Moja ya sababu inayowafanya wageni wapendelewe kwenye kazi zaidi ya wazawa

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Nadhani tunakubalina na ukweli kwamba Wageni wanaokuja kufanya kazi nchinihasa kwenye makampuni na mashirika ya kigeni wanawazidi wazawa kwa kukubarikakatika utendaji kazi wao.Nimelifuatilia hili na kukugundua kwamba, hata watanzania wanaokwenda kufanyakazi nje ya nchi upata upendeleo huo huo.Si kweli kwamba wageni hawa wanakuwa na uwezo mkubwa wa mawasiliano, uelewamkubwa wa kazi husika wala uzoefu zaidi ya wazawa na wala si kweli kwamba wageniwanafanya kazi kwa bidii kuliko wenyeji. Mimi nimegundua sababu ifuatayo, ambayo kwa hakika, haitowezekana hata mara mojakwa wazawa kuweza kujikwamua katika hili na kuwashinda wageni, si kwa Tanzania tubali ulimwenguni kote.UPWEKEWageni ni wapweke sana, hawana ndugu wa kuwatembeleana nao, hawana ndugurafiki na jamaa wa kushirikiano katika mambo yoyote ya kijamii kama, vikao na hatimayesherehe za harusi, misiba, wagonjwa, na haya si kwa yale yanayowahusu wao direct, balihata kwa yale yanayowahusu directly ndugu jamaa na marafiki zao. Ukizingatia hapapesa zao wanarudisha majumbani kwao, hivyo hawana hata muda wa kwendakusimamia ujenzi, hawashiriki kwenye mambo ya kisiasa kama mikutano n.k.n.kHiki kinawafanya waishie kutumia muda mwingi katika kufikiria na kufanya kazi,wanafanya kazi bila interaptions hizo wakiwa maofisini na wakirudi nyumbani wanaendeleakukamua kazi zaidi, tofauti kabisa na wazawa ambao ni lazima washiriki kwenyemambo niliyoaanisha hapo juu hasa ukizingatia kwamba wakati mwingine mambohayo yanajitokeza katika namna ambayo yanakuwa na umuhimu zaidi ya kazi.Kwa mantiki hii, Wageni wataendelea kuonekana bora zaidi ya wageni siku zote.
 
Back
Top Bottom