Mnyika fanya kazi yako, la sivyo 2015 utashindwa ubunge

Mimi nakaa ubungo, maeneo ya mbezi luis mitaa ya magarisaba, kule kunatengenezwa barabara sasa.
greda linapita kuchonga barabara, japo wananchi mnachangia kidogo hela ya mafuta (mm sijachanga
lakini brbr imeshatengenezwa). Eneo la kata fulani pana kiongozi wa chamachetu ni mmama, yeye aligoma greda lisipite eti kwa nn wapinzani waweze, walimwita yule mm wakamsuta kama mtt mdogo, siku iliyofuata yaani jmosi iliyopita greda likafanya kazi.

Mm naona walau kumefanyika kitu, japo nilienda kupiga kura na uzee wangu sijajuta sana kwa kuwa hakujawahi kufanyika chochote toka ccm imezaliwa.

Nashauri wale walalamikaji wajipange ili wajiletee maendeleo msibweteke kumngoja mnyika, naye ni mtu kama ww
tena mjue kabisa kuwa hana say kwenye serkali yetu ya kifisadi.

Nawasilisha.
 
kama wewe ni mwalimu basi ni wa vidudu, hujui hata kazi za Mbunge ni zipi na za serikali ni zipi unataka Mnyika alime barabara alete maji kwa fungu lipi la hela? hujui kwamba tunalipa kodi kwa serikali ili ifanye hayo? kazi za Mbunge ni kuisimamia serikali na kutunga sheria na kwa kuwa serikali yenu ya magamba imeshindwa tutaiondoa 2015 ili Mnyika apate serikali sikivu na yenye uchungu na watanzaania ya kuisimamia, kama umetumwa na huyo mwana magamba mwenzako Nape mwambie amechemka sana. alafu habari za aina hii peleka kwa vilaza wenzako huko mtaani. eti Mnyika unamjua kuliko yeyote humu wewe ni mke wake?
 
kabla ya kujadili hoja kama hizi kwanza tunataka kujua kama mtoa maada ana uelewa wa kile alichokiandika, ni ajabu kwamba jitu linaingia humu jf kuleta mishuzi tu, je unajua kazi za mbunge, msitake kuleta ujinga wa magamba hapa kugeuza wabunge ATM mwishowe tunapeleka vilaza bungeni kulala tu, Mnyika ataendelea kuwa mbunge kwa mda mrefu sana. kwasababu anafanya kazi zake za kibunge vizuri.
 
Nakaa Ubungo, ni kweli huyo jamaa hajafanya lolote.Sehemu kubwa ya jimbo haina kabisa huduma ya maji au maji hayatoki mabombani,barabara ndo usinikumbushe machungu nabadilisha bush za gari kila leo.barabara ni mbov asikwambie mtu.Foleni ya mataa kila mtu anayeishi dsm ni shahidi.Mbaya zaidi anapatikana kwa bluetooth jimboni kwake! Ni kwa roho safi tu Mnyika anatakiwa arudi jimboni kusikiliza wananchi na kuweka mambo sawa.YOTE YAWEZEKANA.

Mwezi wa tatu sasa hakuna maji hapo maeneo ya kibangu. hebu ukawabip na dawasco waje kurekebisha mabomba yao ya kichina waloweka.
 
Huu uzi ulikuwa hewani nikataka kuchangia lakn kwa mshangao nikakuta naambiwa niwasiliane na moderators! Njia rahisi kwangu imeamua ni kuianzisha tena.

Jamani eneo la Ubungo Kibangu tuna matatizo makubwa ya maji na barabara. Eneo hili lipo umbali mchache kutoka kituo kikuu cha mabasi cha ubungo lakini ukifumbwa macho na ukaletwa kwenye eneo hilo unaweza kudhani upo mpakani kwa nchi. Huduma ya maji imekuwa ni ya kubabaisha na barabara ni mbovu hailezeki, barabara imejaa mashimo hauna mfanowe! saivi vijana wameamua kujichukulia hatua ya kumwaga vifusi barabarani na kuvisambaza huku wakiomba donei ya shilingi mbili tatu. Jamani!! Utafikiri halmashauri haina uongozi au Jimbo halina Mbunge wa kutetea maslahi ya wananchi walomchagua? Haya ni matusi kwa nchi yenye rasilimali tele.

Ubovu wa barabara umesababisha daladala zinazosafiri maeneo ya huko kuongeza nauli kutoka 200 hadi 300, pikipiki kutoka 1000 hadi 1500-2000 wakilalamika ubovu wa barabara unaongeza gharama ya matengenezo ya vyombo vyao. Mtandao wa maji umefika maeneo machache na mbaya zaidi maji yenyewe hayatoki! Na mbaya zaidi dawasco wamekuwa mahiri sana wa kukurupuka na kuleta bili ya maji (cjui ni kwa maji gani wanayotoa!). tunaomba mbunge wetu mnyika asikie kilio cha wananchi waliomchagua ili kupata ufumbuz wa mambo hayo, angalau kuwe na barabara hata ya kiwango cha changarawe basi! Na kuhusu hao dawasco tunafahamu wana mkataba wa huduma kwa wateja, kwann mkataba usiangaliwe kujua majukumu ya kila pande ni yepi na je mkataba unazingatiwa au unakula upande mmoja tu?
 
Nina hasira nao hawa watu.
 
Naunga Mkono. Njia ya Mchichani - Makoka ilileta mzozo kidogo hapa nyuma baada ya wenye daladala kugoma kutoa huduma kwa sababu ya ubovu wa barabara. Katika mzozo huo mambo kadhaa yalijitokeza.

1. Wenye mabasi huchanga fedha kila siku na baadhi ya fedha hizo hukabidhiwa kwa wenyeviti wa serikali za mitaa ya Makoka na Chipkizi. Kwa kifupi fedha hizo zinaliwa na mwenyekiti wa Mtaa wa Makoka (CDM) na wa Chipkizi (CCM). Mzozo huu ulizimika kimya kimya kwa barabara kukwanguliwakwanguliwa na jembe la mkono.

2. Maelezo yaliyotolewa na wenyeviti hao kuwa baadhi ya fedha zilishatumika kukarabati barabara si kweli. Barabara ilikarabatiwa na Bulldozer la manispaa na mafuta na vifusi vilinunuliwa na fedha za Mfuko wa pamoja wa ukarabati wa barabara wa Kanisa Katoliki Kibangu na Serikali ya Mtaa wa Kajima.

Nafikiri ingekuwa vyema kwa mbunge kufuatilia jambo hili kwani kiasi cha fedha kilipotea ni kikubwa (millions) na ile kawaida ya kufukiafukia mambo imechukua mkondo wake huku waliotafuna fedha wakiendelea kutesa na barabara bado ni mbovu.
 
Huu uzi ulikuwa hewani nikataka kuchangia lakn kwa mshangao nikakuta naambiwa niwasiliane na moderators! Njia rahisi kwangu imeamua ni kuianzisha tena.

Jamani eneo la Ubungo Kibangu tuna matatizo makubwa ya maji na barabara. Eneo hili lipo umbali mchache kutoka kituo kikuu cha mabasi cha ubungo lakini ukifumbwa macho na ukaletwa kwenye eneo hilo unaweza kudhani upo mpakani kwa nchi. Huduma ya maji imekuwa ni ya kubabaisha na barabara ni mbovu hailezeki, barabara imejaa mashimo hauna mfanowe! saivi vijana wameamua kujichukulia hatua ya kumwaga vifusi barabarani na kuvisambaza huku wakiomba donei ya shilingi mbili tatu. Jamani!! Utafikiri halmashauri haina uongozi au Jimbo halina Mbunge wa kutetea maslahi ya wananchi walomchagua? Haya ni matusi kwa nchi yenye rasilimali tele.

Ubovu wa barabara umesababisha daladala zinazosafiri maeneo ya huko kuongeza nauli kutoka 200 hadi 300, pikipiki kutoka 1000 hadi 1500-2000 wakilalamika ubovu wa barabara unaongeza gharama ya matengenezo ya vyombo vyao. Mtandao wa maji umefika maeneo machache na mbaya zaidi maji yenyewe hayatoki! Na mbaya zaidi dawasco wamekuwa mahiri sana wa kukurupuka na kuleta bili ya maji (cjui ni kwa maji gani wanayotoa!). tunaomba mbunge wetu mnyika asikie kilio cha wananchi waliomchagua ili kupata ufumbuz wa mambo hayo, angalau kuwe na barabara hata ya kiwango cha changarawe basi! Na kuhusu hao dawasco tunafahamu wana mkataba wa huduma kwa wateja, kwann mkataba usiangaliwe kujua majukumu ya kila pande ni yepi na je mkataba unazingatiwa au unakula upande mmoja tu?

Jimbo la ubungo ni kubwa sana,kwa kuangalia tu eneo la kibangu ni kati ya maeneo mazuri yenye unafuu mkubwa ukilinganisha na maeneo mengine yaliyo ndani ya jimbo.Tembelea maeneo kama saranga,bonyokwa na Golani utona hali ilivyo mbaya.Miundombinu ilivyo mibaya imesababisha hali ya maisha iwe juu maeneo hayo kuliko hata masaki.Nilienda kibangu nikanunua kg 1 ya nyama ng'ombe kwa shs 4000 wakati maeneo tajwa ni shs 6000. Mnyika ni mchapakazi kuna mambo mengi tu ameonesha kuyafanyia kazi anachotakiwa ni kupewa muda na kuungwa mkono na siyo kupewa mashinikizo ya ovyo ambayo hata rais wa nchi yamemsababisha achelewe kutoa maamuzi muhimu ya nchi kwa kuogopa malumbano.Swala la maji na barabara ni tatizo la muda mrefu ambalo mnyika hawezi kulimaliza kwa muda huu mfupi aliokaa kama mbunge ambao ni chini ya mwaka mmoja.Kwanza sijui kama wewe ni mfuatiliaji wa issues,maana hakuna kipindi kibaya kifedha ambacho serikali imewahi kuwa nacho kama sasa.Activities nyingi zimekuwa cancelled kwa sababu nchi haina fedha. sasa nyinyi kibangu mkiandamana(na si ubungo yote) hela ya kutatua matatizo yenu itatoka wapi.Daraja la mto unaotenganisha suka na golani lilitengewa pesa, ujenzi umeshindwa kufanyika kwa sababu hela haipo.Manispaa na halmashauri nyingi nchini hazijapata mgawo wao kwa muda sasa kwa sababu hamna hela.
 
hivi haya mambo diwani wenu anayajua? au mnaropoka tuu humu, mngeanza kwanza kumuwajibisha diwani husika wa kata yenu ili amuwajibishe mmbunge wenu. sisi huku msewe diwani ndo mpango mzima ijapo mwenyekiti wa mtaa ndo anazingua.
 
tatizo si mnyika bali halmashauri yawilaya ya kinondoni, na pengine si wao ila wamezidiwa na ukubwa wa wilaya ya kinondoni. Kiuhalisia Wilaya ya kindondoni inapaswa kuwa na halmashauri zaidi ya moja na au ipasuliwe itoke wilaya nyingine moja au mbili na halmashauri ziwe mbili au tatu. Ni kubwa mno!
 
Kazi ya Mbunge ni kuwakilisha wananchi, kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa serikali. Hizo kazi zote zinahitaji Mbunge kwenda eneo husika (sio kutulia ofisini asubiri taarifa za kuletewa), kutembelea wananchi kusikiliza yanayowakuta wananchi wake. After ol Mbunge hatapimwa kwa utendaji wa diwani, bali ni kwa utendaji wake!
 
tatizo si mnyika bali halmashauri yawilaya ya kinondoni, na pengine si wao ila wamezidiwa na ukubwa wa wilaya ya kinondoni. Kiuhalisia Wilaya ya kindondoni inapaswa kuwa na halmashauri zaidi ya moja na au ipasuliwe itoke wilaya nyingine moja au mbili na halmashauri ziwe mbili au tatu. Ni kubwa mno!
Hivi ukubwa wa Kinondoni unasababisha matatizo tu? Mimi nilidhani kuwa na kwa upande wa pili ukubwa huo unasababisha mapato yawe makubwa pia kutokana na shughuli mbalimbali za kijamii na kibiashara humo (UBT-bus terminal, masoko, maduka, ukusanyaji wa takataka, viwanda (power plants, textile, cement, chibuku etc)
 
Binafsi ningekuwa na Mbunge kama Mnyika ningefarijika sana na ningempa ushirikiano wangu wa dhati, tatizo ninaloliona hapa sometime Wabongo tumekaa kimajungu majungu, maana mimi ambaye sio mkazi wa Ubungo nina access ya kumuuliza na kutaka ufafanuzi wowote kutoka kwa Mnyika na atanijibu, sasa inakuwaje mkaazi wa Ubungo usiwe na hizo access?

Tujifunze kuwabana madiwani wetu maana kuna majukumu mengine hupaswi kumlaumu Mbunge yanakuwa ni majukumu ya diwani na kwa tabia za wabongo sioni kama hawa madiwani huwa wanabanwa kiasi kwamba wajue majukumu yao.
Ulalamishi huu wa kitoto ndio maana saa nyingine tunamuona JK mbaya na majibu yake kama, Mimi sio wingu kufanya mvuwa inyeshe ili kujaza mtera au majibu kama Mzee nyerere alitoka akaingia Mzee Mwinyi hakuyamaliza matatizo, akaja Mzee Mkapa nae hakuyamaliza na mie nitaondoka sitoyamaliza!!
 
Naomba niulize, mkisema mtumie maji ya visima vilivyochimbwa kwa mashine, maji vipi, ni ya chumvi? Sisi huku mtaani kwetu (DSM) hatuna haja na maji ya bomba la Ruvu, wananchi wanajiorganise, wanachimba visima, wanateua kamati ya kuendesha mradi na maisha yanaenda. Kamati inatafuta wafadhili zaidi na mradi unapanuka. Anayetaka maji anagharamia bomba (urefu wa kutoka nyumbani kwake hadi lilipo bomba kuu) na mradi unamuwekea mita. Ingawa wanatoza kwa unit, ukiconvert unakuta bei ya lita 20 za maji (ndoo kubwa) ni sh. 25/= tu !! Sijawahi kukosa maji tangu niunganishiwe bomba, na tunatoa ushirikiano kwa Kamati kutoa taarifa in case of any hujuma against the project. Kama eneo lenu halina maji ya chumvi, you may copy this!
 
Hapo ndio wananchi tunapokosea. Vema kufuatilia na kujua kazi za Mbunge. Wanaohusika na maji ni DAWASCO na barabara ni Halmashauri (au TANROADS kwa baadhi ya barabara kubwa). Anayetakiwa kuwafuatilia hao ni Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wilaya. Ikishindikana kabisa Mkuu wa Mkoa. Serikali ndio ina nyenzo ya kutatua kero hizo. Kazi ya Mbunge ni kuwawakilisha, kuisimamia serikali, shughuli za bungeni n.k. Mnyika ni Mbunge mzuri, naamini pamoja na kuwa hilo sio jukumu lake lakini akilipata atajitolea kufuatilia.
 
Back
Top Bottom