Moderm nzuri kuliko zote ni ipi?tigo,airtel?voda?zantel?ttcl? what is the best?

Mbona mara nyingi mahali ambapo kuna voda na zantel inashika? Mimi nakushauri utumie airtel.

Siyo kila palipo na voda basi na zantel ipo,kuna sehemu yes while other no. try airtel,coverage yake ni kubwa.
 
Uchakachuaji is very dangerous. Ukipaa shida utaogopa kwnda kudai haki yako. Anyway take what you heart tells you.
 
Hakuna mtandao ambao unazidi mitandao yote kwa kila kitu. HAKUNA. Narudia, Hakuna mtandao ambao unazidi mitandao yote kwa kila kitu. HAKUNA. Ubora wa mtandao hutegemea na gharama ya awali ya kununulia, gharama wakati wa matumizi baada ya kununua, signal strength n.k. Mtandao unaweza kuwa na gharama nzuri lakini usimfae mtu heavy user kwa sababu ya weak signal strength. Mtandao unaweza kuwa na signal strength kubwa na gharama nafuu lakini hauna coverage kubwa hivyo si kila mtu wa kila mahali atauhitaji.

Fanya utafiti, fahamu coverage na strength. Nilikuwa na sasatel, wakaniboa gharama (enzi hizo MB 400 or 600?) ilikuwa ni 30,000/=. Nikachukua Zantel (120,000/=) Nikajiunga package ya highlife. Zantel spidi safi, nikaenjoy. Wakaja na sera huwezi kurecharge hadi 7 days za highlife zifike, nikavumilia. Wakaja na sera huwezi kurecharge highlife package hata kama 7 days zimefika hadi uwe umepiga simu for not less than 5,000/= per week. Uvumilivu ukanishinda. Nikanunua Airtel 60,000/=. Nilipokuwa naishi (segerea) spidi ndogo kweli. Nikienda town (posta) spidi ya ndege, safi. Nikirudi nyumbani maumivu. Nikarudi tena sasatel. Kwa sasa wakawa wanauza modem kwa 39,900/=. Wana package ya 1.5 GB kwa 7500/= for one week. Spidi ya kusuasua, wakati mwingine kasi. Nikahama makazi kwenda sehemu nyingine hapa Dar (kinyerezi). Sasatel, spidi ya kobe. Nikajarudia modem yangu ya Airtel niliyoiweka kapuni. Spidi kubwa. Ndo nayotumia sasa. Wana packages kadhaa, nazotumia 3GB/week/15,000/= na 400MB/Month/2500/=. Unarecharge hata kama umemaliza package yako hapo hapo, no "hadi wiki iishe" kind of limitations.

Hivyo fanya research. Majibu mepesi ya Tigo, Voda, Airtel, Zantel, TTCL, Safaricom yatakuchanganya tu. Isitoshe spidi za modems kama 3.1 Mbps, 7 Mbps etc ni uwezo wa modem na si mtandao. Gari lenye kasi haliwezi kwenda maximum speed kama barabara ni mbovu au kuna foleni. Simply like that.

Kama unapenda kudanganywa, sawa.

mkuu nilishaanza kuboreka na mikoment huko juu hadi nilipokutana na post yako. umechambua vyema. wanasema voda ni ghali. naona sivyo. voda unatumia 10000 per week au 30000 kwa mwezi na unatumia utakavyo hadi wiki/mwezi uishe. speed ya kutosha kabisa. labda kwa mafaili makubwa sana pamoja na youtube ndo ziko slow kiasi
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Hey guys wala msipate taabu kuumiza vichwa vyenu buree!
Kutokana na mitandao kuzidiana kulingana na maeneo, huna haja ya kununua moderm toka mitandao tofauti! Wote wanatumia Munufacturer mmoja HUAWEI.
Kuna software ipo ya kuflash Moderm ili iweze kutumia Sim card yoyote ile. Mi natumia moderm moja kwa mitandao yote! If interested naweza kukupa for 100% free. Hawa jamaa wantuibia tu pesa zetu na kufanya hali ya kifedha iwe ngumu.

mkuu hebu tupe mchakato wa kuchakachua modem ili iwe multi. halafu, haiwezi mwisho wa siku kuja kugoma kabisa kupokea sim card yoyote?
 
Nakushauri jaribu hii kitu inayoitwa BANYUKA from TTCL, hakika utainjoy though coverage yake si pana sana. Ukiingia huko hutatoka kamwe kwani gharama in affordable, speed usiseme na ni reliable ile mbaya.

maximum na average speed ya hii huduma ni ngapi? kwangu ni ngeni sana. na kwenye website yao sijaiyona maximum speed.
 
sasatel is the Best nenda kushoto nenda kulia.....na wana extreme ya ulimited day weheeeee!!!! nashusha movi kwenda mbele.....so kazi ni kwako mkuu
 
sasatel is the Best nenda kushoto nenda kulia.....na wana extreme ya ulimited day weheeeee!!!! nashusha movi kwenda mbele.....so kazi ni kwako mkuu
Mkuu hapa wanaongelea modem, hiyo unlimited ya jero kwa siku ya sasatel ni kwa watumiaji wa simu kama modem na si wa modem, wanao tumia modem wana dayspeed ya buku unapata mb 40
 
@sharobalo
sasa leo hii unatwambia unatoa buku kwa siku kwa sasatel. weye ulitwambia unatumia internet ya bure ya line zako za tigo. imekuwaje? na unatumia sasatel modem au vipi? au unatumia simu kuunganisha na computer. na speed yake ni KB/s ngapi?
 
Back
Top Bottom