Mnyika Vs Werema: Nani yuko sahihi kuhusu mgogoro wa Serikali na Walimu?

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Werema alimjibu Mnyika bungeni kuwa bunge halina nafasi katika kushughulikia mgogoro kati ya serikali na walimu kwa kuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kuingilia kazi za muhimili wa serikali.

Werema aliyasema hayo baada ya Mnyika kudai kwenye mchango wake kuwa kwa kuwa mahakama imehukumu kuwa Serikali na walimu warejee katika majadiliano kwa kuwashirikisha wataalamu wa masuala ya kazi, ni muhimu wataalamu hao wateuliwe na bunge au kamati husika ya kudumu ya Bunge.

Mnyika alisema ni lazima chombo cha tatu kiingilie kati kwa kuwa tayari walimu na serikali walishashindwa kukubaliana katika hatua ya usuluhishi na kudai kuwa chombo hicho kwa mujibu wa katiba ya nchi ibara ya 63 ni bunge ambalo ndilo lenye mamlaka ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.

Mnyika alidai kuwa suluhisho la mgogoro huo na Serikali baada ya kupanua wigo wa mapato kufuatia marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha iwasilishe bungeni bajeti ya nyongeza yenye kuweka vipaumbele katika masuala ya msingi ya taifa.

Mnyika alidai kuwa chanzo cha mgogoro huo ni bajeti finyu ya serikali na chombo chenye kupitisha bajeti ni bunge hivyo linapaswa kuingilia kati hoja ambayo ilipingwa na Werema kwa madai kuwa mgogoro huo unaohusu walimu na serikali na kwamba mahakama imeshaamua warejee kwenye majadiliano hivyo bunge kuingilia kati ni kuvunja katiba ya nchi na kuingilia mihimili mingine ya dola.

Kwa upande mwingine, Werema alimkosoa Mnyika kuwa mahakama haikusema kwamba serikali imevunja katiba. Werema aliyasema hayo wakati akijibu madai ya Mnyika aliyoyatoa bungeni kuwa katika kipindi cha mgomo wa walimu wapo viongozi na watendaji wa serikali waliokiuka ibara ya 4 na 107 A za katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliyoapa kuilinda na kuhoji hatua ambazo zimechukuliwa na serikali kufuatia hali hiyo.

Aidha Jaji Werema amekemea tabia ya wanasiasa kuwapotosha wafanyakazi na kuwataka pia wasifanye mikutano nao.
 
Acha ushabiki wa kijinga!
Bunge linaingiaje kwenye huu mzozo? Eleza, usipotoszhe mada.
This is too low!!!!!
Bunge ndiyo nafasi (forum) ya Wananchi kupanga na kupitisha mapato na matumizi ya Serikali yao!
Unakumbuka jinsi Bajeti ya Uchukuzi ilivyokataliwa mwaka jana ikabidi Serikali ijipange upya?
The same could have been done juu ya bajeti ya ELIMU.
Tatizo kubwa ni kwamba Wabunge hawaathiriwi na migomo ya Walimu kwa kuwa watoto wao hawasomi shule zilizo chini ya Serikali wanayoisimamia!
Tatizo hili lingekuwa linawagusa, moto ungewaka Bungeni.
Talk of Wabunge na uzalendo!
 
kuna chombo kilichoundwa kisheria CMA ndicho kinachosuluhisha migogoro ya wafanyakazi, walimu wakiwemo. Chombo hicho kikishindwa, kama ni mgogoro wa maslahi wafanyakazi wanapewa haki ya kugoma kwa kufuata utara tibu uliowekwa kisheria. Kama ni mgogoro wa haki, CMA inatoa uamuzi ambao rufaa yake hupelekwa mahakama kuu divisheni ya kazi. Upand ucporidhika inakwenda mahakama ya rufaa.

Kwa msingi huu Werema yupo sahihi. Bunge ndo lililoutengeza utaratibu huo.
 
This is too low!!!!!
Bunge ndiyo nafasi (forum) ya Wananchi kupanga na kupitisha mapato na matumizi ya Serikali yao!
Unakumbuka jinsi Bajeti ya Uchukuzi ilivyokataliwa mwaka jana ikabidi Serikali ijipange upya?
The same could have been done juu ya bajeti ya ELIMU.
Tatizo kubwa ni kwamba Wabunge hawaathiriwi na migomo ya Walimu kwa kuwa watoto wao hawasomi shule zilizo chini ya Serikali wanayoisimamia!
Tatizo hili lingekuwa linawagusa, moto ungewaka Bungeni.
Talk of Wabunge na uzalendo!

This gave you credibility. I like the way you hit the point. If our government is not part of the problem, automatically it cant be part of the solution!!
 
Tatizo huu muhimili wa mahakama unatumiwa kisiasa. Serikali ikiona kuna jambo imelishindwa inatumia mahakama kujilinda, kukandamiza haki na kukomoa wale inaowaona ni maadui zake.
 
Ninyi mnaoitetea Serikali katika mgogoro wa walimu mmekosa uzalendo kwa watoto wa Watanzania na Taifa kwa ujumla, wanaf. Mashuleni hawafundishwi kama inavyotakiwa na hata wanaofaulu kwenda sekondari hawajui kkk, halafu kuna mijitu inashabikia na kushangilia kama mazuzu hatua zilizochukuliwa na serikali ambayo haijatoa suluhu kwa mgogoro huu ambao utaendelea kuwaumiza watoto wetu. Au kwa kuwa watoto wako shule za English medium na nje ya nchi?
 
Back
Top Bottom