Miguu imejikunja kutokana na kugusa chini na kwa njia hiyo mtu huwezi kufa hata wenzetu wahehe wanalijua hilo
Miguu imejikunja kutokana na kugusa chini na kwa njia hiyo mtu huwezi kufa hata wenzetu wahehe wanalijua hilo
Kifo hakina huruma Remmy aliimba enzi za uhai wake. Kwasababu kifo hakina huruma, sishangai kufa kwa huyu askari huku akiwa amepiga magoti.
Unajua damu ya mtu haipotei bure,na mungu huwa hapendi watu wake waangamizwe,hii inaonyesha jinsi gani hao jamaa wameacha nafasi kwa mtu yeyote mwenye akili kujua huyu jamaa hajajinyonga,haiwezekani nguo ichafuke kwa vumbi inamaana kuna kilichotokea kwanza kabla ya hapo.Na kwanini afe akiwa hajaning'inia mtini?Ila kwa nchi yetu litapita tu,ingekuwa kwa wenzetu ingechukua hata miaka kumi ila ukweli ungejulikana na wahusika wangelipia mabaya yao.
Huyu kamanda ninamfahamu, aliingia katika jeshi la polisi kama mcheza mpira na baadae akaacha mpira baada ya kiwango kushuka. Alichanganyikiwa kidogo baada ya kufiwa na mkewe aliekuwa anampenda sana. Alichanganyikiwa mpaka mwajiri wake akaamua kumpumzisha kidogo ili aweze kupona na kurudi kazini. Baadae aliokoka na kuanza kuelezea maovu yao (yeye na askari wenzake) waliyoyafanya kabla ya kuokoka. Viongozi wake hawakumuamini na kudhani kwamba bado amechanganyikiwa, baadae mambo yalivyozidi kuanikwa ndo akaanza kueleza mambo hayo kwa njia ya barua na kuzungumza na waandishi wa habari. Ninaamini kwamba alichoeleza kwenye barua yake hiyo ni kweli.
Hapa IGP na waziri wa mambo wa ndani wanahusika vipi? Kitendo cha mtu kujinyonga kinasikitisha sana hakuna mtu mwenye uwezo wa kuzuia kama mtu ametaka mwenyewe kuidhuru nafsi yake; sababu zipo nyingi ni udhaifu wetu binadamu kushindwa kukabiliana na matatizo yetu sioni sababu ya kumhusisha IGP na waziri wa mambo ya ndani na tukio hili utakuwa ni ufinyu wa fikra.
Chama
Gongo la mboto DSM