S2dak_Jr
Senior Member
- Jul 15, 2012
- 198
- 45
Jamaa ameshinda kesi dhidi ya pingamizi la kutofunga ndoa liliowekwa na mwanamke mmoja anayedai kuwa ana ndoa na PM huyo wa Zimbabwe.
Habari zinadai kuwa anatarajia kufunga ndoa na mwanamke wake wa sasa Bi. Elizabeth na kumuacha yule waliyekuwa na ndoa ya kitamaduni.
Jaji wa Mahakama Kuu aliyesikiliza kesi hiyo kwenye mazingira ya faragha, amesema kuwa ndoa za kitamaduni hazitambuliki kwa sasa na Bi. Tembo hakustahili kufikisha shauri hilo kwenye Mahakama Kuu.
Bi. Tembo ameshauri kulipeleka shauri hilo kwenye Mahakama za chini na si kuzuia ndoa bali afikishe hoja ya kugawana mali kwani ndoa za kitamaduni hazitambuliki na katiba/sheria za nchi hiyo.
Rais Robert Mugabe anatarajiwa kuhudhuria misa ya ndoa hiyo na kuwaandalia sherehe Ikulu, Mjini Harare.
Source: bbc.co.uk/swahili