Mnyika fanya kazi yako, la sivyo 2015 utashindwa ubunge

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Hivi karibuni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alitoa madai kuwa viongozi na watendaji wa Serikali wamekuwa wakiipuuza ofisi yake kiasi cha kupuuza ushauri wa kitaalamu unaotolewa na ofisi hiyo wenye lengo la kupunguza au kubana matumizi ya Serikali na kuongeza makusanyo ya Serikali ili kuipatia uwezo zaidi wa kuhudumia watanzania. Aliendelea kuwa viongozi na watendaji wa Serikali wamefikia hatua ya kuinyima ofisi yake ushirikiano kwa kuinyima nyaraka mbali mbali kwa lengo la kukwamisha ukaguzi wa fedha za umma hususan Shilingi Bilioni 48 katika mfuko wa kufufua uchumi ujulikanoa kama "Stimulus Package".

Katika kile kinachoonyesha kuwa tabia hiyo imekithiri kiasi cha kuwasababishia athari za kijamii na kiuchumi watanzania wa maeneo mabli mbali ya nchi hii, katika kikao cha bunge lililomalizika hivi karibuni Mhe John Mnyika amefichua sababu zinazopelekea wananchi wa jimbo lake la Ubungo kukosa huduma ya maji safi kuwa ni pamoja na DAWASCO kutotekeleza kikamilifu mapendekezo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuanzia 2007/8 ambaye aliitaka kuwekeza katika upatikanaji wa maji safi. Soma kiambatanisho.

Kwa hakika wabunge wa CHADEMA wanaonyesha kwa dhati kuwa wanafahamu wajibu wao bungeni kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) inaeleza wajibu wa Mbunge ni "Kuishauri na Kuisimamia" Serikali.

Mhe John Mnyika tunaomba utueleze zaidi ili tuweze kufahamu zaidi sababuz zinzosababisha tukose maji safi.

Nini maoni yako
 
Attachments

  • MNYIKA AMLIMA SPIKA BARUA.pdf
    333.5 KB · Views: 194
Najua wenye ugonjwa wa vyama mtanuna.
Nikiwa mwana Ubungo nakuagiza mh mbunge wangu uanze kutimiza ahadi ulizotupatia. Sioni au kufahamu hata effort. Mpaka sasa hujafanya chochote zaidi ya maneno,mikutano isiyo na matunda na kuwa blogger. Hatujakutuma hicho wala malumbano. Barabara hatuna,maji kulekule,ulinzi mh haya sioni kipya cha zaidi ya mbunge aliyepita.

Nakuagiza anza kazi ili nisijutie kura yangu, mambo ya kuuza sura hayaendani na wewe. Nilikupigia kampeni ya hali na mali sitaki kujutia efforts zangu. Bado miaka 2 sababu after 2014 utakuwa busy kujipanga kurudi mjengoni. Nataka niwe na sababu tena ya kukukampenia vinginevyo umpishe NAPE mi sing'ang'anii Chama.

Wananchi tuache unafiki na siasa Tuwasukume wabunge watufanyie kazi sio kutafuta umaarufu ambao hautsaidii. tutake vitu tangible. Nchi hii ni yetu wote.
 
Umekosea kumtaja aliyekutuma...Ungefunikafunika jina lake kwanza!
 
umeshuka fresh aya ya kwanza ya pili fresh! ukaja ukanya hapo kwenye red!
 
hao wa CCM waliopita wamefanya nn? mbunge wenu kafanya mengi ikiwemo kuhamasisha wanancnhi kujiletea maendeleo
au ulitaka atoe hela zake mfukoni akuletee ulotaja? lazima serikali ihusike kupitisha bajeti nao pia manispaa wanahusika
ndio maana kuna mkurugenzi wa manispaa,mkuu wa wilaya nk.
kumbe kakutuma ulomtaja umekosea sana kumtaja
 
Msimjibie kwa ushabiki naomba mnipe kipi cha maendeleo alichofanya so far. Mimi sio CCM kama mnavyodhani penye ukweli tuseme Mnyika fanya kazi. BADO
 
Mnyika naomba ushuke humu jf unishawishi kwa ulichofanya hata kama ni mipango. Usikalie tu kucheza na jukwaa tunataka magoli.
 
Nakaa Ubungo, ni kweli huyo jamaa hajafanya lolote.Sehemu kubwa ya jimbo haina kabisa huduma ya maji au maji hayatoki mabombani,barabara ndo usinikumbushe machungu nabadilisha bush za gari kila leo.barabara ni mbov asikwambie mtu.Foleni ya mataa kila mtu anayeishi dsm ni shahidi.Mbaya zaidi anapatikana kwa bluetooth jimboni kwake! Ni kwa roho safi tu Mnyika anatakiwa arudi jimboni kusikiliza wananchi na kuweka mambo sawa.YOTE YAWEZEKANA.
 
ni kweli hajafanya lolote, ubungo standi chafu sana... wakati kiingilio tshsh. 200/= zinaenda wapi? udsm wanalala wanne room ya watu wawili...kwa nini usiongee na wawekezaji waogeze hostel? daraja ubungo msewe hoi....maji ni tatizo la kudumu ubungo.....anafanya nini huyu lakini wakatia alipata kura yangu? ntalia mimim....au ndo nayeye anamshkia bango magufuli wakati yake yamemshinda!
 
Hukai ubungo wewe! Tunaokaa Ubungo tunakupuuza
Kweli maana hata sisi wa golani tunaona dalili nzuri kama ukarabati wa barabara yetu ya kwenda main road pale suka. Sasa hivi anafuatilia ujenzi wa daraja pale, ila naona magamba wanataka kuleta kiwingu. Kijana anafanya vizuri kwa muda wake mfupi ambao hata nusu mwaka hajafikisha
 
Mnyika naomba ushuke humu jf unishawishi kwa ulichofanya hata kama ni mipango. Usikalie tu kucheza na jukwaa tunataka magoli.

Ashuke humu ili iweje wakati wew hujaona alichokifanya, akili nyingine bana
 
Back
Top Bottom