Shinto
JF-Expert Member
- Dec 6, 2010
- 1,781
- 96
Wakuu nimekutana na hii issue mara mbili watu waki-debate. Nikaona si vibaya nikaleta kwa great thinkers tupate mawazo na mitizamo yenu.
Nawasilisha!
- Medical marijuana: Kuna baadhi ya states huko U.S na MExico zimeridhia watu kupanda kisha kutumia marijuana kama njia ya kupunguza aina fulani za maumivu. Kuna mama mmoja alikuwa akitoa ushuhuda kwamba bila kutumia hiyo kitu hiwa hawezi kufanya kazi yeyote productive. Amekwenda kwa treatment for more than 30 years bila mafanikio, relief aliipata alipoanza kutumia medical marijuana!
- Morphine: Hii ni aina ya dawa maarufu kama nusu kaputi! ambayo imekuwa ikitumiwa kwa muda mwingi wakati wa kufanya upasuaji. Muhimu kujua ni kwamba hii dawa ina uhusiano wa karibu mno na madawa maarufu ya kulevya cocaine au heroine. (nadhani yanatokana na mmea mmoja poppy..not so sure)! Katika baadhi ya nchi hii dawa hutumiwa na watu wenye maaumivu makali na endelevu, kama vile cancer isiyopona, HIV AIDS na mengeni kama hayo!
Nawasilisha!