Modern-Day Slavery on D.C.'s Embassy Row? [Afisa Balozi wetu Mzengi na Utumwa mpya?]

Huwa nawaambia kabla ya kutukana angalieni historia huyu Balozi ndie mdhamini Wa kwanza wakati CHADEMA inaanzishwa see the records....
Haya ndo mambo yanayonikera... Watu wanaongelea maslahi ya taifa, we unaleta maswala ya udhamini wa chama... Kwahiyo unataka kusemaje? Kwasababu aliidhamini CHADEMA basi ye ni mtakatifu?... Fikiria!
 
Kwani ni kosa gani alilofanya mpaka kupigwa faini, labda ni ujasusi huohuo. Sijaelewa hii topic:help:
 
What a crap...tied of all these nuisance.....there comes a time people will stop dreaming and act...God make me see that day soon. Bless are those dead protect integri
 
huyu bwana alikuwa jasusi wetu kule marekani isije kuwa alifanya ujasusi wamarekani wameamua kumkomoa kupitia msichana wake wa kazi.
 
mjadala wetu usijikite nani anatakiwa kulipa bali sheria na matokeo ya hukumu, muda wa kulipa na kama hazitalipwa kwa muda uliowekwa na mahakama ni nini kitatokea kwa mzengi mwenyewe na taifa kwa ujumla na ndipo tutaweza kushauri kupitia jukwaa hili nini kifanyike.
 
Ni muhimu tukapata baadhi ya majibu ni kwa nini barozi alitoa ushauri huo? kusoma barua na kile kilichoko nyuma ya barua ni mambo mawili tofauti. Tukumbuke huyu bwana alikuwa jasusi!!!!!!! inawezekana barozi na Rais wanaijua siri hiyo na hawaezi kuinika katika barua.

Lakini kama watanzania tuna uhuru wa kuhoji ingawa kwa tahadhari tusiumbue ujasusi wetu kama ndio umetumika kumuadhibu huyo jamaa kwa kivuli cha house girl. Adhabu yenyewe ni kubwa mno kwa kumlipa mfanyakazi wa ndani japo sheria ziko tofauti kati ya nchi na nchi.
 
Iliyoshitakiwa siyo serikali ya Tanzania? Hivi vijitu vya kwenye ubalozi vinajifanya vyenyewe ndio nchi na vinajifanya vina kila sababu kutumia pesa za walipa kodi vibaya.

Kwa nini akopeshwe kiasi kikubwa namna hiyo cha fedha na serikali? Serikali siyo bank pumbafu kabisa aende kukopa bank na huyu balozi ndio kundi lile lile la mafisadi.
 
wapinzani hawajaipata hii? dr slaa.mbowe,lisu, dr rwaitama,mvungi, membe nae atasemaje kwa hili? I hope inabidi JK ashinikizwe amrudishe huyu mama tanzania mara moja haiwezekani kuandika barua ya kipuuzi namna hiyo alafu aendelee kubaki kuwa balozi.Balozi anatakiwa atetee maslahi ya Tanzania kwa manufa ya Watanzania lakini sii kutetea maslahi ya mtu mmoja.

Shame on her. Nasema hastahili kuwa bolozi wa Tanzania kwa akili zake za kihiyo.
 
Makosa ya maafisa wa ubarozi mahali pengi duniani yanachulikiwa kama ni makosa ya nchi na ndio maana ofisi za kibarozi zikivamiwa au kushambuliwa inahesabika ni nchi iliyovamiwa na kinga ya maafisa hao iko wazi na mara nyingi wakipatikana na kosa wanafukuzwa na sio kufungwa kwa sababu wao wanasimama badala ya nchi sio kama watu binafsi.
 
Endapo sheria ya marekani inahusisha serikali yetu katika kosa hilo ni bayana kwamba kwa mtanzania wa kawaida kulipa deni la zaidi ya shilingi milioni 200 kwa mpigo tena afisa ubalozi labda awe fisadi.

Kimsingi, barua imesema Dr Mzengi kakubali kulipa lakini kwa awamu lakini mlalamikaji hataki kulipwa kwa awamu ni wazi kwamba nyundo hiyo itapigwa serikalini na serikali ndio itakayojua namna ya kurejesha fedha yake kutoka kwa mzengi.

Tujadili tuone kama kuna mantiki au la.
 
Kimsingi barua inasema kosa la Mzengi limewekwa kwenye hatia ya usafirishaji haramu wa watu kwa sheria za marekani. Japo binti Zipora alikuwa msichana wake wa ndani hatujui ni kwa nini alimgeuka bosi wake na hata kumfungulia kesi huko marekani wakati wote ni watanzania na Zipora alipelekwa huko na Mzengi kama msichana wake wa ndani kutoka Tanzania.
 
mjadala wetu usijikite nani anatakiwa kulipa bali sheria na matokeo ya hukumu, muda wa kulipa na kama hazitalipwa kwa muda uliowekwa na mahakama ni nini kitatokea kwa mzengi mwenyewe na taifa kwa ujumla na ndipo tutaweza kushauri kupitia jukwaa hili nini kifanyike.
mbu sugu, asante kwa hii observation yako.

Wanabodi, naombeni tusikurupuke kumshutumu Balozi Maajar.
Maofisa wote wa ubalozi wa nchi zote, wanalindwa na kitu kinachoitwa Diplomatic Immunity under Vienna convention ambapo ofisa ubalozi haruhusiwi kishitakiwa kwa kosa lolote la jinai, ila akifanya jinai huku ana kinga ya kibalozi, then atashitakiwa yeye binafsi, ila nchi husika hutakiwa kufanya haya yafuatayo kwa haraka kadri iwezekanavyo.

1. Kumvua kinga ya kibalozi, hivyo kumruhusu kusimama mahakamani na akikutwa na hatia, huwajibika binafsi hata kama ni jela hufungwa.
2. Nchi husika humrejeshas nyumbani kwa haraka, hivyo kumpatia shield aganst local prosecution, hiki ndicho Tanzania ilichokifanya na ndicho kinachofanywa na nchi nyingi.
-Wale Wataliano waliowalazimisha dada zetu kulala na mbwa ndio waliokolewa kihivi
-Wanabalozi fulani wa nchi ya kiarabu alimbaka msichana wake wa kazi na kuokolewa kihivi
-Mwanabalozi wa Canada aliyemtemea mate Jerry Muro, pia iliokolewa kihivi.
3. Lengo la kuwarejesha nyumbani maofisa hao ni kukwepa legal liability kwa sababu ili kuendesha kesi ya kihivyo, unatakiwa kutumia Private Internation Law ambayo legal fees zake ni very expensive.
4. Huyu binti ametetewa na wanasheria wa msaada wa kisheria, na kushinda kesi. Kwa vile mhusika alitenda kosa akiwa na kinga ya kibalozi, na Tanzania haikumuondolea kinga bali kumrejesha tuu nyumbani na kumpa kazi nyingine, serikali ya Tanzania haiwajibiki kwa deni lake, wala haiwajibiki kulipa, kumlipia, wala kumkopesha bali kitendo cha ofisa mhusika kushindwa kulipa, kutaichafua Tanzania mbele ya jumuiya ya kimataifa.
5. Anachosema balozi Maajar, ni just saving the face of Tanzania, tusikubali kuacha jina la Tanzania likichafuliwa eti kwa sababu ya mpuuzi mmoja aliyefanya mambo ya kishenzi kwa kasichana ka kazi.
6. Kama ilivyo kwa mtoto chini ya miaka 18, akifanya jinai ya madai, mzazio wake atawajibika kumlipia to save his face, ndivyo hivyo Tanzania inavyowajibika kumlipia mpuuzi huyu to save our face!. Balozi Maajar is right.
7. Hii sio mara ya kwanza kwa ofisi za ubalozi kulipa madeni ya watu binafsi na huku serikali ikiwadai wahusika. Kwa wenye kumbukumbu mtakumbuka kisa cha mtoto wa Msekwa ughaibuni, alichuma janga, Baba wakati huo akiwa spika, akakopeshwa, soo likamalizwa, huku nyumbani Msekwa akadaiwa na kulipa mwaka juzi!.
 
Mimi nimevutiwa zaidi na hitimisho la balozi kwamba kwa sababu alizozitoa katika barua hiyo, serikali imshinikize Dk. Mzengi kulipa deni lote kwa mkupuo au uangaliwe uwezekano wa kumkoposhe fedha apate kulipa lote ( ushauri huu naamini umejengwa kwa taratibu za kinga za kibalozi kwa kosa lake kuwa ni la nchi ya kibalozi ndani ya marekani).
 
Nashindwa kuamini km kweli hii barua kaandika Bi Maajar. Kwani kuna watu kazi yao kuchimba wengine kama ambavyo walimchafua sana huyu mama mwaka jana then watu hao wakawa wanatamba Bongo kuwa wamemkomesha maana JK alitaka kumpa post mmoja. Kwa kutumia lobbying power yao kwa Rais wakamchafua huyu mama kikweli kweli mpaka JK kaona noma. Hii ndo kazi ya lobbist.

Whatsoever, yawezekana Dkt Mzengi could have appealed to the Embassy to help paying the penalty since he is an employee, as anyone could do ukiangalia pesa inayodaiwa. Lakini ukisoma hitimisho la barua hii inasema: "nashauri serikali imshinikize Dkt Mzengi kulipa deni lote kwa mkupuo au uangaliwe uwezekano wa kumkopesha ili apate kulipa deni lote" Nadhani kuna suala la ubinadamu na diplomacy pia.
 
Back
Top Bottom