Morocco ilijulikana kama dola yenye ustaarabu katika Afrika ya Kaskazini

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,266
Eneo ambalo linajulikana kama Morocco ya leo lilianza kukaliwa na binadamu Enzi za Zama za Mawe (Paleolithic times), huo ulikuwa kati ya mwaka 190,000 na 90,000 BC. Eneo la Maghreb lilikuwa na rutuba sana tofauti na ilivyo sasa, eneo hili liliweza kulinganishwa na eneo la savannah lilivyo leo. Katika zama kati za mawe takriban miaka 22,000 nyenzo zilizotumika Morocco zilikuwa sawa na zile zilizotumika Oman.

Morocco ilijulikana kama dola yenye ustaarabu katika Afrika ya Kaskazini na Carthage ikikuwa ndani ya dola ya Morocco. Pia Berber Kingdom ya Mauretanaia chini ya mfalme Baga ilikuwa chini ya Morocco (usichanganye na Mauretania ya leo).

Chini ya utawala wa Emperor Claudius, Maurtetania ilikuwa chini ya utawala wa Roman Empire. Katika kipindi hiki watu wa makabila ya Berber waliweza kukomboa sehemu ya ardhi na jambo hilo lilimchanganya sana Emperor Claudius.

Uislamu ulianza kuingia Morocco katika kipindi cha karne ya 7 baada ya kuiteka Maghreb,ushindi huu ulikuja na lugha ya Kiarabu pamoja na dini ya Kiislam. Ingawa hii ilikuwa dola kubwa ya Kiislam, maamuzi yake yaliamuliwa Ifriquya ambalo ni eneo toka Tunisia mpaka Tripoli, na magavana waliteuliwa kutoka Kairouan.

Makabila ya Berber yalianza kufuata dini ya Kiislam lakini yaliendelea kushika sheria zao za jadi. Walilipa kodi kwenye serikali ya Kiislam. Ufalme wa Nekor ndiyo dola ya kwanza kujitangazia dola huru. Ufalme huu uliongozwa na Emir kutokea Emirate wa milima ya Rif. Milima hii iligunduliwa na Salih I ibin Mansur mwaka 710 kama dola shiriki ya Khalifa Rashidun. Watu wa makabila ya Berber walichachamaa na kuleta machafuko makubwa, hatimae waliweza kuanzisha dola zao kama vile Miknasa ya Sijilmasa na Barghawata.

Idris ibn Abdallah alikimbilia Morocco kufuatia mauaji ya ukoo wake Iraq. Alifanikiwa kuwashawishi watu wa makabila ya Berber kujitenga na utawala wa khalifa Abbasid kutokea Baghdada na kuanzisha Idris Dynasty mwaka 788. Utawala huu ulianzisha Fes kama mji wao mkuu na walifanikiwa kuigeuza Morocco kuwa kituo kikubwa cha elimu ya Uislamu pia kuwa eneo lenye nguvu kubwa. Ukoo wa Idriss ulitolewa katika uongozi mwaka 927 na khalifa Fatimid pamoja na washiriki wake wa Kiknasa. Baada ya hapo Miknasa walijitoa kutoka kwa Fatimids 932, ambao pia walitolewa na Maghrawa wa Sijilmasa 980.

Kutoka karne ya 11, mlolongo wa nguvu za ukoo wa Berber zimekuwa zikijitokeza chini ya Almoravid dynasty na Almohad dynasty Morocco ilichukuwa eneo kubwa la Maghreb, eneo hilo ni pamoja na Hispania na Ureno ya leo. Eneo la magharibi ya Mediterranea pia lilikuwa sehemu ya Morocco. Kuanzia karne ya 13 kuendelea kumekuwa na uhamiaji mkubwa wa Banu Hilal kabila la Waarabu. Katika karne ya 13 na 14 Merinids walishikilia dola ya Morocco na walipigana kufa na kupona kutoa nakala ya utawala wa Almohads kwa kutumia nguvu za jeshi ndani ya Algeria na Hispania, utawala huu ulifuatiwa na Wattasids. Katika karne ya 15 Reconquista alimaliza utawala wa Kiislamu katikati na kusini mwa Hispania, Waislamu na Wayahudi wengi walikimbilia Morocco.

Mnamo 1549 eneo la Morocco liliangukia katika utawala wa Arab dynasties unaosemekana unatoka katika ukoo wa mtume Mohammad. Ilianza Saadi dynasty iliyotawala kuanzia 1549 mpaka 1659, baadae ikaja Alaouite dynasty, ambayo ilikaa madarakani mpaka karne ya 17.

Chini ya utawala wa Saadi, nchi iliweza kuushinda uvamizi wa Ottoman (Uturuki ya leo) na pia ilishinda uvamizi wa Ureno na kushinda vita ya Ksar el Kebir mwaka 1578. Utawala wa al Mansur ulileta utajiri na heshima kwa Sultani. Kulikuwa pia na wimbi la mapigano kutoka Afrika Magharibi pamoja na kuanguka kwa Songhay Empire mwaka 1591. Hata hivyo, kumudu utawala wa eneo zima la Sahara haikuwa kazi rahisi baada ya kifo cha al Mansur. Hii ilipelekea nchi kugawanywa kwa watoto wake wa kiume.

In 1666, Morocco ilirejesha mahusiano na Alaouite Dynasty, ukoo uliotawala Morocco wakati wa mapambano na Hispania pamoja na Uturuki kwa upande wa Magharibi. Ukoo wa Alaouite ulifanikiwa kurejesha nafasi yao kwenye utawala katika kipindi ambacho ufalme ulikuwa mdogo lakini wenye mali nyingi. Upinzani kutoka makabila ya asili Ismail Ibn Sharif 1672 - 1727 alijenga urafiki na Jaysh d' Ahl al Rif na kwapamoja waliteka Tangier kutoka kwa Waingereza 1684 na kuiondoa Hispania kutoka Larache mwaka 1689.

Morocco ilikuwa nchi ya kwanza kuitambua Marekani kama taifa, wakati Marekani ikiwa taifa changa kama mtoto yatima 1777. Mwanzoni mwa mapinduzi ya Marekani, wafanyabiashara wa Marekani wakitumia meli kwenye bahari ya Atlantic walishambuliwa na
Barbary pirates. Decembe 20 1777 Sultani wa Morocco Mohammed ben Abdallah - Wikipedia alitangaza kwamba meli ya wafanyabiashara wa Kimarekani inaulinzi wa kisultani na iruhusiwe kupita, kutokana na kitendo hicho, Marekani iliweka sahihi mkataba wa urafiki
Moroccan–American Treaty of Friendship - Wikipedia, mkataba huo unahistoria ya kuwa mkataba wenye umri mrefu ambao haujawahi kuvuvunjika.

Hispania na Ufaransa kuivamia Morocco kama Protectorates.
Jinsi uchumi wa viwanda ulivyozidi kuongezeka ulaya, umuhimu wa Afrika ya kaskani kuwa koloni uliongezeka pia. Ufaransa ilionyesha nia ya kuivamia Morocco kuanzia 1830, si kwa kulinda mipaka ya Algeria ambayo ilishakuwa koloni lake bali pia iliona umuhimu wa Morocco katika bahari mbili. 1860 ugomvi mkubwa ulitokea juu ya eneo la Ceuta, ugomvi huu ulipelekea Hispania kutangaza vita. Ushindi wa Hispania katika vita hii uliiwezesha kuwa mmiliki halali wa eneo la Ceuta, hivyo kuifanya kuweza kuimarisha ulinzi na kujitangaza pia kama Protectorates wa pwani ya Morocco.

Mwaka 1904, Ufaransa na Hispania waliitengeneza Morocco kuwa ukanda wenye nguvu zao. Ufaransa ilijewekea nguvu ya kufanya maamuzi juu ya Morocco na hali hiyo ilitambuliwa na Waingereza, Wajerumani walikasirishwa sana na jambo hilo na mtafaruku mkubwa ulitokea. Algeciras Conference - Wikipedia mgogoro huo ulitatuliwa kwenye mkutano wa Algeciras. Mgogoro wa Agadir Crisis - Wikipedia uliongeza hali ya kutokuelewana baina ya mataifa ya ulaya yenye nguvu. Treaty of Fez - Wikipedia yaliifanya Morocco kuwa protectorate wa Ufaransa, hii ilipelekea 1912 Fez riots - Wikipedia. Hispania iliendelea kuwa protectorate wa pwani ya Morocco na katika mkataba huo huo Hispania ilipewa nguvu ya kulinda eneo la kusini na kaskazini mwa Sahara.

Maelfu ya wakoloni yalianza kuvamia Morocco, wengine walinunua maeneo yenye rotuba kwaajili ya kilimo, wengine bila huruma walianza kuchima madini na kuyasafirisha nje. Makundi yaliyonufaika katika zoezi hili yalizidi kuishawishi Ufaransa kuongeza nguvu ya kuitawala Morocco. Nguvu ya ziada pia ilihitajika kufuatia vita vilivyokuwa vikiibuka mara kwa mara kati ya makabila, baadhi ya makabila yaliunga mkono utawala wa Ufaransa. Aliyekuwa Gavana wa kipindi hicho Generali Marshal Hubert Lyautey - Wikipedia kutoka moyoni mwake alipenda utamaduni wa Morocco na alifanikiwa kuweka utawala wa mseto baina ya Morocco na Ufaransa wakati akijenga shule za elimu ya kileo katika kipindi hicho. Wanajeshi wa Morocco pia walishiriki katika vita ya I na ya II ya dunia katika jeshi la Ufaransa.

Kati ya mwaka 1921 na 1926 kabila la Beber lilianza mashambulizi katika milima ya Rif yakiongozwa na Abd el-Krim - Wikipedia, mashambulizi hayo yalipelekea kuanzishwa kwa utawala wa Rif ambao haukudumu kwa muda mrefu kwani majeshi ya Ufaransa yakishirikiana na majeshi ya Hispania yaliharibu utawala huo.

Mwaka 1943 chama cha Istiqlal Party - Wikipedia kilianzishwa kikiwa na msaada wa siri kutoka Marekani kikiwa na lengo la kupigania uhuru wa Morocco. Chama hiki baadae kiliweza kutoa viongozi walioshiriki katika kulipigania taifa.

Ufaransa ilimpeleka Mohammed V of Morocco - Wikipedia uhamishoni
Madagascar - Wikipedia kama mkimbizi mwaka 1953 na walimweka Mohammed Ben Aarafa - Wikipedia katika nafasi yake, ambae hakupendwa na wengi. Kitendo hicho kiliamsha mapambano ya upinzani dhini ya Ufaransa na Hispania katika ardhi ya Morocco.
Mapambano yanayokumbukwa zaidi katika historia hii ni yale ya Oujda - Wikipedia ambapo wa Morocco waliwaua raia wa Ufaransa na Hispania mitaani. Hii ilipelekea Ufaransa kumruhusu Mohammed V kurejea Morocco na kuanza mazungumzo yaliyopelekea uhuru kupatika mwaka uliofuatia. French protectorate nchini Morocco ilimalizika rasmi mwezi March 1956 na Morocco ilijipatia uhuru wake na kujulikana kama Ufalme wa Morocco. Mwezi mmoja baada Hispania ilimaliza protectorate yake eneo la pwani ya kaskazini ilijibakishia madaraka katika pwani mbili Ceuta - Wikipedia na Melilla - Wikipedia zote zikiwa katika bahari ya Mediterranea. Sultani Mohammed V aliwekwa wakfu kama Mfalme mwaka 1957.

Utawala wa Mfalme Hassan II.
Kufuatia kifo cha baba yake Mfalme Mohammed V, Hassan II of Morocco - Wikipedia aliapishwa kuwa mfalme March 1961. Mfalme Hassan ndiye aliyekuwa mtoto mkubwa wa kiume wa Mfalme Mohammed V, alizaliwa katika ndoa ya mke wa pili Lalla Abla bint Tahar - Wikipedia. Mfalme Hassan alisoma Imperial College Rabat - Wikipedia na alipata shahada ya sheria University of Bordeaux - Wikipedia

Kwa amri ya utawala wa Kifaransa, yeye pamoja na baba yake Sultan Mohammed V walipelekwa ukimbizini Corsica - Wikipedia 20 August 1953. Walihamishiwa Madagascar January 1954. Akiwa huko alikuwa ndiye mshauri wa baba yake katika maswala ya siasa wakati huo akijulikana kama Prince Moulay Hassan. Familia nzima ilirudi Morocco Novemba 16 1955.

Pamoja na baba yake, walifanikisha uhuru wa Morocco na alikabidhiwa madaraka kama Katibu Mkuu Kiongozi wa Royal Moroccan Armed Forces - Wikipedia April 1966, katika machafuko yaliyotokea mwaka huo huo alifanikiwa kuyaongoza majeshi kuelekea maeneo ya Rif - Wikipedia. Mohamme V alipobadilisha utawala kutoka Usultani kuwa Ufalme 1957, Prince Moulay Hassan akawa Crown prince - Wikipedia na baadae Mfalme 1961 kufuatia kifo cha baba yake.

Utawala wa mfalme Hassan II unalalamikiwa sana kwa matukio mengi ya kukiuka haki za binadamu, utawala huu ukipewa nguvu na Alaouite dynasty - Wikipedia. Katika serikali yake ya kwanza mwaka 1963, alisisitiza mfumo wa vyama vingi, kulikuwa na chama kimoja tu upande wa Maghreb - Wikipedia katika kipindi hicho. Serikali ilimpa mfalme madaraka makubwa sana ambayo alianza kuyatumia kudumisha utawala wake, hii ilileta vurugu za kisiasa kati ya National Union of Popular Forces - Wikipedia na Istiqlal Party - Wikipedia ambavyo ndio vyama vikuu.

Mwaka 1965 mfalme Hassan II alivunja bunge na kutawala nchi moja kwa moja, ingawa hakuvunja muundo wa demokrasia wa bunge. Uchaguzi ulipofanyika matokeo yalichakachuliwa na vyama vilivyomuunga mkono mfalme vilipata upendeleo mkubwa. Hii ilisababisha machafuko makubwa, maandamano na fujo mitaani watu walipinga utawala wa mfalme. Marekani waliangalia kwa ukaribu sana na kuripoti kuwa "mfalme Hassan alikuwa na fahari ya kulinda nafasi yake kuliko kuangalia madhara ya matatizo ya kisiasa yanavyo athiri nchi".

Miaka ya 1970 Mfalme Hassan alinusurika katika majaribio mawili ya kuuwawa, la kwanza likiwa ni la mwaka 1971, jaribio hili lililoungwa mkono na Libya na lilipangwa na Generali Mohamed Medbouh - Wikipedia na Colonel M'hamed Ababou - Wikipedia na lilitekelezwa na wanajeshi vijana waliomaliza mafunzo. Jaribio hilo lilitokea katika hafla ya Mfalme kuazimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwake, wageni wa muhimu kama Balozi wa Ubelgiji Marcel Dupet na wageni wengine waliwekwa chini ya ulinzi, mfalme alichukuliwa na kuhifadhiwa kwenye kijumba kidogo kwa usalama wake.

Kituo cha redio cha Rabat kilitekwa na wapinzani na walianza kutangaza kuwa mfalme ameuwawa na utawala wa kiraia umeingia madarakani. Jaribio lilikwisha siku ile ile baada ya askari watiifu kwa mfalme kuingia katika jumba la mfalme na kuwadhibiti wapinzani. Ilikuja kufahamika baadae kwamba askari vijana walitekeleza amri kutoka juu bila wao kufahamu wakijua wanamlinda mfalme.

Jaribio la pili lilitokea August 16, 1972 wakati mfalme akiwa anarudi Rabat akitokea Ufaransa, ndege nne za kijeshi aina ya Northrop F-5 - Wikipedia mali ya Royal Moroccan Air Force - Wikipedia zilirusha mashambulizi kwenye Boeing 727 - Wikipedia aliyokuwa akisafiria mfalme. Ingawa risasi nyingi zilishambulia lakini walishindwa kuiangusha ndege. Mfalme mwenyewe inasemekana alichukua control ya radio kwenye ndege na kutangaza "nyinyi wajinga acheni kushambulia, mtawala wa mabavu ameshafariki". Watu nane walifariki wakati ndege ikiendelea kushambuliwa ikiwa na viongozi wajuu wa serikali. Generali Mohamed Oufkir - Wikipedia ambae alikuwa waziri wa ulinzi ndiye aliyeratibu jaribio hilo, inasemekana alijiua kwa kunywa sumu mara tu baada ya jaribio kushindwa lakini maiti yake ilikutwa na majeraha mengi ya risasi.

Wakati wa kipindi cha vita baridi, Hassan II alishirikiana na nchi za magharibi hasa Marekani. Kulikua na uhusiano wa karibu sana kati ya serikali ya Hassan II na CIA ambao walisaidia kuongoza ulinzi katika idara ya usalama ya Morocco. Hassan alikuwa kiungo katika mapatanisho ya Waarabu na Waisrael, hili liliwezekana kwakuwa kuna jumuia kubwa sana ya Wayahudi Morocco.

Wakati wa utawala wake, alifanikiwa kuirejesha ardhi ya Ifni - Wikipedia iliyokuwa ikikaliwa na Hispania 1969, pia mwaka 1975 jeshi lake lilichukua 2/3 ya Spanish Sahara - Wikipedia kupitia operation Green March - Wikipedia. Swala hili lilikuwa kiini cha mjadala kwenye mijadala ya Morocco na maswala ya nje mpaka leo hii. Uhusiano na Algeria ulidhoofika kwa haraka kwasababu ya swala la Western Sahara - Wikipedia, pia Morocco inadai Tindouf - Wikipedia na Béchar - Wikipedia ni sehemu ya ardhi yake. Hii ilipelekea vita vya 1963 vilivyojulikana kama Sand War - Wikipedia. Uhusiano na Mauritania haukuwa mzuri pia kwani Morocco ilitambua uhuru wa nchi hiyo baada ya miaka 10 kupatikana na pia Morocco inadai sehemu ya Mauritania ni ardhi yake Greater Morocco - Wikipedia

Uchumi, Hassan II alifuata sera za Market economy - Wikipedia ambapo kilimo, utalii na uchimbaji mdini ya phosphate vilikuwa ndiyo vitega uchumi vikuu. Kipindi cha 1960 mpaka 1980 kilikulikana kama Years of Lead (Morocco) - Wikipedia, watu walishuhudia maelfu ya wapinzani wa siasa za mfalme wakifungwa, kuuwawa, kuondolewa nchini au Forced disappearance - Wikipedia. Ilipofika mwaka 1990 mfalme aliliongezea bunge madaraka, aliwatoa wafungwa wengi wa kisiasa magerezani na 1991 aliruhusu vyama vya upinzani kushika madaraka katika serikali yake kwa mara ya kwanza katika Arab world - Wikipedia. Aliunda tume ya Royal Council for Human Rights kuangalia madai ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Kifo cha Mfalme Hassan II.
Kifo cha Hassan II hakikuhusishwa na mkono wa mtu, alifariki katika mji aliozaliwa akiwa na umri wa miaka 70, ilikuwa tarehe 23 July, 1999. Mazishi ya kitaifa yaliandaliwa kwaajili yake mjini Rabat, wakuu wa mataifa 40 walihudhuria mzishi hayo. Alizikwa kwenye Mausoleum of Mohammed V - Wikipedia Rabat, jeneza lake lilibebwa na mwanae Mfalme Mohamed VI, mdogo wake Moulay Rashid pamoja na binamu yake Moulay Hisham, lilifunikwa kwa kitambaa cha kijani kikiwa na maandishi "Hakuna mungu zaidi ya Allah", yakiwa yamenakshiwa kwa maandishi ya dhahabu.

Familia.
Mfalme Hassan II alioa wake wawili mwaka 1961, Lalla Latifa - Wikipedia aliyejaaliwa watoto watano; Meryem, Mohammed VI (mfalme wa sasa), Asma, Hasna na Rashid. Ndoa ya mfalme na Lalla Fatima bint Qaid - Wikipedia haikujaliwa kupata watoto.

Utawala wa Mfalme Mohammed VI.
Mfalme Mohammed VI ni mtoto wa pili kuzaliwa na mtoto mkubwa wa kiume wa Mfalme Hassan II na mkewe wake wa pili Lalla Latifa Hammou. Siku ya kuzaliwa kwake, Mohammed alisimikwa kama mrithi wa taji na kupewa rasmi jina la Crown Prince. Baba yake alikuwa na nia kubwa ya kumpa elimu ya dini na elimu ya siasa tangia akiwa mdogo, akiwa na umri wa miaka mine alishaanza masomo ya Quran katika shule iliyokuwa ndani ya Ikulu.

Mohammed alimaliza elimu yake ya msingi na secondary katika shule ya Royal College na alipata Baccalaureate 1981 kabla ya kupata Bachelor's degree - Wikipedia ya sheria Mohammed V University at Agdal - Wikipedia 1985 na research paper ya law degree ilikuwa " the Arab-African Union and the Strategy of the Kingdom of Morocco in matters of Internationl Relations". Alisoma pia Imperial College and University of Rabat.

Alipewa cheo cha rais wa Pan Arab Games - Wikipedia, alikuwa commissioned kama Colonel Major wa Royal Moroccan Army - Wikipedia mwaka 1985. Alitumikia kama kiunganishi kati ya ofisi na majeshi ya mfalme mpaka 1994.
Mwaka 1987 Mohammed alipata certificate ya political science, 1988 akiwa Brussels pamoja na Jacque Delors ambae wakati huo alikuwa rais wa European Commission, Mohammed alipata Diploma ya public law. Mohammed alipata PhD ya law ikiwa na Latin honors - Wikipedia 1993 kutoka French University of Nice Sophia Antipolis - Wikipedia thesis yake ikiwa EEC-Maghreb Relations.

Mara tu baada ya kuapishwa kama mfalme, Mohammed VI aliwatangazia wananchi wake kupitia television ya taifa kuwa, anaahidi kupambana na umasikini na rushwa na atajitahidi kutengeneza fursa za ajira pia haki za binadamu Morocco zitaboreshwa. Kauli zake zimemletea mgogoro kwa viongozi wa dini ya Kiislam wenye msimamo wa conservative. Mwaka 2004 alipitisha sheria ya Mudawana - Wikipedia, hii ni sheria ya famiiia inayo wafanya wanawake watambulike zaidi katika jamii.

Mfalme Mohammed alifanya ziara ya kiuchokozi Sahara Magharibi mwaka 2002. Mwaka 2007 Morocco iliamua kuweka wazi mkataba wake wa umiliki halali wa eneo la Sahara Magharibi mbele ya baraza la Umoja wa Mataifa, Polisario Front - Wikipedia waliupinga vikali uhalali huo. Hii ilipelekea uamuzi wa kuziweka pande hizi mbili mezani kwa mazungumzo lakini mpaka kufikia 2010 hakua suluhisho lililotoka kati ya pande mbili hizi. Askari wa usalama walishambulia kambi ya upinzani Sahara Magharibi na hii ilisababisha hali ya vurugu na ghasia katika eneo hilo ndani ya mji mkuu wa Laayoune - Wikipedia
 
Sky Eclat I admire your passion for history. (Academics)
Nothing makes me really happy like seeing a living testimony of Emancipated African woman. (If at all you are a lady)
Please keep up the vibe......
;);););););)
 
Sky Eclat I admire your passion for history. (Academics)
Nothing makes me really happy like seeing a living testimony of Emancipated African woman. (If at all you are a lady)
Please keep up the vibe......
;);););););)
I wanted to know the real seed of the Western Sahara dispute and by the look of it the land originally belongs to the medieval Morocco, and Mohammed is well prepared to let it be that way.
 
Back
Top Bottom