Mnyika kufuatilia sheria ya kudhibiti kodi za nyumba

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Imeandikwa tarehe 24 Oktoba 2012 na Oscar Job | HabariLeo

mnyikaz_300_289.jpg


MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) ameahidi kufuatilia utungwaji wa sheria ya udhibiti wa kodi za pango itakayounda mamlaka ya udhibiti wa kodi za nyumba na gharama za vifaa vya ujenzi.

Mnyika ametoa ahadi hiyo jana katika taarifa aliyoituma kwa vyombo mbalimbali vya habari ikieleza kuwa ahadi hiyo inatokana na maombi ya taarifa ya Chama cha Wapangaji wa Shirika la Nyumba (CHAWASHINYU) katika mkutano wa wapangaji wa Shirika la Nyumba uliofanyika Jumapili ijayo jijini Dar es Salaam.

Mnyika alisema ibara ya 63 ya Katiba imeweka wazi kuwa wabunge wanapaswa kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi na kutunga sheria hivyo ameitikia mwaliko wa mkutano huo kutimiza wajibu huo na kuchukua kazi hizo kibunge kwa kuwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi haijawasilisha bungeni sera na sheria kama ilivyoahidi.

"Awali wakati uchumi wa nchi unaendeshwa na dola kulikuwa na udhibiti wa kisheria. Hata hivyo, baadaye sheria hizo zikafutwa kwa kisingizio cha nchi kufuata mfumo wa soko huru lakini ukweli ni kuwa hili la sasa sio soko huru, ni soko holela kwa kuwa hata soko huria lina sheria na kanuni ikiwemo udhibiti," alisisitiza Mnyika.

Mnyika alisema ongezeko kubwa la kodi za nyumba na gharama za vifaa vya ujenzi ni matokeo ya udhaifu wa kisera, kimfumo na kitaasisi katika sekta ya nyumba na makazi.

Aidha alisema katika mazingira ya sasa ya upungufu wa nyumba hususani mijini na gharama za juu za ujenzi, bila kuwa na mfumo wa udhibiti, mzigo mkubwa utawaelemea wananchi sio wapangaji wa Shirika la Nyumba (NHC) pekee, bali wakazi wengi.

Alisema suala hilo limeshajadiliwa bungeni ambapo awali mwaka 2011 liliwasilishwa bungeni na Waziri Kivuli wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Halima Mdee ambapo Kambi ya upinzani iliitaka serikali iweke utaratibu utakaotambulika kisheria utakaoweka mwongozo.

Hata hivyo, aliyekuwa wa kwanza kuwasilisha hoja binafsi ya suala hilo, alikuwa Mbunge wa Bumbuli, January Makamba (CCM), kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia.

Mnyika alisema atamtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi atoe kauli hatua iliyofikiwa katika mchakato wa kukamilisha sera ya nyumba na kuandaa muswada wa sheria husika na lini azimio hilo la bunge litatekelezwa kwa ukamilifu.
 
Mnyika ametoa ahadi hiyo jana katika taarifa aliyoituma kwa vyombo mbalimbali vya habari ikieleza kuwa ahadi hiyo inatokana na maombi ya taarifa ya Chama cha Wapangaji wa Shirika la Nyumba (CHAWASHINYU) katika mkutano wa wapangaji wa Shirika la Nyumba uliofanyika Jumapili ijayo jijini Dar es Salaam.

Kwa hiyo anatumiwa na Chama cha Wapangaji wa Shirika la Nyumba (CHAWASHINYU)? Wapangishaji je? Huu nao ni udhaifu kuliko wa JK
 
Kwa hiyo anatumiwa na Chama cha Wapangaji wa Shirika la Nyumba (CHAWASHINYU)? Wapangishaji je? Huu nao ni udhaifu kuliko wa JK

Kati ya mpangaji na mpangishaji nani anashida ya kutetewa? Hoja ya udhaifu kwa Mnyika J haina mashiko.
 
Kazi nzuri sana mnyika, haki ya makazi mavazi na chakula ni vitu muhimu sana kwa maisha ya binadamu, nchi hii kwenye miji mikubwa unaweza kupata mavazi na chakula kwa urahisi lakini malazi ni gharama kubwa sana..ni jambo la muhimu kwa serikali kujenga nyumba za gharama nafuu kwa wananchi wake pia kutafuta namna nzuri ya kudhibiti bei za upangishaji na ikiwezekana kuwe na sheria maalum ya vipindi vya ulipaji kodi isizidi miezi sita.
Mungu akubariki Mnyika..
 
n00b Ni vema wenye nyumba wakalipa kodi kama wafanya biashara wengine mana wapo wenye nyumba wanaopata pato kubwa.
 
Last edited by a moderator:
Ni wazo zuri ila awe mwangalifu na law of supply & demand. Kodi ya nyumba ni kubwa kwa sababu kuna upungufu mkubwa wa nyumba hivyo economic rent. Ukiweka vikwazo kwenye kodi utasababisha uwekezaji kwenye nyumba upungue na kulifanya tatizo la nyumba kuwa kubwa. tunaweza kudhibiti mfano bei ya daladala kuzuia cartel (zipo nyingi) lakini kwenye nyumba hakuna cartel tatizo ni uhaba. Serikali ilipaswa asimilia 75 ya watumishi wake wote wakiwamo waalimu na wanajeshi wawe kwenye nyumba bora. Haijafanya hivyo ni moja ya tatizo. Kwa kifupi tatizo ni uwekezaji duni kwenye sekta ya ujenzi. Ila hilo la kodi naunga mkono asilimia 100
 
I hope hayo marekebisho yata-address pamoja na mambo mengine, suala la kulipa kodi ya nyumba in advance kwa miezi sita au mwaka wakati sijawahi kuona mwajiri analipa mishahara in advance kwa upande wa wafanyakazi. Kodi inapaswa kulipwa mwezi kwa mwezi kulingana na mishahara inavyolipwa na sio huu uhuni wa advance ya miezi sita mpaka mwaka.
 
this is not practical kuepusha usumbufu serikali ijenge nyumba zake ili kupunguza demand obvious bei itashuka haya mambo ya kunganganiza bei fulani ndio mwanzo wa wenye nyumba kuacha kufanya matengenezo au kama demand ni kubwa kwanini nimpangishe Ali anayetoa pesa ndogo wakati kina Abdallah na Chiriku wanaweza kunipa dau kubwa?
 
Back
Top Bottom