Mongela wa PSPF asimamishwa kazi...

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
MKURUGENZI wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Patrick Mongella, amesimamishwa kazi kuanzia Oktoba 15 mwaka huu, kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Chanzo cha kuaminika kutoka PSPF kimesema kwamba, kusimamishwa kwa mkurugenzi huyo, kumetokana na agizo la Bodi ya Wadhamini ya PSPF, baada ya kubaini kuwapo namna ya kutotekeleza majukumu yake ipasavyo, pamoja na kutotii maagizo halali ya wakubwa wake kuhusiana na uendeshaji wa shughuli za mfuko.

Pia, habari za ndani zinaeleza kuwa kiongozi huyo hakuwa na mahusiano mazuri ya kikazi na watumishi wenzake wa mfuko wa kada zote, akidaiwa kuwa ni mwenye dharau, kiburi, majivuno na lugha chafu kwa watumishi walioko chini yake, wakiwamo viongozi wake wakuu.

Chanzo hicho kimefichua kwamba, majigambo ya bosi huyo yanatokana na yeye kujivunia jina la mama yake, ambaye aliwahi ni mkongwe katika nyanja mbalimbali za siasa ndani na nje ya nchi na ukaribu aliokuwa nao na baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali hapa nchini.

Taarifa zaidi zinapasha kuwa, kiongozi huyo aliyepewa dhamana ya kuongoza kurugenzi nyeti katika taasisi hiyo muhimu, hakuwa na sifa na vigezo hitajika vya kitaaluma wakati wa ajira yake, hivyo kupelekea kusaka sifa hizo baada ya kupewa nafasi hiyo.

Watumishi wengi wa PSPF wamepokea agizo hilo la bodi kwa furaha kubwa, maana kiongozi huyo alikuwa ni kero na kikwazo kikubwa tena cha muda mrefu sana, husus
 
Sishanagai sana huyu jamaa (mtoto) nasikia aliwahi kufanya kazi kampuni ya sigara na alifukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu, alikuwa analazimisha apewe cheo hapo sigara kwa kutumia jina la mama yake.
 
Mama yake naye si alitutia aibu na hasara (financially) kule African Parliment (AP)? Tanzania ililazima kulipa hela za matanuzi yake aliyokuwa anafurahia na familia yake ili kupunguza aibu ya nchi?
 
Madhara ya kuwapa watu ajira na vyeo kwakuwa ni watoto wa vigogo ndo haya.wengi wa hawa watu ni vilaza na hawana utendaji mzuri wa kazi ila majina na system zinawabeba.
 
Angekuwa ana jina fulani, watu wasingekawia kusema wanaonewa.
 
Jamani, tusifike kusikotakiwa...! Ukristo, jina fulani kuonewa tusivipe nafasi katika systems zetu! Sitaki kusema hivyo vitu havipi, hapana vipo ila nasema tusivihusudishe...

Mtu kama alishaonesha failure katika kampuni fulani na akatimuliwa, kunakuwa na ajabu gani tena asipobadilika akitimuliwa na mwajiri mwingine? Napenda sana ndugu zanguni tujenge utamaduni wa kuchapa kazi na kutambua uwezo wa mtu katika nafasi yake no matter what..!
 
Wamemrudisha Mafuru watamrudisha na huyu...hii ndio Tz yetu. Wazembe wapuuzi ndio wanapewa mamlaka ya kuingoza Tz. Anajivuna nini na mama yake?? Mama yake muda wake uliisha..Tatizo la Tz. watoto wa viongozi wanageuza kama nchi ya Tz. ni ya baba zao wanasahau Tz ni ya Watanzania na sio ya ukoo fulani au jina fulani. Dawa ilikuwa kuwaondoa wote tuchukue watoto wa wakulima wanaojua ni kiasi gani wazazi wao walitaabika kuwapekeka shule sio hawa kula kulala kila siku wanafikiri ni wao waliiiumba dunia na kama si dunia Tanzania.
 
greedy... wana mashamba ya Zabibu...

Pesa za UN nyingi... wanajsikia
 
Tunaongea sana, si amepisha uchunguzi kwanini tusiache uchunguzi ufanyike?? hata bata anakuwa msikivu akitaka kujua jambo.
 
Ajira gani? hapo ni shamba la bibi kama Bot. Nafasi ilitangazwa lini? watu kibao hapo wapo haijulikani walifanya lini interview na wala hizo nafasi hazijulikani zilitangazwa lini. Ukiacha BoT hapa ndo target ya watoto wa vigogo. ukifanya kazi kwa zaidi ya miaka 3 unakopeshwa milioni mia hamsini. we kapuku utapata wapi?
 
Yaani mtu mmoja ameanzisha uzi...bila hata wengine kuwa na uhakika wa 1) Ukweli wa habari yenyewe, wameshaanza kutupa mawe 2) Ukweli wa tuhuma zenyewe, wameshaanza kuhusisha watu wengine (Hivi kuwa mkurugenzi kwenye taasisi kubwa kama ile, unaweza kweli kupewa kwa kuwa mama yako alikuwa na jina kubwa? Tena mama mwenyewe sasa hivi hana hata chembe ya madaraka)

Ndugu zangu, tuendelee na kujadili hoja...lakini tuwe objective japo kidogo...

Senki You!!
 
cha ajabu eti anatumia jina la mama yake..kwanini asitumie jina la baba yake kama wengine wote tufanyavyo kama ni mwanaume wa kweli....mwanaume mzima ovyoooo
 
Back
Top Bottom