Mnyika, ubunge sio kujitolea pesa

Kwa hio wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wote ni MAFISADI?- kwa kuchangia elimu -na kila kijiji kuwa na secondari yake?

Itakuchukua muda kunielewa,
shule zote za kata zimejengwa kwa nguvu ya wananchi sio klmnjr tu.
Hapa tunazungumzia kutoa sehem ya pato lako kwa maendeleo ya jimbo ukiwa kama kiongozi,na lazima pia ujue kuna kutoa mchango kwa maana ya harambee na kutoa anakotoa myika au dewj nk.
 
mheshimiwa pauluse au nimekosea sawa tu hakuna hoja iliyosimama hapo kwani mnyika kaonyesha yeye sio mchumia tumbo kaamua kugawana na watu wa jimbo lake, Sikukufikilika Naona una private isue kwani pro maghembe na upro wake kawafanyia nini watu wa mwanga huoni ole lekule na elimu yake ya kuendeleza kawasaidia masai wake hivyo unaweza kuwa dr, digrii, upro na ukuawa hovyo ukadanganya na wasanii kama mlivyo fanya kwenye richmond, na digrii yako ya uchumi una laghaiwa na watu wa sanaa pole weeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu kwenye swala la elimu kweli kaongeza pumba, mimi naongelea point nyingine
 
Mkuu kunawakati Dewj alisema hata hajui mshahara wake sh ngapi sababu hagusu hata senti zote zinarudi kwa wananchi wa jimbo lake the same to others
Tatizo lako nini hasa? Na mimi nikiamua kujitolea sehemu ya ka hela kangu utanihesabu vipi?
 
yeah, namfaham vizuri mnyika, aliperform vizuri sanaa form iv, alipata alama "a" kwenye masomo mengi sana, kama sijakosea kati ya masomo kumi ambayo alifanya mitihani yake mwaka ule wa 2008 alipata 'a' masomo tisa (9). Jamaa ana akili za kuzaliwa na akifundishwa anaelewa, nilikuwa nyuma yake mwaka mmoja na tuliwai kuishi mabweni yanayokaribiana kwa mda fulani kabla ya mimi kuhama/kuhamishwa. Sijui matokeo yake ya form vi pale tambaza yalikuwaje, ila amewai kuongoza hata nilipokuwa nae shuleni na aliongoza vizuri na kwenye debate za kiingereza ndo usisema jamaa alikuwa anatutoa nockout sio kwa kuwa alikifahamu vizuri kiingereza, bali alikuwa na point nzuri pia. Anayetaka kudhibitisha acheki matokeo ya form iv ya mwaka 2008 (ule mtihani uliorudiwaga) ya maua seminary ajioneee mwenyewe. Mnyika angeweza na anaweza kusoma na kuhitimu degree yoyote sio kwa kupata 'gentleman degree' bali second upper or first class. Hongera mate mnyika kwa kupata ubunge na nakutakia kila la heri kwenye majukumu yako ya kuendeleza nchi.


2008 au 1998???????2008 muheshimiwa alikuwa chuo kikuu bana tena nafikiri alikuwa kama sio anamaliza alikuwa mwishoni.
 
Tatizo lako nini hasa? Na mimi nikiamua kujitolea sehemu ya ka hela kangu utanihesabu vipi?

Mkuu wewe huna influensi yoyote toa hata wote sawa tu.
Uliwahi kujiuliza ni kwanini takrima na mambo yake mengine ilibidi yatengenezewe sheria kuyadhibiti. it is simple yanaathiri maamuzi.
Hili limekaa kimaadili zaidi na kwa sababu sio kosa huwezi ona ubaya wake
 
Mkuu wewe huna influensi yoyote toa hata wote sawa tu.
Uliwahi kujiuliza ni kwanini takrima na mambo yake mengine ilibidi yatengenezewe sheria kuyadhibiti. it is simple yanaathiri maamuzi.
Hili limekaa kimaadili zaidi na kwa sababu sio kosa huwezi ona ubaya wake
Kwa hiyo tatizo lako la "kimaadili" kwa JJ ni lipi?
 
Unashindwa kutofautisha kwa sababu umechoka kufikiri... Tofauti ya anachofanya Mnyika na Rostam katika kuchangia wananchi ni vyanzo vya pesa. Kwa nia njema, chanzo cha pesa ya Mnyika kiko wazi kabisa...ni sehemu ya mshahara wake. Kila mtu , hata wewe unajua, Mnyika anatoa sehemu ya pato lake halali. Rostam anachangia kutoka kwa pato la kifisadi, pato la wizi.

Una ushahidi wa hao unaosema wanatumia pesa za wizi tuwapeleke mahakamani?
 
Kwa hiyo tatizo lako la "kimaadili" kwa JJ ni lipi?


Kama ni mwerevu mkuu utajua ni kwanini nasema linaathiri maamuzi.
Leo hii tunao watuhumu mafisadi wakubwa ndio wanaongoza kupendwa majimboni kwa staili hii
Sababu inaahiri upeo na maamuzi
 
Kama ni mwerevu mkuu utajua ni kwanini nasema linaathiri maamuzi.
Leo hii tunao watuhumu mafisadi wakubwa ndio wanaongoza kupendwa majimboni kwa staili hii
Sababu inaahiri upeo na maamuzi
Nielimishe, maana mi sioni tatizo. Na specifically JJ na sio wengineo.
Tuache generalization, tuje kwa Mnyika, tatizo nini?

@ JJ,
Pamba yupo pia JF?
 
Nielimishe, maana mi sioni tatizo. Na specifically JJ na sio wengineo.
Tuache generalization, tuje kwa Mnyika, tatizo nini?

@ JJ,
Pamba yupo pia JF?

Mkuu unajua ila unajifanya hujui, kanuni inasema nikuache kama ulivyo.
Kama ungekuwa hujui na ukawa hujui kama hujui basi ningekuelimisha.
Lakini pia kama ungekuwa unajua lakini hujui kuwa unajua, ningekuelimisha pia
 
Mnyika ubunge sio kujitolea pesa, haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutoa pesa. Kinachohitajika ni mbunge mwenye uwezo wa kuikaba serikali itumie kodi ya wananchi kuboresha elimu, maji,nk...tukijenga dhana kwamba uongozi unapimwa kwa mtu kuchangia fedha kusaidia watu tujue tunajenga mazingira mazuri kwa mafisadi kubaki madarakani. Kwani ni utaratibu huu ambao umefanikisha mafisadi wengi kuziteka hata nyumba za ibada kwakuwa wanachangia sana michango ktk nyumba za ibada. Mimi nilidhani pesa hizo mnyika ungezipeleka chuo kikuu ukalipie ada umalizie degree ili jimbo letu la ubungo liondokane na aibu ya kuwa jimbo linalo ongozwa na kihiyo...jamani ni aibu jimbo la mjini kuongozwa na form six tu..


mheshimiwa...mshahara wa wabunge pia ni kodi ya wananchi.....na mnyika amesoma UD kwa taarifa yako.
 
Kwa jinsi ninavyoona behaviours za wanachama wa Chadema, viongozi wakiingia madarakani watakuwa wamewekewa mazingira mazuri ya ku practice u dictator maana wanachama hawataki kusikia ila/ baya lolote likizungumzwa dhidi ya viiongozi wao. kuweni wavumilivu, wasikivu na sometimes mkubali ukweli unaouma!!
Na wewe unaesema mbunge hana nafasi katika kushawishi allocations ya funds maeneo muhimu ni muongo mkubwa!!
 
leo ndio nimeamini kuwa watz ni walalmikaji sana kwa kila kitu si kibaya tu hata kizuri pia, Kila siku mlalalamikia mishahara mikubwa kwa wabunge wetu leo wanaamua kujitolea walau hata wanachokipata wakipeleke moja kwa moja ili kiwafikie jamii husika ,hapo hapo unaona watu wanakuja na kuanza kubeza .akiwa kama kijana najua anamambo mengi sana yakufanya pia lakini ameona wananchi wake ndio priority yake....duh kwa hali hii watanzania bado tunasafari ndefu tena sana,sababu kubwa tuna mioyo ya kinafiki,uchoyo na kuoneana husuda hata kwa mtu anayefanya kizuri hatuwezi ku-appreciate, this is real a big problem for us.
Kuhusu pesa za maendeleo mbunge hawezi kuzisimamia bali anazipitisha tu bungeni, ila kwa matumizi gani na kiasi gani hizo ni kazi ya DC na RC ambao ndio serikali, ndio maana tunaona kila siku kuna kuwa na kutoelewana wakati wa kupitisha hizo bajeti maana wanaozipitisha hawazisimamii ingawa wanahaki ya kuhoji kama zimetumika isivyopangiliwa, je ni miradi mingapi iliyopangwa na nhuwa haikamiliki wakati muafaka na wakati bajeti yake huwa imeshatengwa? mlisha uliza hata siku moja kwa hao ma Dc? haya ndio matatizo ya MIafrika kila kitu ni kulalamika tu..sasa manataka viongozi wenu wawafanyie nini? wawaache tu muendelea na shida zenu..Ndio maana watu wananiambia ukija Tz utapata pressure tu maana hawa watu hawaelezeki wala hawasaidiki, kun uwezekano hata hao CHICHIEMU walishawasoma na kuwaelewa kuwa hawa ni MAVUVUZELA ndio maana wanafanya mambo kama ya watoto wachanga kumbe wanajua wahusika hawana lolote maana kunawengi sana watu kama wewe..?.aghhhhhhhhhh
 
Binafsi siamini kama kuna ukweli wowote kwa mdau aliyea andika kuwa jimbo la Ubungo linaongozwa na Form 6 leaver! Labda kwa kumtaarifu tu huyu jamaa ni kwamba Mnyika ni miongoni wa vijana wachache wenye IQ kubwa hapa Tanzania. Nimewahi kuongea na mwalimu wake aliyemfundisha Maua seminary akanieleza kuwa wakati John Mnyika akiwa shuleni walimu walikuwa wanamuita dalali wa Marks, Hajawahi kupata chini ya B wakati akiwa Form 1 mpaka Form 6. Sasa huo ukilaza unaongelewa hapa ni upi?!

Kilichomfanya akubalike sana mwaka 2005 ni kukubalika kwake na wanachuo wengi wa pale mlimani na jimbo zima la ubungo kwa kuonyesha uweazo wa kudeal na mambo mbalimbali ya kijamii na hata kisiasa. Kuanzia kwenye ufuatiliaji na usuluhishi wa migogoro ya ardhi, kwenye michezo kumbuka Mnyika Cup na mambo mengine kadha wa kadha kwa kutaja hayo machache. Sasa tunaposikia Mnyika ni Form 6 leaver hizi hoja zinatoka wapi?

Naomba ukajipange upya.

Naomba kuwasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom