MNYIKA tunaomba utoe fafanuzi kwa niaba ya CHADEMA juu ya hili

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
5,040
Siku chache zilizopita kumekuwa na tetesi ktk mitandao mabalimbali hapa nchini na mtaani ya kwamba kulikuwa na kikao cha siri kilichofanyika kati ya Mwenyekiti wa CDM taifa(Freeman Mbowe) pamoja na mwenyekiti wa CCM taifa( Rais JK).

Sasa naomba JJ Mnyika utoe maelezo ya kina kwa sisi wanachama wenu tujue the major theme ya kikao hicho na kwann kimekuwa cha siri? Pia ama uje ukanushe tetesi hizo.

Maelezo juu ya hili swala yatasaidia kuondoa hofu ambayo ipo mioyoni mwa wanamabadiliko wote hapa nchini ambao wamekuwa wakitatizwa tetesi za kikao hicho cha siri.

Wako ktk mabadilko
Shardcole@Tabora1
 
Ondoeni dhana ya kwamba tofauti ya itikadi za kisiasa ni uadui. Maana yake ukiwa CHADEMA huwezi kusimama wala kuongea na mwana CCM. Hizi fikra ni potofu sana.

Sasa ikiwa Mbowe na Kikwete walikuwa marafiki toka kabla hawajapata madaraka walio nayo sasa, je watengane simply kwa kuwa wanatofautiana kiitikadi tu za kisiasa. Mbowe kuwa na kikao na Rais Jakaya Kikwete inaweza kuwa katika sura mbili; moja huyu ni Rais wa nchi anaweza kuwa na kikao na mtanzania yeyote anayotaka kuzungumza na huyo mtu ni siri yake na Mbowe akiona ni ya wazi atawaeleza wafuasi wake.

Pili Mbowe ni Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni, Kikwete ni Mwenyekiti wa Chama Tawala, kuna shida gani wakiitana na kuzungumza. Kwani Mbowe ni mtoto mdogo? Tutalinda mpaka lini kiongozi wa CHADEMA asiongee na kiongozi wa CCM. I dont think Mbowe is that cheap.
 
Siku chache zilizopita kumekuwa na tetesi ktk mitandao mabalimbali hapa nchini na mtaani ya kwamba kulikuwa na kikao cha siri kilichofanyika kati ya Mwenyekiti wa CDM taifa(Freeman Mbowe) pamoja na mwenyekiti wa CCM taifa( Rais JK). Sasa naomba Jj mnyika utoe maelezo ya kina kwa sisi wanachama wenu tujue the major theme ya kikao hicho na kwann kimekuwa cha siri? Pia ama uje ukanushe tetesi hizo.
Maelezo juu ya hili swala yatasaidia kuondoa hofu ambayo ipo mioyoni mwa wanamabadiliko wote hapa nchini ambao wamekuwa wakitatizwa tetesi za kikao hicho cha siri.

Wako ktk mabadilko
Shardcole@Tabora1

Nafikiri hapa ungeuliza je ameenda kumwona kama mwenyekiti wa chama ama kama mtu binafsi kwa maana mwananchi wa kawaida kwa mambo yake binafsi.....
 
Wanakumbushana lile DISCO la RSVP kabla halijaitwa Mbowe Hotel Dj Kalikali
 
Sijui kama CDM huwa wanatoa taarifa juu ya mikutano ya faragha. Kuna mkutano walishafanya na mkuu wa nchi Dr. Slaa akasema wangetoa taarifa lakini hadi hii leo hakuna taarifa yoyote. Utamuonea tu Mnyika wa watu. Mwache Mnyika atupiganie wana Ubungo tupate maji na barabara badala ya kujikita kujibu masuala ya watu binafsi.
 
Chadema mtaambiwa baadae kama mlivyoambiwa wakati Chadema walivyokwenda Ikulu...hakuna ubaya wowote JK kukutana na Mbowe siasa sio uadui.
 
Jamani wakuu niseme kwamba sina maana mbaya lakini ktk harakati hizi inatubidi na ss wananchi tuwe makini na tusiache asilimia zote tufanyiwe na viongozi wetu pia inatupasa kuwa tunahoji mambo ambayo yanatutatza na hiyo ndio demokrasia, tusiamini sana viongozi wetu na kuwapa credibility ya kuwa wakamilifu kama malaika.
 
Sijui kama CDM huwa wanatoa taarifa juu ya mikutano ya faragha. Kuna mkutano walishafanya na mkuu wa nchi Dr. Slaa akasema wangetoa taarifa lakini hadi hii leo hakuna taarifa yoyote. Utamuonea tu Mnyika wa watu. Mwache Mnyika atupiganie wana Ubungo tupate maji na barabara badala ya kujikita kujibu masuala ya watu binafsi.

mkuu mnyika ndio anahusika na maswala ya habari kama haya, alafu ni wajibu wetu wanachama kupata updates zihusizo chama na viongozi wetu, pia ni lazima tuhoji kama jinsi tulivyohoji miendendo na mahusiano ya Zitto na Jk.
 
kuna vitu vya kuhoji,lakini si vyote.kwakua kuna vitu vinakua siri kwa kua tupo kwenye uwanja wa mapambano,kuna vitu inapaswa vijulikane kwa viongoz tu tena ngazi ya juu,na ndio maana tunakua chama makini
 
wananchi tuwe makini na tusiache asilimia zote tufanyiwe na viongozi wetu pia inatupasa kuwa tunahoji hiyo ndio demokrasia, tusiamini sana viongozi wetu.
Shardcole tulia,chademda ni chama makini kuliko hata wananchi,umakini wao ndio umekufikisha hapo had ukawakubal,lazm uwaamini viongz kwan angalia walipotutoa na wanapotuelekeza twende,kumbuka mwananch wa leo si wa enz zile.nafaham kuna meng viongoz wetu hawa wanakutana nayo na kuyatatua.na ndio maana tuko tusonga mbele
 
Last edited by a moderator:

Mkuu [MENTION]Ruhazwe [/MENTION]naomba maelezo ya ziada hapo kwenye red.
 
Kama twamwamini mwkiti wa chama hatuna sababu ya kumtaka atueleze kila anachozungumza na kila mtu, busara ni kuwa na subira, hekima ni kusubiri ufahamishwe unachostahili.

Pia chama lazima kiwe na mazungumzo na wengine yamkini mwkt wa CCM alipenda kuomba ushauri kutoka kwa mwkt wa cdm,so laweza lisiwe la public au utendaji wake ndo ukawa publicly.

Usiwe na hofu kama wewe ni mjenzi makini wa taifa.karibu!
 
Sijui kama CDM huwa wanatoa taarifa juu ya mikutano ya faragha. Kuna mkutano walishafanya na mkuu wa nchi Dr. Slaa akasema wangetoa taarifa lakini hadi hii leo hakuna taarifa yoyote. Utamuonea tu Mnyika wa watu. Mwache Mnyika atupiganie wana Ubungo tupate maji na barabara badala ya kujikita kujibu masuala ya watu binafsi.
kama mkutano wa faragha yanini kuutolea maelezo.
 
hii hoja si ya busara sana kwani si kila kitu baba wa nyumba anaweza kuwaeleza watoto wa familia yake hata kama ni la maslahi yao..tatizo la kuropoka ropoka kila kitu ni la makamba na vuvuzela wake yule dogo wa uenezi
 
Back
Top Bottom