Mohamed Trans yapinduka na kuua

KAUDO

Senior Member
Aug 10, 2011
138
67
Basi la Mohamed Trans lililokuwa linatoka Dar kwenda Bukoba limepinduka eneo la Kyetema kilometa chache kabla ya kufika Bukoba na kusababisha kifo na majeruhi.

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Kagera Marison Mwakyoma amethibitisha na kuwa alikuwa anaelekea eneo la tukio.

Tayari abiria mmoja amepoteza maisha na wengine wako hahututi hospitali ya mkoa.
 
Duh!wiki ya usalama barabarani mkoani Kagera na bado ndani ya wiki moja the bus overturns?tunamshukuru Kikwete na sie hatutaacha kuwazika bandugu betu lakini ccm ikae ikijua,IPO SIKU.
 
Duh!wiki ya usalama barabarani mkoani Kagera na bado ndani ya wiki moja the bus overturns?tunamshukuru Kikwete na sie hatutaacha kuwazika bandugu betu lakini ccm ikae ikijua,IPO SIKU.

hapo ccm imehusika vipi?. Tuache ushabiki usio na maana.
 
Ninavyofikri kwa sasa serikali ifikilie namna ya kudhibiti hizi ajari..Ajari imekuwa kama sehemu ya Maisha yetu..
 
Road accidents are second to Malaria in causing deaths and disabilities in Tanzania, UN report says. In the first half of 2011 alone, more than 20,000 souls perished in road carnages while 5,000 others were critically maimed. The figure only indicates number of casualties which was reported and officially compiled, without considering unreported accidents.
 
Kuna haja ya kuja na radical measures to reduce road accidents.Binafsi sipendi dereva kijana,hawa wengi wanakesha bar na kuzini usiku then asubui tunawakabidhi mabasi,matokeo ni kuendelea kutuchinja.Dereva mwenye familia mara nyingi ni makini zaidi,sheria ipitishwe ya kuwazuia vijana chini ya umri wa miaka 30 kuendesha mabasi ya abiria kwani vijana wengi kwa kutokuwa na familia na umri mdogo wanakuwa less responsible.
 
Poleni wafiwa. Tunawatakia nafuu ya haraka majeruhi. Tunataka kuona ushirikiano kutoka serikali kama ilivyokuwa kwenye msiba wa yule Mchina ,maana ajari zimekuwa nyoka hatari anayeua watanzania kila uchao huku serikali kazi yake kutuma rambirambi tu.
 
Mohamed Trans nayo ifungiwe, nadhani katika mabasi yanayoongoza kwa ajali nalo hili lipo kwenye orodha! Poleni wajeruhi wote na nawaombea kwa Almight God mpate nafuu.
 
Poleni wafiwa. Mungu awajaalie waliojeruhiwa kupona haraka na kurejea kwenye shughuli za ujenzi wa familia zao
 
Hapo juu mkuu (Mzee) kataka kujua ccm inahusika vipi,ni hivi ccm ndo chama kinachotoa dola na si vinginevyo na kwa vile chama kipo ili kutoa mwongozo kwa serikali na serikali inatekeleza ilani inawezekana chama kimeshindwa kuona tatizo la ajali kama ni tatizo na hivyo kushindwa kuishauli na kuielekeza serikali...chama legelege daima kinazaa serikali legelege (EL falsafa i.e,tenganisheni kofia)

Hiyo ni moja,pili ni jukumu la serikali kulinda maisha ya raia wake,sasa leo ndugu zetu wanachinjwa kama kuku barabarani kwanini serikali imekaa kimya?na kwanini chama kimekaa kimya?ama hakina washauri?
Sasa tumlaumu mtoto ama mzazi kwa kutokuwajibika katika kumlea mtoto na kumtunza

Mkuu hoja yangu iko hapo,siilaumu serikali ila chama maana chama ndo kilishinda ili kuunda serikali
 
Subirini salam za JK za rambirambi!! Yani sijui lini ajali zitakwisha..And bad enough it seems no one is responsible....Mungu tuepushie mbali!! Get well son majeruhi...
 
yooo mawe! Kyetema,balabala mpya,kibeta,rwamishenye,kwa fokasi stendi km chache tu kufika wanaua kesho narudi home kulivalia njuga lazima nionekane mshari kwa hili! Inamaana kale kakona ndiko kaliko mshinda..
 
Back
Top Bottom