Mnyika live ITV: Afafanua vipaumbele vya Chadema

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Naibu katibu mkuu wa Chadema anaendelea kuhojiwa sasa hivi ktk televisheni ya ITV. Kwa jinsi anavyofafanua ilani ya Chadema na changamoto zinazoikabili taifa letu, na namna gani wao wakipewa nafasi ya kuongoza nchi hii watakavyotekeleza ilani yao....inapendeza sana! Naamini hata Kinana na mgombea wake wa Urais hawawezi kuelezea changamoto za kitaifa na namna ya kuzitatua kisayansi. Kama mpiga kura ktk jimbo la ubungo, ni wazi kura yangu itaenda kwa Mnyika!
 
Kwa kweli nimemkubali Mnyika kwa umakini mkubwa na uelewa mkubwa kwa jinsi alivyojieleza na kuieleza Ilani ya CHADEMA, Sijawahi kuvutiwa na mwanasiasa yeyote ngazi ya ubunge katika kampeni hizi kama Myika kwa jinsi nilivyomwelewa na anavyojiamini! kuanzia sera ya mambo ya ndani ya nchi, ulinzi na usalama wa Taifa na mahusiano ya kimataifa.
Wana Ubungo hoyeeeee! pia watanzania hoyeee!
 
HIVI KWANINI KWENYE VIPINDI VIZURI KAMA HIVI HUWA HUTOAGI TAARIFA HAPA JAMVINI??

UJUE BAADA YA ILE TAARIFA YA HABARI ITV KUTOKANA NA INFLUENCE YA WATOTO IKABIDI TUBADILISHE STATION NA KUANZA KUANGALIA FUTUHI-STAR TV, AAGH KURUDI HUKU NAKUTA MNYIKA ZIMESALIA DAKIKA 10 TU AMALIZE KIPINDI....AAGH NNNILIPATA TAABU SANA KUWAAMBIA WATOTO WAKALALE, ILA WALIKUSIKILIZA NA HAPA LENGO LANGU KUBWA NI KUWAASA HAWA WATOTO KATIKA MAKUZI YAO WAICHUKIE CCM NA KUJIRIDHISHA NA CHADEMA...

...ILA ANGALIZO TU SIKU ZIJAZO KAMA KUNA KIPINDI CHADEMA KWENYE TV NI BORA MKATOA ''ALERT'' MAPEMA ILI TUFAHAMU,..MBONA ZITTO KABWE ANAFANYAGA MARA NYINGI TU HAPA JF.......

:director:
 
hivi kwanini kwenye vipindi vizuri kama hivi huwa hutoagi taarifa hapa jamvini??ujue baada ya ile taarifa ya habari itv kutokana na influence ya watoto ikabidi tubadilishe station na kuanza kuangalia futuhi-star tv, aagh kurudi huku nakuta mnyika zimesalia dakika 10 tu amalize kipindi....aagh nnnilipata taabu sana kuwaambia watoto wakalale, ila walikusikiliza na hapa lengo langu kubwa ni kuwaasa hawa watoto katika makuzi yao waichukie ccm na kujiridhisha na chadema......ila angalizo tu siku zijazo kama kuna kipindi chadema kwenye tv ni bora mkatoa ''alert'' mapema ili tufahamu,..mbona zitto kabwe anafanyaga mara nyingi tu hapa jf
 
Mnyika anafaa kuwa katibu mkuu baada ya Dr Slaa kuwa Rais. Kijana anaweza kujenga na kutetea hoja zake. Nimemkubali jinsi alivyokuwa akinadi ilani ya uchaguzi ya Chadema ITV usiku huu
 
mkuu kumbuka kuwa hii ilikuwa recorded kwahiyo ITV wanaweza wanaweza kurusha muda wowote
inawezekana mnyika alikuwa haujui watarusha lini
 
Hon. Mnyika, at this moment you must strive to seize any opportunity which could give your campaign an edge. Zitto did it and he received the feedback and suggestions as regarding to the same. Candidates who are struggling to overcome the CCM hurdles must capitalize the air time provided.
 
NI HABARI NJEMA KAMA HATACHAKACHULIWA NA CCM.................SI UNAJUA CCM wana pesa za EPA kwa hiyo full kununua watu.......wamewanunua waandishi wa habari makini......wamenunua vyombo vya habari makini.........wanajitahidi sana kutumia vizuri umasikini wa watz............lkn naamini kizazi hiki hakitakubali kuendelea kuchakachuliwa!
 
Ni kweli kijana ameiva,anafaa kupewa kura!Hongera Mnyika,Hongera Chadema!
 
Mnyika anafaa kuwa katibu mkuu baada ya Dr Slaa kuwa Rais. Kijana anaweza kujenga na kutetea hoja zake. Nimemkubali jinsi alivyokuwa akinadi ilani ya uchaguzi ya Chadema ITV usiku huu

Mkuu Mchukia Ufisadi nawezaje kukutumuia Audi ya Mahojiano ya mnyika ili wana jamvi wapate kusikia
 
Kitu kizuri zaidi CHADEMA wanaweka mtu katika nafasi kutokana na Uwezo. Hivi tukimlinganisha Mnyika na Makamba (interms of knowledge and capacity to analyse Tz problems) nani zaidi?
 
Kitu kizuri zaidi CHADEMA wanaweka mtu katika nafasi kutokana na Uwezo. Hivi tukimlinganisha Mnyika na Makamba (interms of knowledge and capacity to analyse Tz problems) nani zaidi?

Unataka kulinganisha visivyolinganishika! Mnyika na Makamba, hutakuwa umemtendea haki Mnyika. Mnyika na Makamba = mbingu na ardhi. Makamba mlinganishe na Mr. Bean
 
Kitu kizuri zaidi CHADEMA wanaweka mtu katika nafasi kutokana na Uwezo. Hivi tukimlinganisha Mnyika na Makamba (interms of knowledge and capacity to analyse Tz problems) nani zaidi?

Makamba ana umri mkubwa kuliko Mnyika..
 
Chuwa alibaki akimshangaa tu..kabla alionyesha kama mtu anayetaka kumshambulia Mnyika..
Hata CCM walioangalia kipindi hicho..walitingisha vichwa kazi Ubungo wanayo..
 
Kwakweli Kijana Mnyika yuko vizuri sana kichwani, huyu ni hazina kubwa mno kwa Taifa, nimetazama mahojiano haya jana, kila alipo kuwa akiulizwa swali na mtangazaji Chuwa ambaye mwanzoni alikuwa a bit rude, alilijibu vizuri mno na kumalizia vyema kwa kuomba wananchi tuwape ridhaa watekeleze hayo yaliyomo kwenye ilani yao.

Ni ukweli usiopingika kwamba kutokana na mjaibu mazuri yasiyo teteleka hata mtangazaji Chuwa alijikuta akibadilika nakuanza kuuliza maswali yake kistaarabu tofauti na alivo anza,
Namalizia kwa kusema, Mnyika umenikuna, kura yangu ni kwa chamadema, na naamini kila mtanzania aliye angalia jana kipindi hicho kura yake atawapatieni ili mtekeleze hayo mliyo yaahidi.

Go go go Chadema and God bless you
 
Dogo anatisha. Ni heri mtumwa kijana mwenye busara kuliko mfalme mzee asiye na busara.
 
Nami namkubali kijana Mnyika, yuko makini saana utadhani ametunga yeye maana alijibu kwa ufasaha sana, jamani Chadema wamejipanga vizuri kushika dola, Du amanifurahisha saaaaaaana kujana Mnyika asiyesikiliza jana amekosa uhondo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom