Monalisa atoa ya moyoni kifo cha Tyson

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
7,484
5,142
Haya ndio aloyasema, Let me clear the air ni hivi, pamoja na ujinga tulioufanya mimi na George katika maisha yetu, kwa macho ya kibinadamu utasema alikuwa na mke mwengine but kwa macho ya kimungu mimi ni mke halali wa George Otieno Okumu aliyelala.

Anayesema mke wa tyson alijifungia ndani mimi nikawa nachukua pole zisizo zangu, dah! Kwanza wanawake walikuwa wawili ndani sio mmoja na wote walijifungia ndani.

Kwanini? ni wakristo na wanaijua dini waombolezaji waliokuwa wakinipa pole mimi,ni kwanini? jiulize kabla ya kuropoka halafu wewe ni mwanamke kuna siku yatakukuta.

Nilienda kutimiza wajibu wangu kama mke, ningelia peke yangu kwetu mngenisema sana, nimekaa msibani naambiwa nachukuwa pole za bure wacha nikukumbushe maandiko.

Alichokiunganisha Mungu?....;kilichofungwa duniani?.....;nikupende,nikutunze hadi kifo?..... sasa kifo kimetutenganisha siku ya mwisho unadhani George ataitwa na nani?

Pamoja na mambo yake yote wacheni nimlilie he was a good father kwa Sonia wangu especially miaka 5 ya mwisho wa uhai wake, acheni nimlilie he was my best friend 1998-2014.

Nimeshare nae kitanda 2000-2006. Nitakuwa mtu wa aina gani nisiwe na uchungu, ukiona mwanamke mwenzio kaishindwa ndoa usimcheke jua kuna sababu.

Na ni fundisho kwa wachukua waume za watu wote mjini, mume akiumwa huwa anarudi kwa mkewe, na akifa? and for ur info msianze anajifanya mke sasa hivi ili apewe mali.

Sonia ni mali kubwa sana alioniachia am so happy. Waaache wao wanaolilia kupewa pole wapiganie, mwenyewe aliyetafuta kafa kaziacha sembuse tuliobaki? niacheni nimlilie, waacheni fans wangu walie na mimi".

My take: haina haja ya kujibu kila kinachojadiliwa na walimwengu. Unasema haya ili tujue marehemu mlipendana sana au?

All in all mioyo yenu ndio inajua kipi ni kipi kuhusu mapenzi yenu.

okay Bayiiii
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    25.3 KB · Views: 2,551
Jamani kasema ukwelii kwan si walifunga ndoa au, na wamezaa nae na alikua akimtunza mtoto

Okay ni ukweli ila kuna haja ya kujibu kila usemwacho na waja? ni kama anawasimanga waliochepuka na mumewe wakati wa utengano wakati yeye pia alichepuka. kwangu mimi kimya ni jibu kuliko kutoa matamko. wema ana masoo ila huwezi mkuta akijibujibu hovyo kutafuta huruma.
 
Ungetolea mfano mie sio mpaka Wema tu
Moyo ni sirii na ukiwa mchungu lazima useme mi naona haina shida, ingekua tu kazaa nae basi halaf hatunzi mtoto angenyamaza kimyaa
 
Ki Kristo hiyo ndoa ilishakufa maana alibadili dini akaolewa tena asijishaue alichounganisha Mungu ndoa za kikristo nazo zina mipaka yake na zinaweza kutenguliwa na kanisa hasa mmoja wapo akibadili dini tena na kuzaa kabisa nje basi ndoa haipo tena na mwanaume au mwanamke yupo free kufunga ndoa tena kanisani.

What if yule mwarabu angekuwa bado yuko nae kwenye ndoa na yule mtoto wao wakiume je Mona angetamka haya anayoyasema kuwa ni mke halali... mambo mengine its better to keep quiet tu yaishe ukiongea unajidhalilisha tu.
 
Haaaaahaaa eti "alichokiunganisha Mungu?" Duh ivi uyu mdada si aliwahi kuolewa tena alisahau kua waliunganishwa?wamuache jamaa apumzike zake kamaliza safari yake wasimfanye kua njia ya kuurudisha umaarufu.

Umeona eeh kuwa mzazi mwenza ni tosha na si kujidhalilisha hivi.. hivi angekuwa hajapewa talaka na muarabu wake angeyasema haya kuwa ni mke halali
 
Sonia ni mali kubwa sana alioniachia am so happy.waaache wao wanaolilia kupewa pole wapiganie.mwenyewe aliyetafuta kafa kaziacha sembuse tuliobaki?niacheni nimlilie,waacheni fans wangu walie na mm".

Nimeyapenda hayo maneno pesa inatafutwa sio uhai wa mtu.............
 
Sometimes watu wanasema saaaana na tena siku hizi na haya masosho netiweki hatari tupu bora siye wa zamani wakisema mtaa huu unahama kwisha habari yake......si kazi ndogo kubeba pressure ya maneno ambayo unaona sometimes useme ukweli ili waelewa wakae kimya na wale ambao midomo yao iko activated since wamezaliwa waendeleze libeneke.....pole zake Monalisa.......
 
sasa amekufa ndio anajidai kukumbuka hiloo
Haaaaahaaa eti "alichokiunganisha Mungu?" Duh ivi uyu mdada si aliwahi kuolewa tena alisahau kua waliunganishwa?wamuache jamaa apumzike zake kamaliza safari yake wasimfanye kua njia ya kuurudisha umaarufu.
 
aliyefiwa mi naona ni yule aliyekuwa naye hadi mauti yanamfika...ye asubiri mwarabu wake afe akakae eddah kama akifanikiwa kuwepo
Ki Kristo hiyo ndoa ilishakufa maana alibadili dini akaolewa tena asijishaue alichounganisha Mungu ndoa za kikristo nazo zina mipaka yake na zinaweza kutenguliwa na kanisa hasa mmoja wapo akibadili dini tena na kuzaa kabisa nje basi ndoa haipo tena na mwanaume au mwanamke yupo free kufunga ndoa tena kanisani.

What if yule mwarabu angekuwa bado yuko nae kwenye ndoa na yule mtoto wao wakiume je Mona angetamka haya anayoyasema kuwa ni mke halali... mambo mengine its better to keep quiet tu yaishe ukiongea unajidhalilisha tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom