Mnyika kuwasilisha hoja binafsi bungeni

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
811
mnyika%20katiba.jpg
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika amesema kuwa atawasilisha bungeni hoja binafsi ya kutaka mabadiliko ya katiba na kupinga moja ya mapendekezo ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda la kuunda tume ya kuangalia mchakato huo.

Tangu kumalizika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, Chadema imewasha moto wa mabadiliko ya katiba na kufufua mjadala wa kutaka kuandikwa kwa katiba mpya kiasi cha Waziri Pinda kuamua kutoa tamko mwishoni mwa wiki kuwa atamshauri Rais Jakaya Kikwete aunde tume kuchunguza madai hayo.

Miongoni mwa viongozi waliojiunga kwenye mjadala huo wa kutaka katiba mpya ni mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Sinde Warioba na Frederick Sumaye, Jaji Mkuu Agustino Ramadhan na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa ambaye alitahadharisha kuwa bila ya katiba mpya nchi inaweza kuingia kwenye vurugu.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mnyika ambaye ni mmoja wa wabunge vijana kwenye Bunge la Kumi, alisema atatimiza ahadi yake katika kipindi cha wiki moja kwa kuwasilisha taarifa kuhusu hoja binafsi ya katiba mpya kwa katibu wa bunge.
"Ibara ya 8 kifungu kwanza cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mapungufu yake inaeleza wazi umuhimu wa wananchi kushirikishwa katika uundwaji wa katiba. Pia Ibara ya 63-(2) nayo inaeleza wazi," alisema Mnyika.
Aliongeza kuwa kama mbunge ana haki ya kuwasilisha hoja binafsi kuhusu katiba mpya na kwamba ni vyema suala la uundwaji wa katiba likarejeshwa mikononi mwa Bunge kwa kuwa ni mhimili wa dola unaofanya kazi kwa niaba ya wananchi.

"Ibara ya 98 ya katiba ndio sehemu pekee inayozungumzia marekebisho ya katiba hivyo ni wakati muafaka suala hili la katiba likapelekwa bungeni ili wananchi wawakilishwe," alifafanua Mnyika.
Mwanasiasa huyo kinda, ambaye pia ni mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chadema, alieleza sababu za kutaka kupeleka hoja hiyo bungeni ni kutaka chombo hicho lipitishe mchakato wa kuundwa kwa katiba mpya.

"Unajua katiba ni sheria na kwa kuwa bungeni ndiko kunakotungwa sheria basi wanaopaswa kutoa mwelekeo wa katiba mpya ni Bunge," aliongeza.
"Pia katiba ni mkataba kati ya wananchi na watawala... ikumbukwe kuwa anayeandika mkataba ni mwenye mali, na hapa mwenye mali ni mwananchi na Bunge lipo kwa ajili ya wananchi. Kutokana na hilo, ipo kila sababu ya suala hili kurudi bungeni."

Lakini Mnyika alipingana na moja ya mapendekezo ya Waziri Pinda ya kuunda tume ya kuangalia mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya.
"Sikubaliani na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu katiba,” Mnyika aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana.
“(Waziri Mkuu) Amesema atamshauri rais kuunda timu itakayoangalia mapendekezo ya tume zilizoundwa na pia kuanzisha utaratibu wa marekebisho ya katiba. Naona kauli yake haijalenga kuwepo kwa katiba mpya, bali inalenga zaidi marekebisho ya katiba."

Mnyika alifafanua kwamba, hoja hiyo ya Pinda ina mwelekeo wa kuchukua suala la katiba mpya mikononi mwa wananchi na kulipeleka kwa kundi fulani.
Waziri Pinda aliwaeleza wahariri wa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki kuwa kuna njia mbili za kushughulikia kilio cha wananchi cha katiba mpya, akiitaja ya kwanza kuwa ni kumshauri rais aunde kamati ya watu ambao wataangalie maeneo gani ya kuingiza katika katiba.

Alisema njia ya pili ni rais kuunda timu yake ya kiserikali itakayoangalia mapendekezo ya tume zilizoundwa awali kuangalia marekebisho ya katiba na kuchukua mapendekezo yaliyojirudia yatakayoonekana kufaa kuingia katika katiba.

Lakini Mnyika alipingana na mapendekezo hayo akisema haoni sababu ya kuundwa kwa tume nyingine kwa kuwa tangu nchi ipate uhuru, zimeshaundwa tume nyingi kushughulikia suala la katiba.
Alitoa mfano wa Tume ya Jaji Nyalali ambayo ilipendekezwa kufutwa kwa sheria kadhaa ambazo zinaonekana kukandamiza haki za binadamu na Tume ya Jaji Kisanga, akisema matokeo ya uchunguzi wa vyombo hivyo viwili hayajafanyiwa kazi.

"Kutokana na hoja hii napendekeza kwamba, Bunge liweke mfumo wa tume ya kikatiba pamoja na kupitisha azimio ili nchi ifanye mkutano mkuu wa kikatiba kujadili suala hili na kisha zipigwe kura za maoni," alisema.
Alisisitiza kuwa katika suala la katiba mpya, ni lazima wananchi washirikishwe kwa kuwa sasa Watanzaania wanataka katiba mpya.

"Kwanza, katiba inayotumika hii leo ni ya mwaka 1977, tangu kipindi hicho kuna mabadiliko mengi yameshatokea kama ya kiuchumi, kiteknolojia; pili uundwaji wa katiba hiyo haukuwashirikisha wananchi; tatu katiba hii inakabiliwa na changamoto nyingi, mfano suala la Muungano na Tume ya Uchaguzi," alisema.

Chadema ilionyesha kwa vitendo dhamira yake ya kudai katiba mpya wakati wabunge wake walipoondoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kutoa hotuba ya ufunguzi. Viongozi wa chama hicho pia walisusia hafla ya kutangazwa kwa matokeo na sherehe za kuapishwa kwa rais na wiki mbili zilizopita hawakuonekana kwenye sherehe za uhuru.

Source: Radio one news alert (2100hrs) + Mwananchi

Mytake:
Moto ndiyo umeanza rasmi kuwaka sasa,lets see if CCM are really ready for this huko bungeni au watachinjia baharini.
 
Suala la katiba mpya Tz kwa sasa halikwepeki. The wind of change is sweeping across. Na kama ni vidonge,lazima Serikali imeze kipindi hiki. Ni hatua nzuri na inapaswa iungwe mkono na wadau wote wa bunge wakiwemo wale wa CCM. Nadhani ni wakati muafaka sasa hivi kuanza kuunda katiba mbadala. Vinginevyo mchakato wa kuunda katiba ni mrefu sana. Kwa maana nyingine, mapendekezo haya, yaendane na muundo wa katiba hiyo mpya.
 
walio ishiwa hoja watampinga na walitumwa na wananchi Bungeni watamuunga Mkono...
 
kwani CCM hawajui kwamba katiba mpya inahitajika na wananchi,mpaka ipelekwe huko bungeni kama hoja binafsi?
 
Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA, Mh Mnyika John John, ametangaza nia yake ya kupeleka hoja binafsi bungeni kudai katiba mpya ya Tanzania.

Source: Radio One news alert.

Mytake:
Moto ndiyo umeanza rasmi kuwaka sasa,lets see if CCM are really ready for this huko bungeni au watachinjia baharini.

Mbona kachelewa sana, Mheshimiwa Pinda kisha Tangaza kuunda tume ya Katiba, sasa hoja binafsi ya Mnyika na hoja ya Serikali iliotangazwa na Waziri Mkuu ipi yenye nguvu? Anataka kupoteza muda wa kujadili mambo muhimu, hili tayari linafanyiwa kazi. Mijitu mingine hata sijui huwa ina fikiri kinyume-nyume, siielewi.
 
kwani CCM hawajui kwamba katiba mpya inahitajika na wananchi,mpaka ipelekwe huko bungeni kama hoja binafsi?

Kwa wao huu sio muda muafaka..Tusubiri kidogo..hayo ndiyo maneno yao..hata raisi alisema huu siyo muda wake! Ila kama kweli watataka kukumbwa na kuenziwa esp JK, kupitisha na kukamilisha mchakato wa katiba vitafunika sehemu kubwa ya incompetence yake aliyoionesha katika kipindi cha miaka yake yote kumi..na watanzania watamuenzi..ngoja tuone km yupo tayari kuenziwa
 
Mbona kachelewa sana, Mheshimiwa Pinda kisha Tangaza kuunda tume ya Katiba, sasa hoja binafsi ya Mnyika na hoja ya Serikali iliotangazwa na Waziri Mkuu ipi yenye nguvu? Anataka kupoteza muda wa kujadili mambo muhimu, hili tayari linafanyiwa kazi. Mijitu mingine hata sijui huwa ina fikiri kinyume-nyume, siielewi.
hoja ya katiba mpya ipo kwenye ilani ya chadema na si ccm.pinda ndiye aliyechelewa
 
Hiyo tume unafikiri itaundwa keshokutwa? Kama kawaida ya serikali ni kupooza mijadala,sidhani na sitegemei kama hiyo tume itaundwa kwa urgency inayotakiwa..! Nice move Mnyika,isitoshe yeye anapeleka hoja kwenye chombo kikuu kinachohusika na utungaji wa sheria yenyewe, so kama kuna haja kweli na Pinda anamaanisha alichosema basi itaundwa tume huru ya Bunge ya katiba..bado hiki ni kipimo tosha kwa Pinda na Bunge lake if they are really seriuos kwnye katiba au ni funika kombe ....
 
hoja ya katiba mpya ipo kwenye ilani ya chadema na si ccm.pinda ndiye aliyechelewa

Hata Kikwete alisema kama kuna mazuri kutoka kwa upinzani kwa nini tusiyatimie. Kama ipo kwenye ilani ya chadema basi pia si jambo jipya kwani ipo kwenye ilani ya CUF tokea mwaka 2000. Wala hakuna ubaya wa kuwepo tena kwenye ilani ya Chadema, na kama Waziri Mkuu katangaza kushughulikia sual la katiba, huoni kuwa ni jambo jema na sifa kwa Chadema kwa kuwa ni ilani yao imepewa kipaumbele? Tatizo ni nini hapo?
 
Yeah, we must be aware that 'it is said that the present is pregnant with the future'. Anybody working to derail us from this cause must be considered hostis humani generis (enemies ofmankind). We must demonstrate our desire to do the right thing for our own betterment, knowing that better is the enemy of good.
 
go Mnyika go... tumechoshwa na serikali inayoendeshwa kimajungu....leo mara Six kapigwa chini mara Tido....waswazi ni wakuwaogopa....
 
Mbona kachelewa sana, Mheshimiwa Pinda kisha Tangaza kuunda tume ya Katiba, sasa hoja binafsi ya Mnyika na hoja ya Serikali iliotangazwa na Waziri Mkuu ipi yenye nguvu? Anataka kupoteza muda wa kujadili mambo muhimu, hili tayari linafanyiwa kazi. Mijitu mingine hata sijui huwa ina fikiri kinyume-nyume, siielewi.
Yaani wewe akili yako ni ndogo sana, Pinda kama ulimsikiliza vizuri alisema wataangalia kuyafanyia kazi mambo yanayolalamikiwa, maana yake ni kwamba swala la kuandikwa katiba mpya halipo watakachofanya ni kuweka viraka. Na kama nilivyokwisha kusema hivyo viraka watakavyo viweka bado vitakuwa vinapendelea CCM. CCM kamwe hawatajichimbia kaburi lao. Katiba nzuri iliyozingatia matakwa ya wananchi italetwa na chama tofauti na CCM. NAOMBA UYANUKUU MANENO YANGU HAYO.
 
Mbona kachelewa sana, Mheshimiwa Pinda kisha Tangaza kuunda tume ya Katiba, sasa hoja binafsi ya Mnyika na hoja ya Serikali iliotangazwa na Waziri Mkuu ipi yenye nguvu? Anataka kupoteza muda wa kujadili mambo muhimu, hili tayari linafanyiwa kazi. Mijitu mingine hata sijui huwa ina fikiri kinyume-nyume, siielewi.

Kazi unayo mwaka huu khe khe kheeeeeeeeeeeeeeee

ccm is the first victim in the verdict of the trial "the long oppression of tanzanian natives" to be delivered in 2015 elections at the expense of fresh, new and virgin constitution

Aludra continue ..... pipos pawa..... JJ private motion is an aggravating circumstance to denounce the need of new draft constitution is legitimate
 
Mbona kachelewa sana, Mheshimiwa Pinda kisha Tangaza kuunda tume ya Katiba, sasa hoja binafsi ya Mnyika na hoja ya Serikali iliotangazwa na Waziri Mkuu ipi yenye nguvu? Anataka kupoteza muda wa kujadili mambo muhimu, hili tayari linafanyiwa kazi. Mijitu mingine hata sijui huwa ina fikiri kinyume-nyume, siielewi.

Usihukumu kabla ya kujua kinachokusudiwa! Hakuna asiyejua usanii wa ccm, Kombani alidai kuwa apelekewe draft, Pinda anadai eti anataka akamshauri JK, Makamba atatokea atadai kivyake, Chiligati, Kinana, Salma (sijui amepotelea wapi mama yetu) vile vile! Miaka 5 itaisha patupu kama ahadi hewa nyingine tulizopewa! Acheni basi watu wenye nia njema na nchi yetu, akina Mnyika, kuifanya kazi hiyo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom