Morogoro: Viongozi wa CHADEMA wakamatwa na polisi, vurugu zaibuka!

Hiyo nguvu ya kuutawanya umma bora ingetumuka kule kwenye mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania.
 
Kisa cha maandamano ni nini? au watu wanaelekea kwenye mkutano (M4C) na polisi wanawatawanya. Hivi hawa akina Mwema 2015 watakimbilia wapi?
 
Eeeee!!!Kimenuka wazee wa fataki wamelala mbele kama wakimbizi!!Kutetea Ccmagamba kunahitaji moyo!!Na sio kama wameishiwa ila wameelimika na wamegundua chadema ndo mtetezi wao na wanyonge wengine wa nchi hii!!Japo najua bado kuha wale waliopelekwa kwenye kazi hiyo na akina zombe watatafuta risasi za moto...
 
Mida hii nikiwa hapa morogoro mjini msamvu ambapo polisi wamewatia mbaroni viongozi wa CHADEMA akiwemo na BENSON KIGAAlA.

Subirieni taarifa zaidi.

Ni kweli. Polisi wamevuruga maandamano yaliyokuwa yafanyike kwenda eneo la mkutano, Uwanja wa Ndege, hapa Morogoro Mjini. Wamedhalilisha viongozi waliowakamata na sasa wameanza kuomba samahani, yaishe.

Kamanda wa Polisi Morogoro, Shilogile (mnaojua alihamishwa Dar es Salaam kuja hapa...) amevunja makubaliano yaliyofanyika mara mbili ya kuruhusu maandamano. Tunajua wapo wanasiasa hapa Morogoro ambao hawataki meseji ifike leo kwa wakazi wa Morogoro Mjini.

Inajulikana namna ambavyo CCM wamekuwa shaken big time na operesheni iliyokuwa na mafanikio huko vijijini, itawaumiza zaidi ikifanikiwa hapa mjini. Kwa hiyo lengo hapa si kuvuruga tu maandamano, bali ni kuvuruga mkutano, ili hatimaye watu waogope kuja mkutanoni, ujumbe usifike. Hawatafanikiwa kwa hilo, maana wananchi sasa wanazidi kujikusanya, maeneo kama ya Masika, kwenda eneo la mikutano, kwa maandamano.

Polisi wanachafua mji sasa, polisi wanawapitisha wana-Morogoro kwenye tanuru ambalo watu wa Mwanza, Mbeya, Arusha, Moshi, Musoma, Tarime, Ruaha na kwingineko kwingi, walipita/kupitishwa ili kuwa hapo walipo wakiwa na imani isiyoyumba katika mapambano haya ya kudai na kuwaandaa Watanzania kwa mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala. Chuma hakiwezi kuwa chuma mpaka kipite kwenye tanuru, lakini why doing it unnecessary?

Tutawapatia more updates on the issue?
 
Polisi naona wanaelekea kushindwa nguvu ya umma,Morogoro mnanipa raha kwa muamko huu!
 
Mbunge mwarabu Abood ndio kalazimisha eti huo mkutanoM4C, usifanyike kwa garama yoyote!
swali; kwa nini polisi inatumiwa/ kuamuliswa na mtu yoyote hapa Bongo? mbunge na jeshi la polisi wapi na wapi?
 
Kunafanyika maandamano ya m4c kutokea msamvu kuja mjini ni kufuru umati wa watu sijawahi kuona, HAPA NGOME YA CCM IMETINGISHWA
 
Ni kweli. Polisi wamevuruga maandamano yaliyokuwa yafanyike kwenda eneo la mkutano, Uwanja wa Ndege, hapa Morogoro Mjini. Wamedhalilisha viongozi waliowakamata na sasa wameanza kuomba samahani, yaishe.

Kamanda wa Polisi Morogoro, Shilogile (mnaojua alihamishwa Dar es Salaam kuja hapa...) amevunja makubaliano yaliyofanyika mara mbili ya kuruhusu maandamano. Tunajua wapo wanasiasa hapa Morogoro ambao hawataki meseji ifike leo kwa wakazi wa Morogoro Mjini.

Inajulikana namna ambavyo CCM wamekuwa shaken big time na operesheni iliyokuwa na mafanikio huko vijijini, itawaumiza zaidi ikifanikiwa hapa mjini. Kwa hiyo lengo hapa si kuvuruga tu maandamano, bali ni kuvuruga mkutano, ili hatimaye watu waogope kuja mkutanoni, ujumbe usifike. Hawatafanikiwa kwa hilo, maana wananchi sasa wanazidi kujikusanya, maeneo kama ya Masika, kwenda eneo la mikutano, kwa maandamano.

Polisi wanachafua mji sasa, polisi wanawapitisha wana-Morogoro kwenye tanuru ambalo watu wa Mwanza, Mbeya, Arusha, Moshi, Musoma, Tarime, Ruaha na kwingineko kwingi, walipita/kupitishwa ili kuwa hapo walipo wakiwa na imani isiyoyumba katika mapambano haya ya kudai na kuwaandaa Watanzania kwa mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala. Chuma hakiwezi kuwa chuma mpaka kipite kwenye tanuru, lakini why doing it unnecessary?

Tutawapatia more updates on the issue?

Tunashukuru kwa taarifa mkuu......Mungu yupo upande wenu daima......tunawaombea yasijetokea mauaji manake hawa police wa CCM akili zao zinawatosha wao wenyewe...... M4C daima!
 
Back
Top Bottom