MOI Wajiunga Tena na MGOMO

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,006
1,254
Ni baada ya mabadiliko ya hali ya Ulimboka.

Wagonjwa waliokwishalipia tu ndo wanaonwa leo.

Emergence yasimama.

Source: Mimi niko ground zero

UPDATE:
Kutoka gazeti la Mwananchi
Huduma za matibabu MOI zasimama tena
Taarifa za kutatanisha kuhusiana na hali ya Dk. Ulimboka, zilisababisha kusitishwa kwa huduma za matibabu katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) baada ya madaktari karibuni wote kwenda katika mkutano wa dharura kujadili tukio hilo.

Habari za kuaminika kutoka MOI, zimethibisha kuwa taarifa za kuzidiwa na hata kuzuka kwa habari nyingine kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, ziliwachanganya kwa kiasi kikubwa madaktari hao, ambao walilazimika kusitisha huduma na kuwapangia wagonjwa tarehe nyingine za kurudi.

Kutokana na hatua hiyo ya madaktari, wagonjwa waliofika MOI baada ya kusikia kwamba huduma zimerejea, walishindwa kupata tiba badala yake waliandikishwa majina, wakalipia na kupewa tarehe ya kurudi kwa madai kwamba hakuna madaktari wa kuwahudumia.

Taarifa ya kurejea kwa madaktari hao ilitolewa juzi hospitalini hapo jana na Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Balozi Charles Mtalemwa na kusisitiza kwamba hospitali hiyo haiko katika mgomo kwa sasa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa waliokosa tiba, walidai kuchoshwa na usumbufu huo huku wakiwaomba madaktari hao kurejea kazini.

"Nimekuja hapa tangu saa moja kulikua na foleni; wenzetu waliowahi walionana na madaktari lakini ilipofika saa nne tukaambiwa wote tuliojiandikisha turudi Alhamisi ijayo kwa sababu madaktari wanaenda kwenye kikao," alisema Abdallah Haji mkazi wa Kimara.

Kwa upande wake Jenipher Suka alisema inasikitisha kuona hivyo kwa sababu mama yake ambaye ni mgonjwa mkazi wa Dodoma amekuja akitegemea kupata tiba matokeo yake ameambiwa arudi tarehe 10 mwezi huu kwa kuwa hakuna madaktari kwa sasa.

"Kwa nini serikali isiseme ukweli maana tunahangaika kuja mpaka huku halafu hakuna huduma? Vyombo vya habari vimetangaza kwamba mgomo umesitishwa lakini bado wanatudanganya wananchi kwa faida ya nani?" alilalamika Jenipher.

Akizungumza kwa sharti la kutochapisha jina lake gazetini mmoja wa maofisa waandamizi wa hospitali hiyo alikiri kutokuwepo kwa huduma baada ya madaktari kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka.

"Unajua huduma zinazoendelea kwa sasa ni kliniki na upasuaji kwa waliowahi lakini hawa madaktari wamechanganyikiwa baada ya daktari mwenzao aliyeongozana na Dk. Ulimboka kuwaeleza kwamba hali ya mgonjwa ni mbaya mno.

Kukosekana kwa huduma kulichangiwa na madaktari wanafunzi ambao hupokea na kuwahudumia wagonjwa kuwa katika maandalizi ya mitihani ya mwisho wa mwaka itakayoanza Jumatatu ya Julai 9, 2012 hivyo kusababisha huduma utoaji wa huduma kutokuwepo kabisa.
 
Nadhani this time Kikwete ndo atatafuta mwajiri mwingine na si madaktari.
 
Homa inapanda na kushuka,
Wananchi sasa ndo watagoma barabarani kwa niaba ya madokta
 
Jamani, hii serikali ya aina gani? Mbona kama kuna uhuni unaendelea. Mara Lugalo Hospitali ya rufaa, wakati ya Muhimbili inawashinda.
 
Ni baada ya mabadiliko ya hali ya Ulimboka.
Wagonjwa waliokwishalipia tu ndo wanaonwa leo.
Emergence yasimama.
Source: Mimi niko ground zero

kama mvua za kiangazi,,,,,,,,inanyeshaaa inakata,,,mara inanyesha gongo la mboto ila ukonga kuna manyunyu,,,,,kesho mnaskia ipo msamvu tu,mazimbu jua kaliii,usiku inapiga mlali hadi mafuriko,lakini milima ya SUA kukavuuuu,,,,,,,,
kinachofanyika sasa ni paka na panya wanatekenyana,wao wanaskia raha kutekenyana kwao
 
Ni baada ya mabadiliko ya hali ya Ulimboka.
Wagonjwa waliokwishalipia tu ndo wanaonwa leo.
Emergence yasimama.
Source: Mimi niko ground zero
Kwani afya ya Ulimboka ni muhimu sana kuliko afya za wagonjwa walioko hapo muhimbili?
 
Safari hii Liwalo na Liwe, Dhaifu sijui watasema nini?
Madokta kutoka Iran haiwezekani tena, washalikororoga na bendera zao.
 
Waliohamasisha mgomo kwa manufaa ya kisiasa, wameaibika. Haya nendeni mkawashawishi wanajeshi LUGALO kugoma!!
 
Mkuu mabadiliko ya hali ya ulimboka yanahusiana nini na shughuli za MOI tena?si yalishaisha na wamerejea kazini.au kuna mengine ebu tujuze coz waleta uzi wanaleta news in kidusu dusu form
 
Back
Top Bottom