Elections 2010 Mnyika apitishwa kwa 100% Ubungo, amtangaza Dr Slaa kuwa Shujaa

Serayamajimbo

Senior Member
Apr 15, 2009
191
38
MGOMBEA wa Ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. John Mnyika amepitishwa na na chama chake kugombea jimbo hilo kwa asilima 100.
Bw. Mnyika alipitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa jimbo hilo baada ya wajumbe wote 62 kumpa kura ya ndiyo.
Wajumnbe waliohudhuria katika mkutano huo ni Wenyeviti na makatibu wote wa jimbo hilo, wageni waalikwa 60 na wawakilishi wa vyuo vikuu walioko Ubungo na wawakilishi wa matawi ya CHADEMA katika jimbo hilo.

Wakati huo huo, Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limemtaja, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa kuwa shujaa baada ya kukubalia maombi ya Kamati Kuu ya kugombea urais wakati baado alikuwa anahitajika katika jimbo lake.
Akizungumza katika mkutano wa wakilishi wa vyuo vikuu Mweyekiti wa Kamati ya baraza hilo, Bw. John Mnyika alisema kitendo alichofanya Dkt. Slaa cha kuachia jimbo ambalo alikuwa na uhakika wa kushinda katika Uchaguzi Mkuu ni la kishujaa.
"Tunakutana leo kwa kuwa tendo alilofanya Mtanzania mwenzetu, Dkt. Slaa kukubali kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni la kishujaa," alisema Bw. Mnyika
Alisema Dkt. Slaa ni sawa mashujaa waliokubali kupoteza maisha yao na kulilinda na kuliteta taifa na hivyo ni shujaa wa demokarsia na maendeleo.
Alisema mashujaa wa namna ya Dkt. Slaa hawafii kwa kuwa fikra zao zitakumbukwa milele uamuzi wa huo utandika historia mpya kwa taifa ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo misingi ya CHADEMA
Alisema Bendera ya chama hicho ni rangi ya nyekundu, nyeupe bluu, bahari na nyeusi uwepo kwa rangi nyekundu unatoka na kuthamini mashujaa wa nchi walipigana vita ili kulikomboa taifa hili.
Alisema maadhimisho yanayofanywa na serikali Julai 25 kila mwaka kuwakumbuka mashujaa ni unafiki kwa kuwa hufanywa kwa maneno na si wa kivitendo
Alisema tunu ya taifa hili ziko kwenye ngao ya taifa ambayo ni Uhuru na Umoja lakini uhuru umetoweka na nchi imekuwa tegemezi kwa kuwa sehemu kubwa ya rasilimli zake zimeuzwa kwa bei ya kutupwa kwa wageni na sehenu kubwa ya Watanzania hawafaidi nayo
Alisema umoja umetelemshwa kutokana na kupuuzwa utawala wa sheria kumea kwa ubaguzi na kupanuka kwa matabaka katika jimii kwenye sekta mbalimbali za afya, elimu na hata mifumo ya haki hali ambayo ni tishio la ustawi na usalama wa nchi.
Alisema Dkt. Slaa ametimiza wajibu huo kwa kusimamia ukweli, uwazi, uadilifu na amani kama rangi nyeupe katika bendera ya CHADEMA inayowakilishwa hususani kupitia ngazi ya ubungeni katika jamii na jimboni kwake karatu
Bw Mnyika alisema umefika wakati wa Dkt. Slaa kuinuliwa na kupewa wajibu mkuu zaidi katika nchi wa ili kuunda serikali na kusimamia utekelezaji ilikurudisha nchi kwa wananchi.

Source: Mnyika apitishwa kwa 100% Ubungo
 
Hongera sana bw Mnyika, kuwa makini usipigwe tena changa la macho hapo kwa wajanja...
 
Bw. John Mnyika alisema kitendo alichofanya Dkt. Slaa cha kuachia jimbo ambalo alikuwa na uhakika wa kushinda katika Uchaguzi Mkuu ni la kishujaa.

Alisema Dkt. Slaa ni sawa mashujaa waliokubali kupoteza maisha yao na kulilinda na kuliteta taifa na hivyo ni shujaa wa demokarsia na maendeleo.

Alisema mashujaa wa namna ya Dkt. Slaa hawafii kwa kuwa fikra zao zitakumbukwa milele uamuzi wa huo utandika historia mpya kwa taifa ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo misingi ya CHADEMA

Duh...yaaan ata Mnyika haamini kuwa Dr Slaa anaweza kumshinda Kikwete mwaka huu?kaaazi kwelikweli!!
 
Debe tupu hilo! hana uwezo wowote wa kuwakilisha ubungo...ubungo kuna vichwa si hilo debe tupu

I'm now doubting your objectivity since you seem to hate everything Chadema. Anyway ni vichwa gani hao unaowajua ili na sisi tuwa fahamu na kuwa pima?
 
Go mnyika go its our time now achana na wasotaka kukuelewa waloamua kufumba macho ili wasiuone ukweli. Keep going you will make it!
 
Of course kila mwenye akili timamu hawezi kukubali wabaguzi wa kidini na kikabila ...tht is chadema..with their priest! kwa faida ya Taifa. wenye vichwa watatangazwa na tume ya uchaguzi vuta subira..hilo debe tupu nimeshalisikiliza miaka ya nyuma kwenye campaign zake ...hakuna kitu..however, ana akili sana kwa viwango vya chadema as long as anatoka kanisani period!
Ni walewale tu yaani huachi kuangalia kwa kutumia UDINI, bado narudia umekuwa oriented na elimu yako ya utotoni ndo maana waangalia DINI tu!
 
Of course kila mwenye akili timamu hawezi kukubali wabaguzi wa kidini na kikabila ...tht is chadema..with their priest! kwa faida ya Taifa. wenye vichwa watatangazwa na tume ya uchaguzi vuta subira..hilo debe tupu nimeshalisikiliza miaka ya nyuma kwenye campaign zake ...hakuna kitu..however, ana akili sana kwa viwango vya chadema as long as anatoka kanisani period!

Do you have problem with priests? By the way kusema wagombea vichwa wata tangazwa na tume ya uchaguzi ni unasema kwamba tume ya uchaguzi ndiyo ina halalisha na kichwa au nani siyo kichwa au una maanisha Tanzania tuna mfumi wa kisiasa na wa kijamii uliyo kamili sana kiasi kwamba kigezo pekee cha mtu kushinda ni kuwa kichwa au la? Maana kuna wanaoshindwa kwa rushwa nk na wana tangazwa na tume....je wao ni vichwa? Na pia huyo "padre" unayempinga kuwa hawezi kuwa raisi na yeye ni mbunge aliye tangazwa na tume ya uchaguzi kwa hiyo je mkuu ni sawa niki chukulia kwamba unamkubali Mh. Slaa ni kichwa?
 
Tumain anahaha sasa hivi kwenye JF akihama thread hadi thread kumtukana Slaa.

Wenye akili zao sasa hivi wameshaacha kumjibu.

Acheni kupoteza muda na umeme/nguvu zenu kumjibu.

Hata Malaria Sugu jana alimuonya ila jamaa ngangari.

Usibishane na ....... watu hawataona tofauti.

Kila mkisoma ujumbe wa Tumain, mumhurumie Masikini wa watu. Sijui kalipwa au anafanya kazi ya bure?
 
Debe tupu hilo! hana uwezo wowote wa kuwakilisha ubungo...ubungo kuna vichwa si hilo debe tupu

" Fear and Surrender are not the options for me" it does not sound like it comes from your heart! it looks like itis ctrl + P, ctrl+ v. no wonder unajiita tumain! endelea kuwatumain hao unaowatumaini labda miaka mingine 50 wataleta maendeleo, miaka 50 tuliyowapa wametuzalishia mafisadi tu! Na sasa wanasema wanakuja kwa kasi zaidi! Mwaka huu hawachomoki!
 
kijana anastahili hiyo heshima aliyopewa,hakika hili jimbo ni lake kama uchaguzi ukiwa free n fair binafsi siami kama LAST TIME alishindwa kihali!Ila wote wenye nia njema tuamua kwa busara hatma ya nchi yetu tuachana na hawa wenye hoja zisizo na mashiko za udini tujipange kupoka madaraka kistaarabu kwa NGUVU YA UMMA,mnyika aluta cntnue mpaka kieleke hapo ubungo oct.
 
Butola hebu acha uvivu Hotuba ya Mnnyika ipo sasa kwa nini unakariri Magazeti?

Hapo Mnnyika alikuwa anawakosoa wale wote wenye Fikra kama zako kwamba kwa kuwania Urais basi Amejiua Kisiasa

Tunakutana leo kwa sababu ya tendo la kishujaa la mtanzania mwenzetu Dr Wilbroad
Slaa kukubali ombi la kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tendo
hili la kishujaa la kuachia jimbo la uchaguzi ambalo alikuwa ana uhakika wa
kuletetea na badala yake kugombea nafasi ya urais ambayo baadhi ya watu
wametafsiri kama ni 'kuuawa ama kujiua' kisiasa.

Hapa Chini Mnyika anazidi kupiga Nondo

Maneno yoyote ya kupingana mwelekeo huu wenye kutanguliza taifa kwanza iwe ni
kwa nia njema inayosukumwa na hofu ya ombwe la Dr Slaa bungeni au mashaka ya
pengo lake Karatu ama dhamira mbaya ya wapambe wa Kikwete za kuhadaa nafsi za
watanzania yanapaswa yapingwe kwa matendo ya wote wenye kuitakia mema nchi yetu
kwa kumuunga mkono Dr Slaa kwa hali na mali

Na hapa anamaliza kabisa

Ni falsafa hii hii ndio tutakayotumia kuwezesha ushindi wa Dr Slaa na ushindi wa
wabunge na madiwani mbadala kwa vijana kuwa mstari wa mbele kugombea ama kuunga
mkono wagombea ikiwemo kutafuta na kulinda kura kwa kupitia pia falsafa ya
Baraza la Vijana wa CHADEMA(BAVICHA) kwamba: Vijana; Nguvu ya Mabadiliko.
Serikali yenye woga wa mabadiliko inayotawala kwa hujuma imetoa waraka na
kuziingilia ratiba za vyuo husasani vya umma na kufanya vifunguliwe baada ya
uchaguzi kwa hoja kanyaboya na hivyo kukwamisha baadhi yenu kupata haki ya
msingi ya kikatiba ya raia ya kupiga kura pamoja na kuwa mlishajiandikisha
tayari.
 
Of course kila mwenye akili timamu hawezi kukubali wabaguzi wa kidini na kikabila ...tht is chadema..with their priest! kwa faida ya Taifa. wenye vichwa watatangazwa na tume ya uchaguzi vuta subira..hilo debe tupu nimeshalisikiliza miaka ya nyuma kwenye campaign zake ...hakuna kitu..however, ana akili sana kwa viwango vya chadema as long as anatoka kanisani period!
Mkuu wangu hakikisha unaweza kuyakoga maji haya..Ni fikra kama hizi zinazowafanya nchi za kiarabu kuendelea kuibiwa uchumi wao wakilinda dini badala ya ardhi, matokeo yake wote wamemezwa na dini inapotea ktk matendo yao walichobakia nacho ni imani tu..Dini inalindwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe kwani ni swala la imani na sii binadamu walioileta wala kutakiwa kuilinda imani iliyosetirika ktk mioyo ya watu..

Hivyo jaribu sana kutofautisha siasa na Dini. Dr.Slaa anaweza kuwa Padre lakini kwa nia na dhamira yake ni mbora zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko huwa wanaothaminisha haramu zote. Uislaam sio jina la mtu wala elimu ya mtu isipokuwa ni imani inayofuatiwa na Ibada. Sii Mwinyi wala JK wanafuata mafundisho ya dini zaidi ya majina yao..Na hakika hakuna Waislaam din - Bongo, ni unafiki mtupu..
 
Mkuu wangu hakikisha unaweza kuyakoga maji haya..Ni fikra kama hizi zinazowafanya nchi za kiarabu kuendelea kuibiwa uchumi wao wakilinda dini badala ya ardhi, matokeo yake wote wamemezwa na dini inapotea ktk matendo yao walichobakia nacho ni imani tu..Hivyo jaribu sana kutofautisha siasa na Dini. Dr.Slaa anaweza kuwa Padre lakini kwa nia na dhamira yake ni mbora zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko huwa wanaothaminisha haramu zote. Uislaam sio jina la mtu wala elimu ya mtu isipokuwa ni imani inayofuatiwa na Ibada. Sii Mwinyi wala JK wanafuata mafundisho ya dini zaidi ya majina yao..Na hakika hakuna Waislaam din - Bongo, ni unafiki mtupu..

Mkuu Safi sana kwa Maneno yako yenye Busara Tele, tuwaache hawa wanaopiga kampeni za kidini! Hazina Nafasi
 
dini- tena imeingiaje kweye siasa? Hawajapata urais wameanza udini wakipata itakuwaje? Afghanstan jamani!!
 
Of course kila mwenye akili timamu hawezi kukubali wabaguzi wa kidini na kikabila ...tht is chadema..with their priest! kwa faida ya Taifa. wenye vichwa watatangazwa na tume ya uchaguzi vuta subira..hilo debe tupu nimeshalisikiliza miaka ya nyuma kwenye campaign zake ...hakuna kitu..however, ana akili sana kwa viwango vya chadema as long as anatoka kanisani period!

All is good but what I seeing is no sense message from another suppoter of left wing politician!

Kama udini basi CCM ndiye namba one maana mgombea wa Urais TZ ni Mwislam,Makamu wake ni Mwislam,mgombea wao Urais ZNZ ni mwislam!Tumaini iweje umeweza kuona kibanzi kwenye"macho"ya CHADEMA lkn ukashindwa kuona boriti kwenye"macho"ya CCM?Cheapest ever CCM propagandist indeed!
 
.. kwa asilima 100.

Tunaopeda demokrasia ya kweli tukiona mtu anashinda 100% tunashtuka, tunasikitika. Binadamu, na zaidi wanasiasa, wana shabaha na matamanio ya uongozi. Kundi la wanasiasa linapokutana na wote kukubaliana kitu 100%, inawezekana kuna wengine hawaruhusiwi kufikiri au wameoshwa ubongo.


... Dkt. Willibrod Slaa kuwa shujaa baada ya kukubalia maombi ya Kamati Kuu ya kugombea urais
Kwa nini mpaka Kamati ndio iteue? Kwa nini kila mwananchi mwenye kadi ya CHADEMA asiwe na uwezo wa kusimama peke yake, kivyake, asema "nataka kugombea urais" halafu wapigiwe kura?

Utakuwaje na mgombea urais ambae yeye mwenyewe hakuomba, hakutaka, hakunyoosha mkono juu kusema "nataka kuwa rais", ameteuliwa?

 
Back
Top Bottom