Mnyika azuiwa kutoa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,709
Mbunge John Mnyika leo ameomba muongozo wa naibu spika ili atoe hoja ya kutokuwa na imani na majibu ya waziri mkuu, naibu Spika akamzuia kwa kumwambia ametafsiri kanuni ndivyo sivyo na kumtaka akae chini na apeleke hoja yake kwa maandishi.

TAARIFA KWA UMMA

Leo tarehe 11 Agosti 2011 katika kikao cha 48 cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi nilitaka kuomba muongozo wa Spika kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007 ) kifungu cha 68 (7) kuhusu maswali na majibu ya Waziri Mkuu na nikarejea pia kanuni ya 133 (1).

Hata hivyo, kabla hata ya kutoa maelezo kamili ya kuomba muongozo wa Spika nilizuiwa na Naibu Spika Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) bila hata ya kusikilizwa muongozo ambao nilitaka kuomba kinyume na kanuni ya 5 (1) inayotaka Spika kuongoza Bunge kwa kuzingatia kanuni na pale ambapo kanuni hazijatoa muongozo Spika anapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia katiba, sheria nyingine za nchi, kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya awali na desturi za kibunge.

Naomba kutoa taarifa kwa umma kwamba sijaridhika na uamuzi uliofanywa na Naibu Spika Mheshimiwa Job Ndugai hivyo nawajulisha kwamba ninakusudia kuwasilisha malalamiko kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu 5 (4) na 7 (3) mara baada ya kupata nakala ya kumbukumbu rasmi ya Bunge (Hansard) ya kikao husika.

Mara baada ya kunukuu kanuni husika nilipoanza tu kuzungumza kwamba katika kipindi cha Maswali na Majibu kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekuwa akitoa majibu yenye upotoshaji yasiyokuwa ya kweli; baada ya kauli hiyo kabla hata ya kumaliza maelezo niweze kuomba muongozo kwa Spika; Naibu Spika alinikatisha na kuninyima fursa ya kuomba muongozo kinyume na kifungu 68 (7) na 5 (1).

Naomba umma uelewe kwamba nilikuwa naelewa kwa kina mahitaji ya kanuni za bunge kifungu cha 133 na vipengele vyake kuanzia cha kwanza mpaka cha sita; ndio maana katika kuanza kuomba muongozo nikasoma kifungu cha 133(1).

Napenda umma ufahamu kwamba muongozo ambao nilitaka kuomba kwa Spika ni kwamba kumekuwa na kawaida ya Waziri Mkuu wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoa maelezo yasiyokuwa ya kweli yenye upotoshaji ambayo ni kinyume cha katiba ya nchi, sheria mbalimbali pamoja na kanuni ikiwemo kanuni za bunge hivyo nilitaka Spika atoe muongozo wenye kumpa nafasi nyingine Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi wa kweli kuhusu masuala husika ili kuepusha uwezekano wa wabunge kupoteza imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa kanuni za bunge kifungu cha 133.

Katika maelezo yangu ya kuomba muongozo huo nilikusudia kutaja mifano miwili mikubwa ya majibu ya Waziri Mkuu kwenye maswali ya papo kwa papo yasiyokuwa ya kweli yenye upotoshaji kuhusu kashfa ya Meremeta na kuhusu mgogoro katika Manispaa ya Arusha.

Ikumbukwe kwamba tarehe 14 Aprili 2011 wakati wa kikao cha saba cha mkutano wa tatu wa Bunge la Tanzania wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, nilimuuliza Mheshimiwa Mizengo Pinda kuwa "Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye vile vile ni Mwenyekiti wa CCM amenukuliwa akizungumzia kuhusu haja ya Chama kinachotawala kujivua gamba. Kati ya mambo aliyoyazungumza ni pamoja na kuondokana na watuhumiwa wa ufisadi. Mheshimiwa Mkuu uliwahi kulieleza Bunge hili tukufu kwamba usingetaka kabisa kuzungumzia masuala ya Meremeta kwa sababu ni siri za Jeshi. Baada ya kauli hii ya Rais na dhamira hii ya kujivua gamba kuhusiana na masuala ya ufisadi. Je, uko tayari Mheshimiwa Waziri Mkuu kutaja wahusika wa Kampuni ya Meremeta na kuelekeza Serikali kuchukua hatua zinazostahili kuhusiana na tuhuma hizo? . Waziri Mkuu katika majibu yake Mheshimiwa Mizengo Pinda hakuitumia nafasi hiyo kurekebisha kauli zake zisizokuwa za kweli zenye upotoshaji alizozitoa kwa nyakati mbalimbali katika Bunge la Tisa kuhusu kashfa ya Meremeta.

Ikumbukwe pia kwamba tarehe 10 Februari 2011 katika kikao cha tatu cha mkutano wa pili wa Bunge la kumi Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu maswali ya papo kwa papo ya Mheshimiwa Freeman Mbowe (Mb) kuhusu matukio yaliyojitokeza Arusha wakati na baada ya uchaguzi batili wa Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha. Tarehe 11 Agosti 2011 katika kipindi cha Maswali ya papo kwa papo ya Waziri Mkuu kuliulizwa maswali kuhusu maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA ya tarehe 6 na 7 Agosti 2011 kwa kurejea pia mazungumzo baina ya Waziri Mkuu na viongozi wa taifa CHADEMA kuhusu muafaka batili juu ya mgogoro katika Halmashauri ya Jiji la Arusha na uamuzi wa kuwafukuza uanachama madiwani watano kutokana na kukiuka maagizo ya kamati kuu. Badala ya Waziri Mkuu kuitumia nafasi hiyo kutoa majibu yenye kulenga kutoa ufafanuzi wa kurekebisha upotoshaji uliofanyika awali Waziri Mkuu Mizengo Pinda akatoa majibu mengine yasiyokuwa ya kweli kuhusu mazungumzo yake na viongozi wa CHADEMA pamoja na uamuzi wa chama wa kuwafukuza uanachama madiwani waliokiuka maamuzi ya kamati kuu ya chama.

Majibu ya Waziri Mkuu kuhusu ufisadi wa Meremeta, matukio katika halmashauri ya Jiji la Arusha na masuala mengine ya kitaifa katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo yenye uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri Mkuu yaliyoanishwa katika ibara ya 52 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yana mwelekeo wa kuvunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma, sheria nyingine za nchi yetu pamoja na misingi muhimu ya utawala bora kama ambavyo nitafafanua katika hatua zinazofuata. Naomba umma upuuze upotoshaji uliofanywa na Naibu Spika Job Ndugai kuhusu muongozo nilioomba mpaka pale maamuzi yatakapofanywa na Kamati ya Kanuni za Bunge kwa mujibu wa kifungu 5(5) na Bunge kujulishwa.

Wenu katika utumishi wa umma,

John Mnyika (Mb)
Bungeni-Dodoma
11/08/2011

Naibu Spika angempa fursa yakumalizia maelezo yake kama alivyo omba ili mwisho wa maelezo yake aweze kumuhukumu ila ndo hivyo kwakutumia kiti amehakikisha hatoi maelezo.
Pinda naona jicho limemtoka akaona ugali unamwagika!!!!

Serikali hii inawakati mgumu sana maana si wasafi hata kidogo. Kila wakati mwongozo kutoka kwa wapinzani unawapa kiwewe na hasira zisizo na msingi. MNALO NA LIMEWAGANDA.

Anaposimama mbunge wa cdm mwenyekiti anaanza kufikiria maneno ya kumwambia akae chini na alete hoja kwa maandishi

Naibu Spika angempa fursa yakumalizia maelezo yake kama alivyo omba ili mwisho wa maelezo yake aweze kumuhukumu ila ndo hivyo kwakutumia kiti amehakikisha hatoi maelezo.
Pinda naona jicho limemtoka akaona ugali unamwagika!!!!

Kwani hapo Naibu Spika amekosea nini.

Mimi naona amempa sasa nafasi nzuri sana kueleza hoja yake kwa kituo tena akishauriana na wenzake namna ya kuitoa mchicha.

Hakuna spika,au naibu wake atakayekubali kuona chama cha magamba kinafedheheshwa..hatuna imani nae huyo waziri mkuu. bei ya pamba imeshuka,angalia sukari ilivyopanda bei,angalia huku mafuta serikali ilivyoumbuka.hii ni kutokuwa na mpango mkakati.kwenye mambo ya msingi yanayoweza kuleta tija kwenye ardhi hii yetu.
Leo ikipigwa kura ya kutokuwa na imani na serikali mimi binafsi ntaipa ndiyo.nimechoka na ubabaishaji,na mizengwe.

Haahahahaah safi sana Naibu Spika! Kwanza apeleke hoja kwenye Kamati kuu ya Chadema kwa kutokuwa na Imani na mbowe baada ya kuidanganya kamati kuu kuwa kuna Mazungumzo ya Muafaka kati ya CDM na Waziri Mkuu!

Haahahahaah safi sana Naibu Spika! Kwanza apeleke hoja kwenye Kamati kuu ya Chadema kwa kutokuwa na Imani na mbowe baada ya kuidanganya kamati kuu kuwa kuna Mazungumzo ya Muafaka kati ya CDM na Waziri Mkuu!

Akili hizi kazi kwelikweli!

Haahahahaah safi sana Naibu Spika! Kwanza apeleke hoja kwenye Kamati kuu ya Chadema kwa kutokuwa na Imani na mbowe baada ya kuidanganya kamati kuu kuwa kuna Mazungumzo ya Muafaka kati ya CDM na Waziri Mkuu!

ndio maana unaitwa mlengo yaani ukiwekwa kwenye manati unaenda popote kulenga..pole sana mlengo ,
kuna mtu alishawahi kukueleza kuwa hana imani na waziri mkuu kivuli?

ametafsiri kanuni ndivyo sivyo.

Kuna haja sasa kwa kuwa maandamano yamemalizika CDM ikachukua muda kuwafundisha wabunge wake hasa hawa njuka, kanuni za bunge. Mbowe, Zitto na Slaa simamieni hii show.

Naibu Spika wa Bunge la Muungano Job Ndugai alibaki kidogo kuendelea kuchifau kama kiongozi wa bunge baada ya kukataa mwongozo wa Mbunge wa Ubungo bwana John Mnyiika, Mbunge huyo aliomba mwongozo wa kuibua hoja ya kutokuwa na imani na waziri Mkuu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mara ya kwanza Naibu Spika alionekana kumbuluza Mbumge huyo aliyeonekana kuwa na hoja muhimu sana kwa jamii,baada ya kipindi cha Maswali na majibu yanaongozwa na Waziri Mkuu Pinda leo hii,lakini aliikatisha hoja hiyo ya mbunge kuwa ilapaswa kuletwa mbele ya bunge kwa maandishi kwa mujibu wa vipengele na kanuni zilizotajwa za 153 na 133 ki kanuni na ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Niliyekuwa na fuatilia mjadala huo,nilijisikia vibaya sana jinsi Naibu Spika huyo alivyokatisha jambo hilo,kilichojili kichwani kwangu ni mwendelezo wa yaleyale ya chama mbele na serikali na si umma.

Lakini baada ya hotuba ya Waziri wa Habari na Utamaduni Emannuel John Nchimbi,Naibu Spika Job Ndugai aliamka na kutoa taarifa juu ya jambo la Mbunge wa Ubungo bwana John Mnyika na kuwa ni njia gani zifuatwe ili kuleta jambo hilo mbele ya bunge kwa njia sahihi na kanuni sahihi.

Akitoa muongozo huo Naibu Spika amesema jambo hilo la muhimu sana hivyo ichukuliwe kwa umuhimu huu huo huku akitoa njia gani zitumiwe ili kufikisha hoja hiyo mbele ya Bunge.Amesema bunge litapoke hoja hiyo ikiwa kwenye maandishi lakini ikiwa na sahihi za wabunge wenye idadi ipatayo asilimia 20% ya idadi ya wabunge wote walioko bungenii,ambao kwa jumla yao ni mia tanu na kitu,ili upate idadi hiyo mwongozo unasema itatakiwa kuwe na wabunge kuanzia 72,amabo ndio hao wanaunda asilimia 20%.

Wadau JF wanaojua kanuni na sheria za kuendesha bunge tusaidieni wengine tujue.Manake nilishajisikia kuchoka kabla lakini kwa maelezo ya Ndugai nimeona kama iko sawa na hivyo kuludisha hamaki yangu kuweza kupima ufafanuzi huo wa hoja na wazo na hoja ya mleta hoja.

Nawasilisha Wadau tusaidieni manake hoja hii ni muhimu..

Haahahahaah safi sana Naibu Spika! Kwanza apeleke hoja kwenye Kamati kuu ya Chadema kwa kutokuwa na Imani na mbowe baada ya kuidanganya kamati kuu kuwa kuna Mazungumzo ya Muafaka kati ya CDM na Waziri Mkuu!

ndio maana unaitwa mlengo yaani ukiwekwa kwenye manati unaenda popote kulenga..pole sana mlengo ,
kuna mtu alishawahi kukueleza kuwa hana imani na waziri mkuu kivuli?

ndio maana unaitwa mlengo yaani ukiwekwa kwenye manati unaenda popote kulenga..pole sana mlengo ,

kuna mtu alishawahi kukueleza kuwa hana imani na waziri mkuu kivuli?

Be careful na maneno yako itaku-cost Manati ni alama ya Chama fulani Cha Siasa hapa Nchini Tanzania chenye suara ya Jeshi la Mgambo!

Ndugai sio mwanasheria sijui amepata wapi utaalam wa kusema kuwa Mnyika katafsiri vibaya kanuni. Kuna aibu kubwa sana wanaishi nayo waongoza vikao vya bunge. Wanaongea kama vile Taifa na dunia nzima haiwaoni. Hata hivyo, kwa hayo machache aliyosema Mnyika nadhani ujumbe umefika, kwamba watanzania tumechoka na ubabishaji. Hii tactic ya kutaka ushahidi/maelezo kwa maandishi tunajua ni feki kama ambavyo ccm imekuwa feki maana hawajawahi kusoma aina yoyote ya ushahidi uliwasilishwa i.e Lema, Lissu na Zitto. Kwa sasa hivi tayari wananchi wameshasikia kidogo alichosema Mnyika na wanaanza kuongea (mafano hapa JF).

Haahahahaah safi sana Naibu Spika! Kwanza apeleke hoja kwenye Kamati kuu ya Chadema kwa kutokuwa na Imani na mbowe baada ya kuidanganya kamati kuu kuwa kuna Mazungumzo ya Muafaka kati ya CDM na Waziri Mkuu!

acha upumbavu wewe w/mkuu mwenyewe amekubali kuwa kuna kitu kama hiko kinaendelea,fuatilia vyombo vya habari siyo unakurupuka tu hata chai hujanywa na kuleta upupu wako hapa.watu wanajadili vitu vya msingi unaleta upupu wako.

Back
Top Bottom