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Mussa Yusuf naye alikamatwa, lakini wamemwamchia. Bado wanamshikilia Kigaila, hawataki kumpeleka kituoni, badala yake wanazunguka naye ndani ya gari. Pia walimkamata mwandishi mmoja wa habari, kwa kupiga picha (sijui ni kosa?????), lakini naye pia wamemwachia.
Huo ni ujumbe tukiamua tunaweza kwa nguvu ya umma M4C forever!Nguvu ya umma imeshinda mabomu ya polisi na mabavu ya polisi. Watu wameandamana na tayari wameshakusanyika eneo la mkutano, Uwanja wa Ndege. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Mussa Yusuf naye alikamatwa, lakini wamemwamchia. Bado wanamshikilia Kigaila, hawataki kumpeleka kituoni, badala yake wanazunguka naye ndani ya gari. Pia walimkamata mwandishi mmoja wa habari, kwa kupiga picha (sijui ni kosa?????), lakini naye pia wamemwachia.
Nguvu ya umma imeshinda mabomu ya polisi na mabavu ya polisi. Watu wameandamana na tayari wameshakusanyika eneo la mkutano, Uwanja wa Ndege. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Mussa Yusuf naye alikamatwa, lakini wamemwamchia. Bado wanamshikilia Kigaila, hawataki kumpeleka kituoni, badala yake wanazunguka naye ndani ya gari. Pia walimkamata mwandishi mmoja wa habari, kwa kupiga picha (sijui ni kosa?????), lakini naye pia wamemwachia.
Mbunge mwarabu Abood ndio kalazimisha eti huo mkutanoM4C, usifanyike kwa garama yoyote!
swali; kwa nini polisi inatumiwa/ kuamuliswa na mtu yoyote hapa Bongo? mbunge na jeshi la polisi wapi na wapi?