Mnyika Bunge linakwisha, njoo uone ya jimboni

Mnyika kama hawakutaki njoo ktk jimbo letu wala kampeini hutafanya tutakupa kura za NDIYO.

Nafikiri aliyeanzisha thread hii kama siyo Hawa Nghumbi basi ni mpambe wake!
 
Hizi mania ni mbaya sana. Wewe badala ya kutuambia Mnyika kafanya nini unarejea kwenye historia. Tuliikataa CCM baada ya kuridhika kwamba hawakufanya vizuri wakati wa uongozi wao na ni baada ya kushawishiwa na Mnyika kutoka na sera na ahadi zake. Na kwa vile ahadi za mgombea kwa mpiga kura ni kama makubaliano kati ya pande mbili, tunachotaka afanye ni kutekeleza upande wake wa ahadi kwani sisi tumetekeleza la kwetu kwa kumpatia madaraka. Kinachoskitisha ni kwamba hata kule kuonekana akahamasisha wananchi kujitolea na kuchangia maendeleo hakuna.

Sasa kama una-resort kwenye matusi badala ya kujikita katika hoja, humsaidii kipenzi chako Mnyika maana atakapotuhitaji hatatuona na wewe hutamuokoa. Kilio hiki ni cha wana ubungo kwa sababu kero zilizopo hazichagui itikadi, in fact, wengi wa wanaolalamika ni wafuasi wake ambao walimnadi na sasa wanaona aibu kupita kwa watu waliokuwa wamewajengea matumaini makubwa. Kujibu swali lako, mimi nafikiri kwa kutumia kichwa na wewe mwenzangu unatumia moyo, ndo maana haya mapungufu ya Mnyika kwako wewe ni chuki na uzandiki. Bora Keenja alijenga madaraja na barabara za msumi, makabe na bonyokwa zilikuwa zinapitika.

Kama ni wana mageuzi wa ukweli ni vyema kuwakumbusha viongozi waliochaguliwa na wananchi kuwa ahadi ambazo walizitoa majimboni ndio mkataba wao wa ajira na waliowaajiri, kama hawatatekeleza hayo wananchi hawawezi kutofautisha waliowatema na waliowachagua
 
Mnyika ni useless, tulimuona kama ni mtu wa maana na mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko lakini hamna lolote. 2015 ubunge atausikia kwenye bomba.
 
Mleta hoja hajakosea katoa maoni/mawazo yake na sisi ndio tunayafanyia kazi. Wanachi wa jimbo la ubungo niwaambieni kwamba maendeleo yanaletwa na wanchi wenyewe ktk sehemu husika mbunge kama kiongozi anashauri, anafuatilia, an kuwajulisha mara kwa mara kinachoendelea.
Sisi huku Mbezi Beach tuliona barabara zimeharibika na masika ndio yalikuwa yanakaribia. Tukahamasishana tukapata hela ya kutosha mafuta ya greda na operator wake. Mtendaji wa mtaa akaenda manispaa akalipa tukapata greda likasawazisha zile barax2 tulizoziainisha. Sasa ndio tunapambana na tatizo la majambazi! Inawezekana..play your part.

Brilliant! Lakini kama mbunge angehamasisha hili au angewaambia wapiga kura wachangie mafuta yeye afanye mpango wa greda.
 
Join Date : 9th August 2012
Posts : 9

Rep Power : 302
Likes Received: 0

Likes Given: 0


Naona umeingia na kuanza na kamanda Mnyika, nadhani jaribu kujifunza namna ya kuandika na kupost hoja hapa JF...
Wewe ulitaka aanze na kuwasifia kina Slaa? JF sio mali ya CDM na sio kila member ni kibaraka wa CDM. Tatizo lenu mnafikiri kila mtu anakula posho ya propaganda kama nyie.
 
Wewe ulitaka aanze na kuwasifia kina Slaa? JF sio mali ya CDM na sio kila member ni kibaraka wa CDM. Tatizo lenu mnafikiri kila mtu anakula posho ya propaganda kama nyie.

Ndio Nape kakutuma uje kusema haya...kweli unakaa na kuandika hoja kama hii. Akili zako ni fupi kuliko kawaida.
 
Mkuu, kabla ya Mnyika kuna wabunge wangapi wa Chama cha Magamba waliowahi kuongoza Ubungo? Na ni wangapi wa CDM? Na hao Magamba wameongoza Ubungo kwa miaka mingapi? Na Mnyika kaongoza muda gani? Je, matatizo hayo yameibuka wakati wa Mnyika tu? Kama yalikuwepo tangu huko nyuma (na ni ukweli ndio maana hayajatatuliwa hadi sasa) nani tapeli, wabunge wa Mabwepande au Mnyika? Hivi kwa ku-post thread hii, unatumia kiungo gani cha mwili wako ktk kufikiri? Ni hayo tu Mheshimiwa, sasa naomba unijibu. Ahsante sana!

Sio sababu..
 
Huyo ana brain cancasion

Mkuu, kabla ya Mnyika kuna wabunge wangapi wa Chama cha Magamba waliowahi kuongoza Ubungo? Na ni wangapi wa CDM? Na hao Magamba wameongoza Ubungo kwa miaka mingapi? Na Mnyika kaongoza muda gani? Je, matatizo hayo yameibuka wakati wa Mnyika tu? Kama yalikuwepo tangu huko nyuma (na ni ukweli ndio maana hayajatatuliwa hadi sasa) nani tapeli, wabunge wa Mabwepande au Mnyika? Hivi kwa ku-post thread hii, unatumia kiungo gani cha mwili wako ktk kufikiri? Ni hayo tu Mheshimiwa, sasa naomba unijibu. Ahsante sana!
 
Acha kulea na kuupaka mafuta uzembe. Mbunge yeyote anpoingia madarakani anakuwa na platform yake ya uchaguzi na huyu bwana nilipokuwa nasikiliza na kusoma habari zake za kampeni, yale yaliyoorodheshwa na mwanzilishi wa thread hii ndo zilikuwa platform zake. Alipoahidi alipaswa kujua kwamba kuna financial or resource implications na alitakiwa kujua namna ya kuzipata. Katika hili hatutarajii afanye kama traffic anayemwambia mke wake abandike sufuria ya ugali yeye ankwenda barabarani kupiga bao ndo arudi na mboga.

Wala suala hapa siyo kupigania vioski viuze maji 20/= bila kujua wenye vioski wameyatoa wapi na kwa gharama zipi. Wala zile juvenile tricks za kufanya maandamano kwenda Dawasco (ambazo ni mbinu za kiuanaharakati na siyo za kiongozi) haziwezi kutatua kero. Mbunge anapaswa kuwa na mikono miwili ya kuhemea. Mmoja bungeni na serikalini, na mwingine kwa connections zake na washirika wa maendeleo na tumeona hili kule Karatu ambako shida ya maji ilikuwa kubwa lakini Dr (Phd) alitaguta wafadhili wakafadhili mradi wa maji na mambo yakawa poa.

Kuhusu barabara, mie ni shahidi. Last week nilikwenda kwa jamaa yangu maeneo ya Kimara Vyumba vinane. Nilitamani niache gari barabarani kusudi nichukue taxi kwa hofu ya kutoboa sample na hali hii ni kila mahali ndani ya maeneo ya pembezoni ya jimbo, ambako alichaguoiwa kwa kura nyingi kwa matumaini kwamba ahadi zake zingebadilisha mambo. Wanajuta.

Kuhusu kumchagua au kutomchagua kwenye uchaguzi uliopita, hiyo ni hoja kengeza. Mbunge hatakiwi kubagua katika kuhudumia na wala kutompigia kura hakumnyimi mwananchi haki ya maendeleo. Kura ji mchakato wa kidemokrasia na inawezekana yule alimkataa alikuwa na mashaka na uwezo wake. Mnyika awe na busara na kupuuza hoja za kishabiki zinazompamba ili akidhi matumaini ya wananchi wake waliosubiri miaka mitano ili wampe kura, baada ya kushindwa 2005. Hizi siasa za kitaifa na kulia lia hata sisi kule jimbo la Kawe tunapata shida hiyo hiyo.


Sisi kama wapiga kura wa Mh Mnyika, tunaomba yafuatayo;
1. Njoo wakazi woote wa kimara na vitongoji vyake, Msakakuzi, Makabe, Msumi, Mpiji, Mbezi nk ili usikie matatizo ya wananchi wako.
2. Njoo tukueleze kuwa sisi wakazi wa Msakuzi- Karibu na kwa MASISTA tunateswa sana na TANESCO. Hawa jamaa walikuja kuleta mradi wa umeme toka makabe hadi msakuzi-masitata. Cha ajabu waliishia njaiani na kutelekeza nguzo barabari zikioza yapata miaka miwili sasa. Wakati huo kitongoji cha pili karibu na kwa masista umeme unawaka. Tumejitahidi ili tununue nguzo na gharama zingine TANESCO inakataa kuwa huo si mradi wetu. Sasa tunajiuliza ni kwa nini mambo haya ynatendeka hivi. Tunaomba mbunge wetu uje tukueleze hizi shida zetu.
3. Maeneo ya msakuzi, Mbezi-luis, Kibamba kuna mabomba ya maji ya siku nyingi, lakini maji hayatoki. Mh. Mnyika tunaomba ututembelee ili tukuambie hizi shida upige ututetee watu wako.
 
Kweli mti wenye matunda hutupiwa mawe. Mnyika una watu kibao wanaotaka jimbo lako.
 
Join Date : 9th August 2012
Posts : 9

Rep Power : 302
Likes Received: 0

Likes Given: 0


Naona umeingia na kuanza na kamanda Mnyika, nadhani jaribu kujifunza namna ya kuandika na kupost hoja hapa JF...

hahahahahaha mbavu zangu!
 
Mnyika ni useless, tulimuona kama ni mtu wa maana na mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko lakini hamna lolote. 2015 ubunge atausikia kwenye bomba.

unaliwa akili yako na magamba wewe kula hukupiga wewe na magamba magamba na wewe nini unalia naona kazi nzuri ya kufanya mtu kama wewe ni kutoa mbwa kwa mzungu baadla ya kupwatuka pwatuka hovyo. M4c moyoni!
 
Mmerudi tena?
Kweli Mnyika amewashika pabaya sana. Narudia kusema tena, nyie kila mara mnaokuja na uzi wa kumwandama Mnyika, ni wanafiki, wafitini na wazandiki.

1. Hivi mlikuwepo zama zile za Ubungo kukosa maji halafu kuna Mh. akawa anatumia maji kwake hivyo kwa bustani na kuwanywesha ng'ombe?

2. Au yule mbunge, aliyekuwa anavaa JEANS bungeni halafu akawaambia wapiga kura wake "mnataka Maji, mnataka Nikojoe niwape maji"
 
Back
Top Bottom