MOI: Mgomo wa Madaktari Bingwa unaendelea

Serikali ilishasema (JK) kwamba hawana kitu cha kuongea na madaktari, kama daktari haridhiki na achomoe aende atakako. Na kweli wengi sana wameenda nje kuhudumiwa mara saba ya hapa, wanawacheka waliobaki. Hao waliobaki ni kwa sababu hawataki kwenda nje ili waionyeshe serikali kwamba Tanzania sio ya wanasiasa tu, ni yetu sote. Halafu kumbuka Kayaanza mizengwe pita pinda kwamba liwalo na liwe na likawa. Madaktari wamezibwa midomo na kila atakayeongea analimbokiwa. Wote twataka kuishi, hakuna daktari mjinga wa kujining'iniza kamba shingoni wakati watu kibao wanamtegemea, na watoto wao huzaliwa uzeeni sababu miaka mingi wako shule. Waandishi umeona nao wakiisema serikali kwamba inatupeleka ndiko siko wanawadaudi. Kwa hiyo mambo kimyakimya, wananchi waendelee kuishabikia serikali yao maana imeona kwamba ndo inalipa.
hapo kwenye red serikali itapata wakati mgumu sana ndani ya muda mfupi na si serikali tu bali wananchi haswa maskini walala hoi
 
maswali yap? mkuu nakumbuka we huwa unawaponda sana hawa jamaa....nakumbuka kuna thread uliwaponda sana jamaa mpaka kuna jamaa ikabd atupe ufafanuz wapo kumbe nawe pia ni dr ..........

Si kuponda kiongozi. Kuna wakati unaona tatizo halafu utatuzi wake uko obvious, lakini maswali yanakuwa mengi kuliko majibu pale inapoonekana watu wanaojua utatuzi wanaamua kufuata njia inayotengeneza matatizo zaidi katika fani!!!
 
wao wanatibiwa india, uingereza nk hawana muda na na wananchi, hata hivyo waziri wa afya si alisema madaktari bingwa hawahitajiki?
 
Pole sana ndugu kwa kuuguliwa nimesoma post yako lakini hali halisi sio kwamba kuna mgomo MOI suala la wagonjwa kulala chini MOI ni la kawaida miaka yote labda hujawahi kufika kabla wagonjwa ni wengi sana . sio MOI tu muhimbili mugonjwa kulala chini ni kawaida maana vitanda na majengo hayatoshi . kuhusu suala la kuruhusiwa kuingia ndani napenda nipingane na wewe kwa utaratibu uliopo ndugu wa wagonjwa wanaruhusiwa jion saa kumi ila saa sita huwa anaruhusiwa mtu mmoja kwa ajiri ya chakula , hii ni kwa ajiri ya kuruhusu shughuri za matibabu kuendelea na kutoa muda wa wagonjwa kupumzika fikiria kila wakati ndugu wawemo wodini wakati huo huo wagonjwa wanatakiwa wapumzike itakuaje. kwa hali halisi morali ya wafanyakazi iko chini sana maana mazingira ya kazi fikiria wagonjwa kumi na tano wamelala chini nurse mmoja ainame kuwahudumia maumivu ya mgongo anayopata sijui, ni kawaida kwa wagonjwa arobaini mpaka hamsini kuhudumiwa na nurse mmoja au wawili tu.Hali ni ngumu watu wanapogoma watu wanafikiri ni siasa lakinii inauma .
 
Jogi,

Niseme tu kwamba nimeandika bila kusukumwa na mtu isipokuwa kwa nia ya kuona tatizo linajadiliwa na hatimaye kupata ufumbuzi. Hebu fikiria imefikia mahali mgonjwa anajilaumu kwa nini amekosa pesa za kulipia matibabu yake kwa njia ya rushwa! Mgonjwa anajilaumu mwenyewe. Anamlaumu ndugu yake mwenye kauwezo kidogo lakini hajaonekana kipindi hiki cha shida. Mgonjwa anasema zingepatikana shilingi kadhaa kuna madaktari walikuwa tayari kunifanyia upasuaji. Mgonjwa analia kwa uchungu mwingi.

Jogi,
Ninaamini kwamba mgonjwa, na hata binadamu yeyote, akifikia hatua hii anakuwa kwenye kiwango cha juu kabisa cha utambuzi. Hachukulii matatizo yake yanatokana na wengine bali yeye mwenyewe. Hamlaumu mama yake, baba yake, serikali, wala mazingira. And at last this very person surrenders to God! He/she starts to prepare himself/herself for life after death!

Mkuu Pius Kafefa,
nimerudia na kurudia na kurudia, bado ufahamu wangu unaingiwa tashwishwi na hiyo sentesi inayoitaja serikali. Nazingatia kuwa kwa sasa serikali iko busy sana kujisafisha, ukifuta maandishi hayo yanayookumbatia serikali ya ccm, naweza kuchangia zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Lakini mkuu, nini kifanyike? ...kwani hata wagonjwa unaowaona pale, wengine ni wa mikoani!! yaani wamepewa Referral tu kuja MNH or MOI sasa shida inaanzia kule kile yaani vifaa na huduma yenyewe!
Hapa cha kufanya inategemea ni nani afanye nini, JK anasema hana cha kujadili na madaktari, madaktari wameamua kuonyesha professional arrogance, Pinda kasema liwalo na liwe sasa limekuwa, wagonjwa hawatibiwi ila wenye pesa wanatoa hongo wasio nacho wanakufa bila rekodi, dhaifu anaenda kutibiwa ulaya na jamii yake, madaktari waliosomeshwa kwa kodi zetu kubwa wanaenda ulaya, bondeni hadi marekani wanakojaliwa. Kifupi nchi haitawaliki tena, wenye jukumu wamejibinafsisha na kuwajibika kwa wapendwa wao tu. Let everybody for him/herself and God for us all, let the satan take the hindmost. JK 0 vs Madaktari 0
 
Mkuu kapongoliso, that happen when politics hit proffesion...kila mtu anajifanyia vyake, ila mimi nilikuwa nashindwa kuwaelewa wananchi wenyewe walikuwa wanaona madai ni ubinafsi mtupu sasa kidogo wanapata kuelewa waliyaelewa madai vibaya.
 
Nianze kwa kuwapa pole wagonjwa wote waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili.
Nilifika Muhimbili kwa mara ya kwanza siku ya Alhamis tarehe 13.09.2012, majira ya saa nne na nusu asubuhi. Baada ya kutoa maelezo kwa walinzi wakanishauri nisubiri hadi saa sita na nusu mchana ndiyo ningeruhusiwa kumwona mgonjwa niliyeenda kumjulia hali. Nikasubiri.

Muda huo ulipofika nikaingia na kuongoza moja kwa moja hadi wodi ya Mwaisela, namba 2. Hapo nikakutana na kikwazo. Walinzi wawili na muuguzi mmoja walikuwa wanahakiki watu wote wanaopita hilo lango la kuingia wodini. Ilani ikatolewa wenye chakula tu ndiyo wanaoruhusiwa kuingia.

Katika mchujo huo wote waliokuwa na juisi, maji, na matunda wakazuiliwa na hao walinzi. Kwangu mimi ambaye sikubeba chochote ilikuwa ni ngumu zaidi kueleweka. Akaja kijana mwingine aliyeonekana amevalia nguo nadhifu, mkononi kashika Biblia na kitabu cha maombi. Akasema amekuja muda huu kwa ajili ya kufanya maombi kwa Mungu kwa ajili ya mgonjwa wake aliyelazwa wodi hiyo. Akaambiwa "hakuna kuingia, huu ni muda wa chakula kwa wagonjwa, muda wa kuona wagonjwa ni saa kumi".

Baada ya msongamano kupungua nikamfuata Mzee mmoja aliyeonekana anasaidiana na walinzi. Nikamwambia: "baba nina dharula, nahitaji kumwona mgonjwa wangu muda huu ili nijue mahitaji yake, siishi mji huu (Dar) na ninahitaji kufahamu mahitaji yake mapema kabla ya saa kumi." Mzee yule akaniambia nimweleze yule kijana mlinzi aliyenizuia, tena niseme kwa hisia zile zile kama nilivyokuwa namweleza yeye. Nikamsogelea tena yule mlinzi na kumweleza. Yule kijana akaniambia: "nenda, halafu kata kulia". Nikaingia.

Nilipofika mlangoni nikaanza kuona wagonjwa waliolala chini, kwenye korido ya kuingia wodini. Nikasita kwa kudhani labda nimekosea. Nilipoenda mbele kidogo nikatokeza chumba cha kulaza wagonjwa. Wagonjwa walikuwa ni wengi sana. Wamejaa hadi wengine kulazwa chini. Nikaanza kuangaza huku na kule nikimtafuta mgonjwa wangu! Nikamkuta mahali akiwa amelala, chini. Vitanda vimejaa!

Akiwa katika siku ya nne toka afike alikuwa bado hajaelezwa kama atapatiwa matibabu lini. Yuko MOI. Sehemu ya wataalamu bingwa wanaotegemewa kuokoa maisha yake. Hapa hayuko peke yake. Wapo wagonjwa wenzake wengi. Na wengine walikuwa wanalia kwa maumivu makali.

Kwa nini nasema MGOMO BADO UNAENDELEA?
  1. Wagonjwa wameongezeka na kufikia hatua ya kulala hadi kwenye korido. Kasi ya kuwatibu ni ndogo.
  2. Wale wanaoweza kutoa rushwa wanalazimika kulipia operation kwa siri. Unaweza kulipia shilingi ngapi, lini, kwa nani ndicho kigezo kwa sasa. Siwasingizii madaktari.

Ilipotimu saa nane kasoro dakika tano kengele ikalia ikiashilia muda wa kuwapa chakula wagonjwa umekwisha. Nikasubiri hadi dakika tano baadaye ndo nikainuka pale sakafuni nilipokuwa nimekaa. Nikaanza kutembea kurudi nilikotoka huku mawazo tele yameniandama.

Baada ya kufika geti la kutokea nikaona maandishi "OFISI YA MAONI/MALALAMIKO YA WATEJA". Nikashtuka! Nikawa nahaingaika moyoni kama niende kutoa maoni au nisiende. Baadaye nikaamua kwamba sitaenda kutoa maoni yangu kwenye kile kiofisi. Nikajiuliza kwani maoni yangu:
  • atakayeyapokea ni nani?
  • atakayeyachambua ni nani?
  • atakayeandaa ripoti ni nani?
  • atakayepokea ripoti ni nani?
  • atakayefanyia kazi mapendekezo ya ripoti ni nani?

Nikafikia uamuzi. "JAMIIFORUMS.COM". Sikuwa na kompyuta siku ile, na simu yangu ndo hizi za bei poa. No intaneti. Nikaondoka na kuchukua dala dala kuelekea Ubungo. Kichwani mawazo tele! Huu mgomo nani anaujua? Hivi sakata lenyewe liliishaje? Dr. Ulimboka yuko wapi? Dr. Mkopi anaendeleaje na kesi yake? Je, ana mashahidi wa aina gani watakaowezesha asipatikane na hatia? Serikali nayo je, imeweza kudhibiti mgomo au imeuahirisha tu? Je, madhara ni yapi?

Lakini pia nikajiuliza hivi chakula hasa ni kitu gani? Je, Watanzania wanaelewa maana hasa ya chakula? FIKIRIA: maji tu, hapana. Machungwa mawili matatu, huingii wodini. Umebeba Juisi, No. Eti "NI KWA WALE WANAOPELEKA CHAKULA TU". Nikawafikiria pia viongozi wa kiroho ambao wanatumia Biblia. Imeandikwa kwamba neno la MUNGU ni CHAKULA cha uzima.

Nikiwa wodini, hata hivyo, wagonjwa na ndugu zao wengi walikuwa wanawalaumu madaktari. Wagonjwa wengine walikuwa wanawalaumu ndugu zao ambao wameshindwa kuchangia HONGO ili wafanyiwe upasuaji kwa wakati. Kwa kweli neno serikali sikulisikia. Pia Mungu alikuwa ametawala kwenye vinywa vya wengi. Nami naungana nao kwa kumwomba Mungu awatie nguvu ya kuvumilia machungu yote wanayoyapata, huku wakitumaini wokovu wake. AMEEN!
Ndugu yangu naona wewe huijui MOI,Hicho ulichokiona ndiyo hali halisi ya MOI wala haina uhusiano na mgomo.Ni rushwa kwa kwenda mbele na wagojwa wa ajali ni wengi na wodi ni ndogo.
 
Back
Top Bottom