Mnyika fanya kazi yako, la sivyo 2015 utashindwa ubunge

Tatizo lenu mnategemea vitu vikubwa sana, tena kwa muda mfupi sana kana kwamba alieingia kwenye Uongozi ni Mungu,
Uchaguzi umefanyika October 2010 na mpaka mtu atulie kwenye kiti aanze kazi ni labda ni Dec au January '11,
Msipende kunung'unika nung'unika kila mara!!!
 
Ni tabia nzuri kwa wananchi kufanya tathmini ya viongozi wao, mwaka 1 ni muafaka kufanyiwa evaluation pia . Kenya walifanya siku 100. Tusiwakatishe tamaa wananchi wetu pale wanapotofautiana na mivuto au yale tunayoshabikia.Nawasihi tuache matusi na mwenye mafanikio au mazuri yaliyofanywa aweke humu kwa viwango vinavyo weza kupimwa na mwanchi wa kawaida.Tunapoteza busara za jf kwa kuchangia hoja muhimu kwa matusi. Mnyika ni mbunge alieaminiwa sana na wana ubungo. Je amefanikiwa kiasi gani ,Je aache nini, afanye kipi? Hapa tutakuwa tunamsaidia mbunge si kumfundisha matusi kama kucamerun na mengine.
 
Najua wenye ugonjwa wa vyama mtanuna.
Nikiwa mwana Ubungo nakuagiza mh mbunge wangu uanze kutimiza ahadi ulizotupatia. Sioni au kufahamu hata effort. Mpaka sasa hujafanya chochote zaidi ya maneno,mikutano isiyo na matunda na kuwa blogger. Hatujakutuma hicho wala malumbano. Barabara hatuna,maji kulekule,ulinzi mh haya sioni kipya cha zaidi ya mbunge aliyepita.

Nakuagiza anza kazi ili nisijutie kura yangu, mambo ya kuuza sura hayaendani na wewe. Nilikupigia kampeni ya hali na mali sitaki kujutia efforts zangu. Bado miaka 2 sababu after 2014 utakuwa busy kujipanga kurudi mjengoni. Nataka niwe na sababu tena ya kukukampenia vinginevyo umpishe NAPE mi sing'ang'anii Chama.

Wananchi tuache unafiki na siasa Tuwasukume wabunge watufanyie kazi sio kutafuta umaarufu ambao hautsaidii. tutake vitu tangible. Nchi hii ni yetu wote.


Vyama vinawafanya watu kupoteza uwezo wao wa kutafakari, Ebu mnaompinga mtoa hoja wekeni ushahidi ..1,2,3 aliyoyafanya mnyika. badala ya kumtusi na kukejeli mtoa hoja; Wengi tunapenda mabadiliko ya kweli si ya sura (KEENJA TO MNYIKA). Mimi ni mkazi wa Sinza na nilivote for Mnyika ningependa nijue mkuu so far umafanya nn; MANA SIJAONA MABADILIKO YOYOTE TOKA UINGIE BUNGENI.
 
Mtoa thread tunajua unakanyagwa na huyo NAPE.


Kumtukana mtoa hoja si kumsaidia Mnyika kurudi Bungeni 2015, Tumchallenge, tumsapoti na tumsaidie kutekeleza ahadi zake......thats the way to 2015 victory.
 
Haya Wapendwa, Huyu jamaa anayesema kuwa Mh. Mnyima hajafanya kitu chochote nadhani ana lake jambo. Nilidhani watu wanaotoa mawazo ndani ya Jamii forum wana akili timamu kumbe hata nguruwe watu nao wanashiriki kutoa mawazo. Ubungo ni jimbo linalokuwa, miundo mbinu haikuwa mizuri miaka mingi nenda rudi. Unataka Mnyika achukue jembe alime barabara? Usimamizi anaoufanya jimboni huuoni? Ama kweli nguruwe hawezi kuwa punda. Maana Punda habebi mzigo akiwepo mwanae. Je wewe uko wapi na elimu yako ni kiasi gani mpaka unashindwa kuiona kazi Mh. Mnyika?

Ni bahati mbaya kwa sasa kuna mgomo wa madaktari, unatakiwa uchunguzwe akilli, kama inawezekana kimbilia muhimbili wakuchunguze waone kama uko sawa. Vinginevyo watu watakushangaa! Kwa taarifa yako Mh. Mnyika ni miongoni mwa wabunge wachache wanaofanya vizuri shughuli zao za kibunge. Hatupendi watu wanaolala na wezi wa mali ya umma. Chama cha Majambazi mmezidi mno. Mnafikia hatua ya kuiba kwa kutumia maka.....o.
Jiulize mara mbili
Kwa heri
 
ghasia amewafanyia nini huko mtwara?
Wasirra miaka yote ya ubunge amefanya nini?
Azan amefanya nini?
Nk nk nk

wanasiasa/wabunge wote hakuna wafanyacho,labda kujiongezea posho
 
Njoo kwangu uone mabadiliko kama kwako hayapo. Maana sina uhakika kama kweli ulimchagua Mnyika? Acha kujipendekeza, mlijaribu kuiba kura za mnyika mkashindwa kwani zilikuwa nyingi mno. Badala yake mkaanza kujipendekeza kwamba mlimchagua. Kafie mbele huko kama kwenu hakuna mabadiliko. Hata hivyo mabadiliko unajiletea mwenyewe, wewe kaaa chali usubiri wazungu walete misaada yao ya masharti wakiwa wanataka wanaume nanyi muwe mnaposwa!!! Kama hayo ndo mabadiliko mnayotaka kuyaona basi ng'ang'ania majambazi yabaki madarakani. Maana yamechukua kila kitu alafu mwisho wa siku unaletwa mswada kwamba mwaunaume kuolewa na mwenzake ruksa, na CCM kwa vile ni wengi Mjengoni watasema ndiyoooo! Sasa mtakoma, mpaka Babu zenu nao wataolewa!!! Fikiri vizuri, acha utaahira. Mnang'ang'ania CCM kwani chama cha babako. Wizi mtupu.
Mkome kwa tabia zenu mbaya. Ona mbali, Cameroon ataleta posa za Pound! hapo ndipo utakapojua nini maana ya mabadiliko.
Kenge mkubwa
 
Ulitaka akubebe?

keenja alikuwa mbunge wa ubungo kwa miaka kumi huyu Mnyika hardly ana miaka miwili nadhani matatizo ya jimbo la ubungo ni matatizo yaliyochangiwa na viongozi waluopita, kitu ambacho Mnyika anaweza kufanya ni kuainisha matatizo lukiko yaliopo na kupeleka kunakostahili , kumlaumu mnyika hamumyendei haki
 
kwani mnyika hajaleta hata maji? nilikuona ameandamana na wapiga kura wake kudai maji... sio ndio juhudi hizo...?
 
Mnyika yuko busy kutafuta mchumba, akishapata atawakumbuka jamani kuweni wapole!
 
Ubungo ni Jimbo kubwa..na Rome haiwezi kujengwa kwa siku moja! katika kazi maridhawa za Mbunge Mnyika ni ile barabara ya Ubungo Msewe, Kuanzia Bahama mama inayopita Changanyikeni hadi Chuo Kikuu. Wiki iliyopita tu, imefanyiwa tena Ukarabati mkubwa... Tembeeni muone.


Amesaidia kupatikana kwa daraja la uhakika Msewe, ambalo halikutikiswa na mvua iliyonyesha mwishoni mwa Desemba mwaka jana! na barabara inapitika vizuri...na imepunguza kwa Kiasi kukubwa msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro!

Bado wakazi wa Ubungo tuna changamoto Nyingi, lakini haziwezi kumalizwa na Mnyika peke yake, na pia haziwezi kumalizwa kwa kipindi cha mwaka mmoja!!
 
Mmeifanyia nini Tanzania katika miaka hamsini tangu tupate uhuru kwa domo? "Two things are infinite in Tanzania, the Nation itself and our stupidity"
 
Najua wenye ugonjwa wa vyama mtanuna.
Nikiwa mwana Ubungo nakuagiza mh mbunge wangu uanze kutimiza ahadi ulizotupatia. Sioni au kufahamu hata effort. Mpaka sasa hujafanya chochote zaidi ya maneno,mikutano isiyo na matunda na kuwa blogger. Hatujakutuma hicho wala malumbano. Barabara hatuna,maji kulekule,ulinzi mh haya sioni kipya cha zaidi ya mbunge aliyepita.

Nakuagiza anza kazi ili nisijutie kura yangu, mambo ya kuuza sura hayaendani na wewe. Nilikupigia kampeni ya hali na mali sitaki kujutia efforts zangu. Bado miaka 2 sababu after 2014 utakuwa busy kujipanga kurudi mjengoni. Nataka niwe na sababu tena ya kukukampenia vinginevyo umpishe NAPE mi sing'ang'anii Chama.

Wananchi tuache unafiki na siasa Tuwasukume wabunge watufanyie kazi sio kutafuta umaarufu ambao hautsaidii. tutake vitu tangible. Nchi hii ni yetu wote.

Umeambiwa Mnyika ndo anakaa na fuko la hela za hazina????
 
Huyo Mnyika ameahidi kutumia pesa zake binafsi kujenga barabara, kuleta maji n.k? Unakurupuka ndugu, mimi nakaa Ubungo lakini najua utaratibu wote lazima ufuate ngazi. Kama mnyika anapata kauzibe kwa walio juu unataka afanyeje? ajiuze? Ungetaka mteremko ungemweka Slaa pale uone makeke.

napita
 
Back
Top Bottom