Moja ya nyimbo za JB Mpiana isiyochuja(FEUX DE LAMOUR)

Wenge Musica BCBG wanaujua muziki! Mtoa mada shukrani umetukumbusha mbali
 
Dah yani thanks kwa hiyo mistari mana nulikuwa najiimbiaga tu. One ov my best African song. Sichoki kuuskiliza. Actually JB ni namba moja Africa kwa kuimba then ndyo watafuata kina Yosour ndour nakina Keita
 
Asante sanana je kwanini alijiita Sadam Husein?

Alikuwa Ni Mbabe, Mwenye Roho Mbaya Na Muuaji Kama Aliyekuwa Rais Wa Iraq Hayati Saddam Hussein. Na Kama Utakumbuka Ni Huyu Huyu Joseph Kongolo Mobutu Ndiyo Alimuua Kwa Kumpiga Risasi " Live " Yule Waziri Wa Ulinzi Wa Wakati Ule Wa Yale Mapigano Ya Majeshi Ya Serikali Dhidi Ya Majeshi Ya Muungano Yaliyokuwa Chini Ya Banyamulenge. Kisa Kilichopelekea Hadi Huyu Mtoto Wa Mobutu Akamuua Huyu Waziri Ni Baada Tu Ya Waziri Kukiri Mbele Ya Vyombo Vya Habari Kuwa Majeshi Yaliyokuwa Yakiongozwa Na Aliyekuwa Kiongozi Wa Waasi Wakati Huo Na Aliyekuja Pia Kuwa Rais Wa Kongo Hayati Laurent Desire Kabila ( Huku Mitaa Ya Oysterbay Na Msasani Tulikuwa Tukimjua Kama Mzee Mwale ) Kuwa Yanakaribia Kuchukuwa Nchi Ya Kongo. Kipindi Pia Cha Baba Yake Akiwa MADARAKANI Joseph Kongolo Mobutu Aliwaua Sana Wanajeshi WASALITI Kwa Baba Yake Na Hasa Wale VIONGOZI Waliojifanya KUJIPENDEKEZA Kutaka Kumpindua au Kumrithi Baba Yake Rais Mobutu. Ni Matumaini Yangu Kuwa Nimekujibu KUNAKOTUKUKA.
 
Sidhani kama wewe ni mzima,so ngoja nikuache.

Ningekuwa Siyo Mzima Kamwe Nisingekupa Hayo MADINI. Hata Hivyo Watu Wenye AKILI Nyingi Sometimes Huonekana Kama Vile WEHU. Kama Vipi Nikugawie Kidogo Tu MAARIFA Yangu Mkuu Ili Na Wewe UTAMBE Huko ULIPO.
 
Kuna Mijitu Humu Inataka Kulinganisha Mbingu Na Ardhi Kwa UPOPOMA Wao. Hivi Kwa Mtu Kweli Unayejua Muziki Unaweza Kusema Koffi Olomide Ni Zaidi Ya JB MPIANA? Watoto Mmekuwa Juzi Juzi Tu Hapa Leo Koffi KAWAPOFUA Tu Na EKOTITEE a.k.a SELFIE Mmepagawa Na Kumwona FUNDI Na Kumwita DJ MOPAO Wakati Tokea JB MPIANA Atoe Album Yake Ya INTERNET Alishapewa Hadhi Ya U DJ Na Miziki Yake Mingi Anaipika Mwenyewe Ktk Studio Yake. Kumfananisha JB MPINA Na KOFFI OLOMIDE Ni Sawa Na Kuifananisha New York City ( JB MPIANA ) Na Tandahimba Town ( KOFFI OLOMIDE ).

Hahahaha. Na miswi ayoo. Likong'o na mosika lite!!!!
 
Katika wanamuziki wote wa Congo huyu jamaa ndio kiboko yangu. Napenda sana kusikiliza na kucheza nyimbo zake. Sijawahi kuhudhuria show ya mwanamuziki wa nje ya nchi, lakini alipokuja JB Mpiana pale leaders, kwa kweli nilihudhuria. Nafeel ile burudani ya ukweli hasa ninaposikia kibao chake chochote kile. Nilikua nina kanda ambayo inabeba kibao hicho mleta mada umekitaja. Kwa kweli nilikua nairudi hata mara kumi sikichoki.
 
Hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hiyo album ilisababisha kundi kumegeka baada ya Mpiana kukataa kuwagawia mauzo wenzie akampa jamaa mmoja tu walimshirikisha. Nimemsahau jina aliwahi kupata soo la kuingiza watu Ufaransa kiujanja.

Ni Kweli Kuna Mtu Alimshirikisha Ktk Hiyo Album Nae Si Mwingine Bali Ni PAPA WEMBA Na Ambaye Aliimba Nae COLLABO Wimbo Mzuri Na Mtamu Uitwao CAVALIER SOLITAIRE. Kusema Kuwa JB MPIANA Ndiyo Alisababisha KUNDI Kuvunjika Siyo Kweli Na Ni Kutaka Tu KUMDHALILISHA JB MPIANA Na Sisi WAFUASI Wake WAKUBWA Bali Ukweli Ni Kwamba Waliokuwa Wakuu Wa Bendi Wakati Huo Mpiga Gitaa La Rhythm Didier Masela, Bingwa Wa Gitaa La Solo Alain Makaba Prense, Ngiama Makanda Werrason, Blaise Bula, Adolphe Dominguez Na Mwenyewe Munkulu Ya Bamukulu Jean Bedele Tshituka Mpiana Walikubalina Wote Kuwa Kila Mmoja Atakuwa Anatoa Album Yake ILA 50% Ya Mapato Ya Album Atakuwa Anachukua Mwenye Zamu Yake Ndipo Kama Mnakumbuka Mtu Wa Kwanza Kutoa Album Alikuwa Ni Alain Makaba Kwa Album Iliyofanya Vizuri Kiasi Iitwato PILE OU FACE Ambapo Kama Unataka Kusikia Watu Wanavyojua Si Tu Kulipiga Bali Kulitekenya Gitaa La Solo Basi Itafute Hiyo Album Ujiridhishe Mwenyewe. Baada Ya Hapo Ikaja Zamu Ya MUNKULU YA BAMUKULU JB Mpiana Ambapo Alitoa Album Ya FEUX DE LAMOUR Iliyokuwa Na Kibao KIKALI Cha Dakika 3 Tu Cha NDOMBOLO YA SOLO Ambapo Bingwa Wa ATALAKU au KURAPU au KUGHANI Kongo Nzima Tutu Caludji ( Yombo Lumbu ) Alionyesha UMAHIRI Mkubwa Kwamba Kwanini ALISTAHILI Kuwa Na UKOO Wa MAREPA Uliobatizwa Kwa Jina La KALUNJISTE Ambapo Hata Hawa Marepa Wengi Wa Sasa Kuanzia Akina Eyale Kalonji KEROZENE Na Rwinga Keps BRIGADE Wa Koffi Olomide Walitoka Huko, Bila Kumsahau Rapa Mahiri Wa Werrason Ila Sasa Kahama Anaitwa Mozami Muviu CELEO STRAM Na Rapa Wa Bozi Boziana Theo Mbala Bila Kuwasahau Marapa Wa Sasa MAHIRI Wa WENGE MUSICA BCBG Akina Pitshou Lisimo Gentamycine Antibiotique Na Mwenzake Jeune Cellulaire Wote Hawa Ni Wanafunzi Wa FUNDI Tutu Caludgi. Hivyo Basi Mara Baada Tu Ya Ile Album Ya JB MPIANA Kutoka KUPOKELEWA Na KUFANYA Vizuri Kwani ZILIUZWA COPY Nyingi Mno Hadi Kuvunja Rekodi Ndipo Kukapelekea JB MPIANA Kupata Pesa Nyingi Kitu Kilichomuumiza Sana Werrason Akaona WIVU Na Kuchukia Mno Hadi Akamshawishi Didier Masela, Adolphe Dominguez, Mpiga Solo Wa Akiba Patient Kusangila Na Aimelia Byake Choix Wahame Na Kuanzisha Kundi Lao La Wenge Musica Intervation Ambayo Baadae Wakabadili Tena Na Kujiita Wenge Musica Maison Mere Huku Rapa Wao Akiwa Mukeba Kalonji Wengi Wenu Mnamjua Kwa Jina La Bill Clinton. Pamoja Na Kwamba Werrason Alihama Lakini Bado Akawa Anasisitiza Kuwa Yeye Ndiyo Atumie Jina La Wenge Musica BCBG Ndipo Siki Moja JB MPIANA Akawaita Wote Wale Waanzilishi Wa WENGE MUSICA BCBG Na Kuwaambia Kuwa WASIDHANI Hiyo Bendi Imekuwa Juu Na Kukubalika Hivyo Kiwepesi Wepesi Tu Hivyo ALICHOKIFANYA JB MPIANA Ni KUMTAPIKA CHURA Kisha Akamwambia Werrason Kuwa Kama Unataka Kuwa Kiongozi Wa BENDI Hii Mchukue Huyu CHURA Na Mmeze Lakini Mpiga Kung Fu Maarufu Mwenye Mkanda Wa MWEUSI Werrason AKAKATAA Ndipo JB MPIANA Mwenyewe Akamchua Yule CHURA Na KUMMEZA Tena Na Hapo Hapo Akabatizwa Jina Ambalo Wengi Leo Mnalisikia La LEADERE Le CHARISMATIQUE Kwamba Ni Kiongozi Mkuu Na Mwenye Mvuto. Mkae Mkijua Kuwa Hakuna Mwanamuziki Wa Kongo Asiyetumia NDUMBA. JB MPIANA Kameza CHURA, Koffi Olomide Huwa Anajipaka au Kujimwagia MKOJO Wake, Werrason Huwa Analala Na SOKWE, Fally Ipupa KAMUUA Mama Yake Mzazi Na Kukichukua Kitambaa Cha Mama Yake Ambacho Ktk Nyimbo Zake Nyingi Hukutumia Fuatilieni Mtaikiona Huku Ferre Gora Akimweka KIMADA Dada Yake Wa Toka Nitoke Namaanisha Baba Mmoja Na Mama Mmoja. Kwa Heshima Ya Akina Marehemu FRANCO, PEPE KALLE Na MADILU SYSTEM Sitasema UCHAWI au NDUMBA Waliokuwa Wakiitumia Kwani KIMAADILI Ya Si Busara Kuyasema Ya MAREHEMU.
 
Yap Papa na Cherry Tshtuka Mukulu Mukulu Souvere Bin Adam aliutunga na KUUISHI wimbo huu kwa MKE wake Kipenzi AMIDA SHANTUR, hata baada ya MKE wake huyo kuzaa naye watoto watatu na KUKIMBILIA KWA YULE PAPAA WA MAWE MWENYE NGOZI NENE DIDI KINUANI, PAPA DIDI STONE, JB MPIANA hakuoa mwanamke mwingine alivumilia yote hayo KWA MUDA WA MIAKA NANE mpaka MAMA AMIDA SHANTUR MAPENZI YALIPOKWISHA KWA TAJIRI AKIWA AMEZAA NAYE MTOTO MMOJA, KWA JINSI JB MPIANA ALIVYOKUWA NA MAPENZI MAZITO YA MUDA MREFU KAMA MASHABIKI WAKE ALIMREJEA MKE WAKE KIPENZI PAMOJA NA YULE MTOTO WA YULE TAJIRI.

KURUDI KWA MAMA AMIDA SHANTUR AMBAYE JB MPIANA ALIMWONA kwa mara ya kwanza mitaa ya PAris ambapo ilibidi aache gari kwenye foleni na kumkimbilia kwa miguu na kumtungia nyimbo za mapenzi zimerudisha nguvu tena BAADA YA UCHUNGU NA MATESO YA TAKRIBANI MIAKA KUMI.

JB MPIANA ANA MAPENZI MAZITO KAMA WALIVYO MASHABIKI WAKE!
 
Katika wanamuziki wote wa Congo huyu jamaa ndio kiboko yangu. Napenda sana kusikiliza na kucheza nyimbo zake. Sijawahi kuhudhuria show ya mwanamuziki wa nje ya nchi, lakini alipokuja JB Mpiana pale leaders, kwa kweli nilihudhuria. Nafeel ile burudani ya ukweli hasa ninaposikia kibao chake chochote kile. Nilikua nina kanda ambayo inabeba kibao hicho mleta mada umekitaja. Kwa kweli nilikua nairudi hata mara kumi sikichoki.

Waambie Hao MAPOPOMA Utamu Tulioupata Siku Zile Pale Leaders Club Wakati JB MPIANA Na Kundi Lake Zima La WENGE MUSICA BCBG Lilipokuwa Likitutumbuiza Mkuu. Unakumbuka Ule Wimbo Mtamu Walionza Nao Wa DJOJO NGONDA Ulivyopigwa Mkuu? Ukumbi Mzima ULISIMAMA Huku Mkono Wa Kushoto Akisimama RAPA KIPENZI Changu Pitshou Lisimo Gentamycine Antibiotique Na Kulia Alisimama RAPA Hatari Namba Mbili Jeune Cellulaire Wakiuamsha UKIMBI Kwa Ghani Zao Na Katikati Wakiwepo Wale Wacheza Shoo MAHIRI Wakiongozwa Na Queen Murder ZAMBROTTA, Nina, Virginie Boukasa, Yeti Munyeti au Igret Mountral, Biliadama Na Kale Kabinti Kadogo Ambako Kamekulia Ndani Ya Bendi Kanaitwa SHAKIRA au Brinette Na Nyuma Yao Walikuwepo WAIMBAJI MAHIRI Akina Chai NGENGE, Jules KIBENS, JB MPIANA Mwenyewe, Rio BIKU, Jean Didier LOKO, Abraham MIGNON Na Nono FUCHI Bila Kumsau Yule MCHEZA Shoo Kabambe Wa Kiume Ambaye Alituganya Watu Wote Pale Tumalize Pesa Zetu MIFUKONI Kwa Kumtunza Aitwae Gladise Wakati Siku Ktk Vyombo Pale Walikuwepo Wapiga SOLO Wawili MKONGWE Ficarre Mwamba MAITRE Na Mpiga Solo Hatari Sasa Ndani Ya Bendi Schevchenko, Huku Ktk Gitaa La Bass Alikuwepo Asiye Na Mpinzani Sunda Bass Le Pro Na Ktk Gitaa La Rhythm Alisimama Siku Hiyo Mtaalam Mwenyewe Zygal Huku Ktk SYSTEM Nzima Ya MUZIKI Ambayo Huongozwa Na Mpiga DRUMS ( Mkaanga Chips ) Alikuwepo Mwenyewe Mwenye Bendi Yake Jamaa Aitwae Seguin Mignon Bongongo Maniata Na Ktk Kumalizia Utamu Wa Siku Hiyo Walikuwepo MAFUNDI Wawili Wa Kinanda Kiongozi Geremi Kitubu Na Cedric Gezeula Huku Upande Wa Zile Ngoma Za Tumba Alisimama Mtaalam Aitwae Tumba. Kama Siku Hiyo HUKUJA Leaders Club KUSEREBUKA Na Wenge Musica BCBG Chini Yake JB MPIANA Basi Jua Ulikosa UHONDO Uliohanikizwa Na Hicho KIKOSI Ambacho Kwa Sasa Nchini Congo Kinaitwa Le Equipe Nationale Yaani Bendi Ya WENGE MUSICA BCBG Sasa Inafananishwa Na TIMU YA TAIFA YA DRC Kwa Kuwa Na MAFUNDI Na WATAALAM KIBAO WALIOTUKUKA.
 
Yap Papa na Cherry Tshtuka Mukulu Mukulu Souvere Bin Adam aliutunga na KUUISHI wimbo huu kwa MKE wake Kipenzi AMIDA SHANTUR, hata baada ya MKE wake huyo kuzaa naye watoto watatu na KUKIMBILIA KWA YULE PAPAA WA MAWE MWENYE NGOZI NENE DIDI KINUANI, PAPA DIDI STONE, JB MPIANA hakuoa mwanamke mwingine alivumilia yote hayo KWA MUDA WA MIAKA NANE mpaka MAMA AMIDA SHANTUR MAPENZI YALIPOKWISHA KWA TAJIRI AKIWA AMEZAA NAYE MTOTO MMOJA, KWA JINSI JB MPIANA ALIVYOKUWA NA MAPENZI MAZITO YA MUDA MREFU KAMA MASHABIKI WAKE ALIMREJEA MKE WAKE KIPENZI PAMOJA NA YULE MTOTO WA YULE TAJIRI.

KURUDI KWA MAMA AMIDA SHANTUR AMBAYE JB MPIANA ALIMWONA kwa mara ya kwanza mitaa ya PAris ambapo ilibidi aache gari kwenye foleni na kumkimbilia kwa miguu na kumtungia nyimbo za mapenzi zimerudisha nguvu tena BAADA YA UCHUNGU NA MATESO YA TAKRIBANI MIAKA KUMI.

JB MPIANA ANA MAPENZI MAZITO KAMA WALIVYO MASHABIKI WAKE!

Na Kwa Anayetaka Kuujua Huo WIMBO Ambao JB MPIANA Aliuimba Kwa HISIA KALI Huku AKIELEZEA Jinsi Mapenzi Yake Na Huyo Mwanamke Yalivyoanza Aangalie Wimbo Uitwao JEANNETE BOMBOLE Unaopatikana Ktk Album Ya INTERNET. Ktk Mziki JB MPIANA Namfananisha Na Gwiji Wa Mpira Wa Miguu Duniani Kwa Sasa Lionel Messi Wa FC Barcelona Na Argentina.
 
Hata kile kibao kinachopendwa hasa na kinamama huko Kongo kiitwacho; Omba hakichuji hasa anapokikanyangia live.
 
Mungu akipenda kesho nitaweka link ya mp3.Inshaallah
 
Kumbe wapenzi wa WENGE MUSICA BCBG tupo wengi humu.Mimi namzimikia sana huyu jamaa.wakati wote na nina collection zake nyingi sana

Mkuu kila siku lazima nisikilize champion kapangala na live in zenith 99
 
Back
Top Bottom