Mnyika, ubunge sio kujitolea pesa

Kweli kazi bado ipo tuwaelimishe wengi, mnyika kaonyesha njia waeleze wapiga makofi wa ccm nao wajaribu mnyika alichofanya
 
Sikuikifika,

Asante kwa maoni yako. Naelewa wajibu wa mbunge na nililieleza hili bayana mwanzoni mwa mwaka huu wakati natangaza dhamira ya kugombea:

Nanukuu: Naamini kwamba mbunge (ambaye pia kwa nafasi yake ni diwani katika halmashauri) ana wajibu katika maeneo makuu manne (kwa kadiri ya umuhimu).

Mosi; kusikiliza na kuwakilisha wananchi, Pili; kuisimamia na kuiwajibisha serikali na viongozi wake, Tatu; kushiriki katika kutunga sheria, Nne; kuhamasisha upatikanaji wa huduma.

Hata hivyo, sehemu kubwa ya wabunge wetu hawaweki kipaumbele katika majukumu ya kwanza matatu ambayo ndio msingi wa ubunge wenyewe. Matokeo yake ni matakwa ya wananchi kutokuwakilishwa kikamilifu, ufisadi, rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na mikataba mibovu; uwepo wa sheria dhaifu na kutetereka kwa utawala wa sheria na mifumo ya haki masuala ambayo yanakwaza jitihada za maendeleo za wananchi binafsi za taifa kwa ujumla.

Wabunge wengi wanawaza kwamba jukumu kubwa la mbunge ni kutoa bidhaa na huduma kwa wananchi; wakiacha taifa katika lindi la umasikini na kufanya sehemu ya wananchi kujenga mazoea ya kutegemea hisani toka kwa viongozi wa umma na wafadhili wao.

Mwaka 2005 pamoja na majukumu hayo makuu matatu, nilizungumzia suala la mfuko wa maendeleo ya jimbo. Lakini si katika mwelekeo wa mfuko wa sasa uliopitishwa kuwa sheria unaosubiriwa kutungiwa kanuni. Kwa hiyo, wakati nikiunga mkono jukumu la mbunge kuhamasisha maendeleo na kushiriki kwenye shughuli za kijamii, siamini katika mazoea na mfumo wowote unaomfanya mbunge kuwa “mtoa bidhaa na huduma” (mithili ya ATM) kwani unarutubisha ufisadi wa kisiasa na kuhatarisha mwelekeo mzima wa utawala bora. Kama ambavyo siamini pia katika siasa chafu za rushwa, uongo na aina nyingine ya upofu wa kimaadili katika kampeni na uongozi kwa ujumla." Unaweza kujikumbusha kauli yangu kwa ukamilifu wake hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-rasmi-dhamira-ya-kugombea-ubunge-2010-a.html

Naelewa kwamba maoni yako yametokana na Hotuba yangu ya tarehe 12 mwezi 12 Kwenye kongamano la maendeleo jimbo la Ubungo ambapo nilitangaza kwamba nimeshaanza kutekeleza ahadi yangu ya kwenye kampeni ya kutenga 20% ya mshahara wangu kwa mwezi kuingiza kwenye mfuko wa Elimu Ubungo ili kuhamasisha wadau wengine nao kuuchangia. Kwenye kongamano hilo wakati najibu mada zilizotolewa na vijana wasomi hususani wazo la kuwa na kituo cha elimu kwa umma nilisema kwamba mpaka kwa pamoja mimi na wao tutakapofanikisha kuanzisha kituo husika binafsi nitaoongoza harakati hizo kwa kutoa 20 % ya posho kwa kipindi chote cha uhamasishaji mpaka kazi itakapokamilika. Nilifanya hivyo nikijua bayana majukumu ya mbunge- lakini nilifanya hivyo kama sehemu ya kuonyesha kwa vitendo kwamba ukijumuisha mishahara na posho kwa mwezi wabunge wanalipwa zaidi ukilinganisha na watumishi wengine wa umma kama walimu, maaskari nk; hivyo nimeamua kurudisha sehemu ya kodi hizo za wananchi kwa wananchi wenyewe kupitia jitihada za pamoja za kuleta maendeleo. Nakukaribisha na wewe utuunge mkono katika harakati zetu ubungo; tutaibana serikali, lakini na sisi wenyewe tunajibana.

JJ
 
Yeah, namfaham vizuri Mnyika, aliperform vizuri sanaa form IV, alipata alama "A" kwenye masomo mengi sana, kama sijakosea kati ya masomo kumi ambayo alifanya mitihani yake mwaka ule wa 2008 alipata 'A' masomo tisa (9). jamaa ana akili za kuzaliwa na akifundishwa anaelewa, nilikuwa nyuma yake mwaka mmoja na tuliwai kuishi mabweni yanayokaribiana kwa mda fulani kabla ya mimi kuhama/kuhamishwa. sijui matokeo yake ya Form VI pale Tambaza yalikuwaje, ila amewai kuongoza hata nilipokuwa nae shuleni na aliongoza vizuri na kwenye debate za Kiingereza ndo usisema jamaa alikuwa anatutoa nockout sio kwa kuwa alikifahamu vizuri Kiingereza, bali alikuwa na point nzuri pia. Anayetaka kudhibitisha acheki matokeo ya form IV ya mwaka 2008 (ule mtihani uliorudiwaga) ya MAUA SEMINARY ajioneee mwenyewe. Mnyika angeweza na anaweza kusoma na kuhitimu Degree yoyote sio kwa kupata 'Gentleman degree' bali second upper or first class. Hongera mate Mnyika kwa kupata Ubunge na nakutakia kila la heri kwenye majukumu yako ya kuendeleza nchi.
 
Thanks JJ, maelezo yako yanajitosheleza.Tunahitaji wabunge wenye mitazamo ya namna hiyo.
 
lakini ubunge ni kuhonga wananchi kanga, kanga,t-shirt na kofia,skafu na chumvi kabla ya kupiga kura! Maendeleo mgando!!
halafu baadaye unawamwaga hukumbuki hata kuwawekea vilaka vya nguo ulizowapa mpaka baada ya miaka 5 mingine NYAMBAFUUUU
 
Mimi nazani SIKULKIFIKA unempongeza kwanza Mbunge alafu umshauri asisahau pia kuhamasisha wananchi wenyewe kushiriki maendeleo na si kumponda maana huu ni moja wapo wa wajibu wa Mbunge. Kama anaweza kuchangia anachangia kuonyesha mfano na pia kuhamasisha wengine na si kumkejeli....Alafu hilo la elimu yake hapo umechemsha...Hivi elimu ya mbunge wa Rorya ndugu Lakairo na Kapten Komba unazijua wewe? Usiropoke tu
 
Duuh, sheria mpya ya rushwa za wabunge haikuliona hili, kuwa mbunge anaweza kufanya mbinu kama Mnyika. Kakopa wakati wa uchaguzi sasa anazilipa ki-stle ya pekee.
Takukuru hebu liangalieni hili, hali fall katika rushwa hili?
 
One of stupidiest post I have ever seen! Yaani sijui utamwambia nini Muumba wako kwa kushindwa kuutumia ubongo wako japo kwa mambo madogo kama haya.
 
mnyika ubunge sio kujitolea pesa, haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutoa pesa. Kinachohitajika ni mbunge mwenye uwezo wa kuikaba serikali itumie kodi ya wananchi kuboresha elimu, maji,nk...tukijenga dhana kwamba uongozi unapimwa kwa mtu kuchangia fedha kusaidia watu tujue tunajenga mazingira mazuri kwa mafisadi kubaki madarakani. Kwani ni utaratibu huu ambao umefanikisha mafisadi wengi kuziteka hata nyumba za ibada kwakuwa wanachangia sana michango ktk nyumba za ibada. Mimi nilidhani pesa hizo mnyika ungezipeleka chuo kikuu ukalipie ada umalizie degree ili jimbo letu la ubungo liondokane na aibu ya kuwa jimbo linalo ongozwa na kihiyo...jamani ni aibu jimbo la mjini kuongozwa na form six tu..

kweli jj huwezi kutatua kila kitu kwa fedha ni lazima uisimamie serikali itumie kodi zetu kwa mafanikio na maendeleo ya tz nzima
 
Mnyika ubunge sio kujitolea pesa, haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutoa pesa. Kinachohitajika ni mbunge mwenye uwezo wa kuikaba serikali itumie kodi ya wananchi kuboresha elimu, maji,nk...tukijenga dhana kwamba uongozi unapimwa kwa mtu kuchangia fedha kusaidia watu tujue tunajenga mazingira mazuri kwa mafisadi kubaki madarakani. Kwani ni utaratibu huu ambao umefanikisha mafisadi wengi kuziteka hata nyumba za ibada kwakuwa wanachangia sana michango ktk nyumba za ibada. Mimi nilidhani pesa hizo mnyika ungezipeleka chuo kikuu ukalipie ada umalizie degree ili jimbo letu la ubungo liondokane na aibu ya kuwa jimbo linalo ongozwa na kihiyo...jamani ni aibu jimbo la mjini kuongozwa na form six tu..

Unasumbuliwa na chuki binafsi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Achana nazo hazitakusaidia utakufa na BP
 
Duuh, sheria mpya ya rushwa za wabunge haikuliona hili, kuwa mbunge anaweza kufanya mbinu kama Mnyika. Kakopa wakati wa uchaguzi sasa anazilipa ki-stle ya pekee.
Takukuru hebu liangalieni hili, hali fall katika rushwa hili?

Kuna wazazi walitakiwa waahairishe uzao wao kuepusha aibu kwa familia
 
Duuh, sheria mpya ya rushwa za wabunge haikuliona hili, kuwa mbunge anaweza kufanya mbinu kama Mnyika. Kakopa wakati wa uchaguzi sasa anazilipa ki-stle ya pekee.
Takukuru hebu liangalieni hili, hali fall katika rushwa hili?

Huyu uti wa mgongo ungalimtosha, akupaswa kupewa ubongo, maana anatumia tumbo kufikiri badala ya ubongo.
 
Muheshimiwa JJ with all due respect.
Mkuu nakuheshimu sana na nisingependa ionekane kama napingana na wewe, lakini kimtazamo mimi sidhani kama ni sahihi kufanya ulichofanya ingawa si kosa pia.
Napata tabu kutofautisha ulichofanya na anachofanya Rostam Igunga, Dewj Singida, Lowasa Monduli nk, nk.
Mimi sidhani kama wananchi wa ubungo wanahitaji pesa yako kuboresha huduma kwa maana ya kupata mshahara mkubwa na kurudisha kodi kwa wananchi.
Ukirejea sera yenu ya elimu, afya bure nadhani si mfano bora sana kuwataka wananchi wako kuchangia gharama zinazopaswa kulipwa na serikali unayo isimamia wewe, wajibu wako wewe ni kuhakikisha wananchi wako wanapata hizo huduma kwa wewe kuibana serikali ipeleke hizo hela na si wewe kutoa pesa zako na kuhamasisha nao watoe kugharamia maendeleo yao.
Kama nilivyosema sio kosa na kijujuu utaona ni sawa lakini kimantiki haileti maana.
wewe kama kiongozi wao unapaswa kuwa mfano wa kuibana serikali na si kuwahamasisha wananchi wazidi kuchangia.
Leo hii Dewj na wenzie nilio wataja wanaonekana lulu majimboni mwao(angalia ushindi wao) sababu tu wanatumia pesa toka mifuko yao na hakuna chochote cha maana walichofanya.
Isome tena kwa umakini hoja yake tafakari, achana na mambo ya elimu aliyoyasema.
Mkuu kuna mambo mengi unaweza fanya kama mbunge, binafsi nakuaminia sana lakini pia soma alama za nyakati.
Best wishes ktk kutumika kwa wanajimbo lako
 
Muheshimiwa JJ with all due respect.
Napata tabu kutofautisha ulichofanya na anachofanya Rostam Igunga, Dewj Singida, Lowasa Monduli nk, nk.

Unashindwa kutofautisha kwa sababu umechoka kufikiri... Tofauti ya anachofanya Mnyika na Rostam katika kuchangia wananchi ni vyanzo vya pesa. Kwa nia njema, chanzo cha pesa ya Mnyika kiko wazi kabisa...ni sehemu ya mshahara wake. Kila mtu , hata wewe unajua, Mnyika anatoa sehemu ya pato lake halali. Rostam anachangia kutoka kwa pato la kifisadi, pato la wizi.
 
Kwa hio wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wote ni MAFISADI?- kwa kuchangia elimu -na kila kijiji kuwa na secondari yake?
 
Unashindwa kutofautisha kwa sababu umechoka kufikiri... Tofauti ya anachofanya Mnyika na Rostam katika kuchangia wananchi ni vyanzo vya pesa. Kwa nia njema, chanzo cha pesa ya Mnyika kiko wazi kabisa...ni sehemu ya mshahara wake. Kila mtu , hata wewe unajua, Mnyika anatoa sehemu ya pato lake halali. Rostam anachangia kutoka kwa pato la kifisadi, pato la wizi.

Mkuu kunawakati Dewj alisema hata hajui mshahara wake sh ngapi sababu hagusu hata senti zote zinarudi kwa wananchi wa jimbo lake the same to others
 
mheshimiwa pauluse au nimekosea sawa tu hakuna hoja iliyosimama hapo kwani mnyika kaonyesha yeye sio mchumia tumbo kaamua kugawana na watu wa jimbo lake, Sikukufikilika Naona una private isue kwani pro maghembe na upro wake kawafanyia nini watu wa mwanga huoni ole lekule na elimu yake ya kuendeleza kawasaidia masai wake hivyo unaweza kuwa dr, digrii, upro na ukuawa hovyo ukadanganya na wasanii kama mlivyo fanya kwenye richmond, na digrii yako ya uchumi una laghaiwa na watu wa sanaa pole weeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom