Mods: I Suggest a Stick Thread for Nape, Napeism and Napeists

English Learner

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
355
355
After going thoroughly through JF for sometimes, I am convinced that time is up for Mods to create a single sticky thread for NAPE , NAPEISM and NAPEISTS. Let us not keep on starting New threads every time we want to advise, criticize, or condemn NAPE. Some of these inputs are repetitious. So let us consolidate them in a single voluminous sticky thread.

For example analyze the message contained in following messages from different thread, it is the same ONLY the boy is big-headed

Watu hufikiri kuwa, labda jinsi pekee ya kummaliza mwanasiasa ni kwa kumhonga pesa/kumnunua au kumtoa uhai, LA HASHA. Hakuna njia nzuri kabisa, yenye matokeo bora yasiyo na ghalama kubwa katika kummaliza mpinzani wako kisiasa kama:

KUJUA VEMA udhaifu wake na kuufanya kuwa FAIDA kwako. Kila mwanadamu ANA udhaifu wake. Kanuni hii pia inayofanya kazi katika Nyanja mbalimbali za maisha mfano katika Biashara.


Wapinzani wa Nape wameujua vema udhaifu wake. Na nampa heko aliyewasaidia kuubaini. Udhaifu wa Nape ni mkubwa katika wepesi wa matamshi/maandishi mazito anayotoa katika hadhi yake kama Katibu Mwenezi. Hapa ndiko wapinzani wake ndani na nje ya CCM wanapojizolea maksi za ushindi vitani. Ukiishagundua huu udhaifu na kubaini kuwa kila tamshi la adui yako ni tata, lisilo na hadhi, lenye kejeli, na kuudhi hadhira, na wakati mwingine ujumbe anaotoa siyo wake kazi unayobaki nayo ni rahisi sana. Utamtengenezea misururu ya waandishi wa habari na kumuandalia matukio na hadhira ili ahutubu. Maana unajua kila baada ya tukio, ujumbe wake ukifika kwa hadhira, heshima na mvuto wa mtoa ujumbe vinashuka.

Awali watu walipomwita Nape vuvuzela ilinipa taabu kuelewa walimaanisha nini. Wajua wakati mwingine kama huna kamusi na umekutana na neno jipya katikati ya sentensi, inabidi utumie uelewa wa maneno yale mengine kupata maana ya sentensi. Sasa naweza kupata maana yake kama bomba tupu linalopitisha upepo wa mpulizaji na kutokea upande wa pili kwa sauti pana. Vuvuzela halipitishi ujumbe wake lenyewe na wala halichuji kinachopitishwa. Matamshi na maandishi ya Nape yanampa sifa ya kulichukua jina hili.

Kuna mambo Nape anabolonga kama vuvuzela na kuna mengine mengi anaharibu kutokana udhaifu wake wa kuanzisha ama kuchangia mijadala kwa kutoa hoja nyepesi kwenye masuala mazito. Na mbaya ni kwamba, yeye kila akiletewa MIC anakuwa kama mtoto kaletewa vanilla ice cream, lazima alambe! Akipigiwa simu na mwandishi anahisi yeye ni Encyclopedia Britannica, majibu yote anayo na ni sahihi! Na kwa sababu ya kuwa pitishio la ujumbe asio uasisi, kuendelea kuonyeshaa udhaifu wa Nape pia ni kuanika udhaifu wa anayepitisha ujumbe kwa Nape.

Angalia hii mifano halisi:
  • Kauli za Nape juu ya msimamo wa kujivua gamba
  • Hotuba ya Nape kwenye Mkutano wa Mwanza juzi - "Nawashukuru Lusinde na Mwigulu kwa utangulizi wenu. …..mmenisaidia kuwabana wagonjwa pua ili mimi niwape dawa"
  • Nape kukana maandishi yake mwenyewe juu ya matokeo ya Igunga kwenye ukuta wake FB na ID yake JF
  • Kutowajua hata wapinzani wake nje ya CCM (Dr. Slaa na Mbowe-hii bado mbishi kabisa)
  • Kauli tata katika midahalo – Ujamaa wa ki-sayansi umepitwa na wakati. Ukiachana na sayansi unashikana na arts (sanaa). Hivyo anamaanisha ccm iko kwenye zama mpya ya ujamaa wa ki-sanii-GOOD! -ccm bado inayaenzi yote aliyoyaanzisha Baba wa Taifa ikiwemo Azimio la Arusha.
Nape anamalizia pumzi yake ya mwisho ya uhai kisiasa. Namshauri ayapokee maoni yangu kama changamoto na yanaweza kumsaidia. Mimi si wa kwanza kumwambia juu ya suala hili. Radio Producer (member JF) naye amewahi kumshauri. Na tunafanya hivi kwa sababu tunamtaka arudi kwenye mstari kwa manufaa ya anachofikiri anakipigania.

Najua nafasi uliyonayo ni nafasi za watoto wa vigogo ila hilo tuachane nalo.
Ndugu yangu nape kazi unayofanya kukiimarisha chama chako kwa mikutano na maandamano ni kazi bure. Nini serikali yako ya CCM ifanye ilikukiimarisha chama:-

(1)kupambana na mfumuko wa bei ya vyakula na huduma za msingi zinazomgusa mwananchi moja kwa moja.

(2)kuongeza pato la mtu mmoja mmoja, hii hasa kwa wafanyakazi,wapeni mishahara itakayowawezesha kuishi,tofauti na hapo hawa ndo watakaowamaliza 2015...mkilifanikisha hili nakuapia hamtapata upinzani wowote

VIDEO
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ti-ya-kikwete-ikulu-itaweza-kumjibu-lema.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/272425-ccm-muhurumieni-nape-ameanza-kuchanganyikiwa.html
 
Back
Top Bottom