Moja ya Maamuzi Magumu ya JK ilikuwa kukulazimisha wewe Lowassa Kujiuzulu; Asema Nape Nauye

nape-mjumbe.jpg


Akizungumza katika mahojiano na Radio Safari ya mjini Mtwara hivi karibuni Nape amesema serikali ya Rais Jakaya Kikwete ndiyo pekee katika nchi hii iliyokwisha kutoa maamuzi magumu kuliko serikali zote zilizopita.

Nape amenukuliwa akisema...." uamuzi mgumu wa kwanza uliotolewa na serikali ya awamu ya nne ni kwa yeye Lowassa kulazimishwa kujiuzulu, kuvunjwa Baraza la Mawaziri, kuwafungulia kesi kina Mramba na Yona, kuivunja kamati kuu ya CCM na sekretarieti, Ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma na Ujenzi wa shule za kata".


Ufisadi unalipi naona Nape kanenepeana ile mbaya kwa siku chache tuu toka aingie kwenye uongozi wa Magamba
 
Maamuzi mengine magumu aliyofanya Jk ni kumshika mkono juu na kumnadi Pesambili Mramba na kusema jembe la zamani haliishi makali! Chukua hiyo Nape ukipenda naomba uipotezee!

Maamuzi mengine magumu ni pale JK alipomnadi EL pale Monduli akiwashawishi wananchi wamchague kuwa mbunge wao huku yeye akiwa amemshinikiza ajiulu Uwaziri Mkuu, Nape uko hapo?
 
Ata kujichekesha chekesha mbele za watu,uku watu wako siriaz ni uamuzi mgumu sana..
 
Napata shida hivi alijiuzuru au alisitaafu jamani mbona mnanipa taabu sana kufikiria sasa analipwa mshahara wa kusitaafu kama aliyekuwa kiranja mkuu wa nini?
 
sawa hayo yalikuwa ni maamuzi magumu, kwahiyo ndio anaishia hapo hapo? tunahitaji aendelee na maamuzi magumu ndiyo maana anasisitizwa afanye maamuzi magumu tena. kipindi kile ayafanye watanzania walifurahi, sasa kwanini haendelee. tanzania inawezekana bila RACHEL kuwa madarakani wala asihofu.
 
Najamaa huyo akasisitiza kuwa serikali ya JK ndio iliyoongeza nafasi za ajira za WATANZANIA
282786_240774025947163_100000437012547_880847_4493548_n.jpg
 

NA MOJA YA KIELELEZO CHA MAAMUZI MAGUMU NI KUENDELEA KUVUMILIA MAWAZIRI WASINZIAJI KAMA HAWA HAPA KWENYE CABINET
261325_175684172493219_100001549126150_454564_1619470_n.jpg


188665_1710919125756_1021446937_31590340_633794_n.jpg
 
Maamuzi magumu aliyafanya Lowassa kwa kukubali kujiuzulu, angegoma kujiuzulu LABDA ndo tungeweza kuona uamuzi mgumu wa JK.
 
Nape kaongea clouds fm sasa hv mafanikio ya sera ya kujivua gamba hadi sasa ni kwa hoja hiyo kujadiliwa na watu mitaani vijiweni na hadi kufikia wengine kutaniana kuwa ntakuvua gamba duh kumbe nia ilikuwa ni watu wajadili hoja duh kweli CCM mmepiga bao juzi baamedi kaniletea ya baridi nikamwambia nimeagiza moto kisha akanijibu kuwa nimejivua gamba kweli haya ndio yalikuwa malengo ya sera ya ccm nimepata picha kamili sasa hv baada ya nape kuongea mwenyewe!!
 
Big up nape tumekupata napendekeza muwasilishe mtaala ili somo la kuvua gamba lianzishwe shuleni
 
Jamaa angu alikuwa anakaa hapa mtaani alikuwa kiwembe sana,kapata mchumba akahama mtaa,akanambia anavua gamba,ila akifika huko wembe ule ule tena zaidi.
 
CCM karibia viongozi wengi ni empty kabisa so nashangaa sana hii nchi tunaendeshwa vipi,maana hata kiongozi wa hii nchi simjui ni nani......
 
Back
Top Bottom