Mongo la ndege hospital

Benno

JF-Expert Member
Nov 21, 2009
332
51
Juzi nimeshuhudia Mgonjwa anayekaa Mongola Ndege Jirani na Hospitali akitaabika Kupata Huduma ya Kwanza, Huku Hospitali iliyo Jengwa na Serikali na imekamilika ipo na haijaanza kutumika mpaka sasa, toka nihamie eneo hili huu sasa MWAKA MZIMA, Hatuoni chochote kinachoendelea.

Taarifa tulizo nazo ni kwamba kuna Madaktari tayari wameshahamishiwa hapa wapo mtaani wanakula Good time.

Hatuoni hata kiongozi akipita hapa kutuambia what next;

Wakati wa uchaguzi tuliambiwa within one month itafunguliwa mpaka leo

Tunapata shida sana!!

Wadau mtusaidie
 
Wakati wachaguzi 2015! poleni lakini huyo mgonjwa naye ni wa magamba??
 
Mmechukua hatua gani kutoa taarifa kwa uongozi husika kuwa Ma-Dr. waliohamishiwa hapo wanakula mshahara bure bila kuingia ofisini? Maana mambo mengine tunalalamika lakini yapo chini ya uwezo wetu. Jiunge pamoja andamana hadi ofisi ya kata, ikishndiikana, piga mguu mpaka ngazi ya juu na juu na juu na juuuuuuuuu zaidi.
 
Mie nina wasiwasi MONGA LA NDEGE haiko hapa Dar!!!! Nimekuwa dereva wa daladala wa karibu ruti zote hapa DAR ES SALAAM sijawahi kusikia abiria yeyote akiongelea KITONGOJI YENYE JINA HILI HAPA DAR.....Labda MJI KASORO BAHARI...
 
Juzi nimeshuhudia Mgonjwa anayekaa Mongola Ndege Jirani na Hospitali akitaabika Kupata Huduma ya Kwanza, Huku Hospitali iliyo Jengwa na Serikali na imekamilika ipo na haijaanza kutumika mpaka sasa, toka nihamie eneo hili huu sasa MWAKA MZIMA, Hatuoni chochote kinachoendelea.

Taarifa tulizo nazo ni kwamba kuna Madaktari tayari wameshahamishiwa hapa wapo mtaani wanakula Good time.

Hatuoni hata kiongozi akipita hapa kutuambia what next;

Wakati wa uchaguzi tuliambiwa within one month itafunguliwa mpaka leo

Tunapata shida sana!!

Wadau mtusaidie
Kama ahadi mlipewa katika kipindi cha uchaguzi 2015 hiyo itakuwa imekula kwenu 100%,cha msingi endeleeni kuamini kuwa ipo siku japo style hiyo ya kusubiri bila kujua ni lini sio nzuri.Poleni wadanganyika
 
Mie nina wasiwasi MONGA LA NDEGE haiko hapa Dar!!!! Nimekuwa dereva wa daladala wa karibu ruti zote hapa DAR ES SALAAM sijawahi kusikia abiria yeyote akiongelea KITONGOJI YENYE JINA HILI HAPA DAR.....Labda MJI KASORO BAHARI...
Kwa hiyo unataka kutuambia kuwa unayafahamu maeneo yote ya Dar es Salaam?
 
Mongola Ndege ipo kata ya Ukonga, Hapa NG'AMBO YA FFU, NI JIMBO LA UKONGA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom