Mnyika amkaanga Waziri Ngeleja kuhusu umeme

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,554
47
Mnyika amkaanga Waziri Ngeleja kuhusu umeme Send to a friend
mnyikanow.jpg
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika

Boniface Meena
MBUNGE wa Ubungo (Chadema), John Mnyika amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja atoe maelezo ya kina kuhusu hatua ambayo serikali inataka kuchukua ya kukodi mitambo ya kuzalisha megawati za umeme 260 ili kuziba pengo la takribani megawati 240 ambalo linakabili taifa kwa sasa.

Mnyika alieleza hayo jana akimtaka waziri Ngeleja atoe ufafanuzi wa kutokukamilika kwa mipango ya serikali wakati ambapo dharura ya umeme ilijulikana toka mwaka 2002, serikali ikaijadili kwa kina mwaka 2006, bunge likapitisha maazimio mwaka 2008 na serikali ikaahidi tena mwaka 2009 kuweka utaratibu wa kukabiliana na dharura hiyo.

"Ni muhimu kwa Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo ya kina kuhusu hatua ambayo serikali inataka kuchukua ya kukodi mitambo ya MW 260. Aidha, Waziri atoe ufafanuzi wa kutokukamilika kwa mipango ya serikali,"alisema Mnyika.

Alisema katika muktadha huo ni muhimu kwa bunge likapata fursa ya kujadili kwa kina suala la umeme katika mkutano unaoendelea wa bunge kama jambo la dharura ili kuweza kulinusuru taifa.

Hata hivyo tayari Spika wa Bunge, Anne Makinda ameishatoa msimamo kwamba suala la uhaba wa umeme halitajadiliwa na katika kikao cha bunge kinachoendelea mjini Dodoma na badala yake ameiagiza Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge kuliofanyia kazi suala hilo.

Spika alitoa msimamo huo juzi kufuatia hoja ya dharura ya Mnyika aliyetaka bunge kujadidi suala la umeme mara baada ya Ngeleja kutoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu suala hilo.

Katika maeleo yake bungeni, Ngeleja alitaja orodha ndefu ya miradi ya serikali inayotarajiwa kukamilika katika muda wa kati ya miaka miwili hadi sita, huku akibainisha kuwa ili kulikabili tatizo la sasa kuna mpango wa kukodi mitambo ya kuzalisha megawati 260 za umeme ili kufidia pengo lililopo hivi sasa.

Jana katika taarifa yake, Mnyika alisema ikumbukwe kwamba kampuni ya Dowans ilirithi mkataba toka kampuni ya Richmond ambayo ilithibitishwa kwa maazimio ya bunge kuwa ilipata mkataba katika mazingira ya ukiukwaji wa sheria ikiwemo sheria ya kupambana na rushwa.

Alisema suala zima likitazamwa kwa undani wake yakirejewa yaliyojiri Costa Rica na Tanzania, hata kampuni Dowans kuna utata kuhusu usajili, umiliki na jinsi ilivyorithi mkataba wa kuzalisha umeme kutoka Richmond.

"Kampuni ya Dowans kama inataka kuepusha kutaifishwa basi wamiliki wake popote pale walipo duniani wajitokeze hadharani wakiri kwamba walipotoshwa na Richmond pamoja na vyombo vya kiserikali wakati wa kuhamishwa mkataba, ili wajijengee uhalali wa kufanya majadiliano ikiwemo ya kufuta madai ya fidia inayotaka kutolewa kwa mujibu wa hukumu ya ICC,"alisema Mnyika.

Alisema mtazamo wake ni kwamba ili kupunguza adha ya mgawo wa umeme serikali itumie mamlaka yaliyopo kwenye katiba na sheria ikiwemo sheria ya uhujumu uchumi, sheria ya kupambana na rushwa, sheria ya mali zilizopatikana isivyo halali itaifishe mitambo hiyo haraka iwezekanavyo na kuiwasha kwa maslahi ya umma.

"Nitatoa tamko la kina hivi karibuni kwa nafasi yangu ya uwaziri kivuli kuhusu suala la umeme kwa kuzingatia hali ya mgawo inavyoendelea sanjari na kupanda kwa gharama za nishati hiyo, kunakoongeza ugumu wa maisha kwa Watanzania walio wengi baada ya majadiliano na baraza kivuli na mamlaka nyingine husika,"alisema.

Juzi mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Dowans iliyoibua mjadala mpana katika jamii kutokana na utata wa mkataba wake, ilitangazwa huenda ikawashwa wakati wowote kwa malengo ya kupunguza tatizo la mgawo wa umeme linaloendelea nchini.

Habari zilizopatikana juzi mjini Dodoma na kuthibitishwa na baadhi ya wabunge waliohudhuria kikao cha Kamati ya Nishati na Madini zilieleza kuwa hoja ya kuwashwa kwa mitambo hiyo ilijadiliwa kwa lengo la kupunguza makali ya umeme nchini.

Chanzo chetu cha habari kilisema kwamba wajumbe wa kamati hiyo walikuwa wakijadili ama waitaifishe mitambo hiyo au waingie mkataba wa dharura ili ianze kutoa umeme kwa siku mbili zijazo.

"Suala lililozua mvutano baina ya wabunge ni ama kutaifisha au kuwapo mkataba wa dharura na kampuni inayomiliki mitambo hiyo,"alisema mbunge mmoja aliyekuwapo katika kikao cha kamati hiyo.

Vyanzo hivyo vya habari vilieleza Mwananchi kuwa mpaka juzi usiku kikao kilikuwa kikielendea na kwamba baada ya kumaliza kikao hicho wangeshauriana na Spika wa Bunge kueleza msimamo wao.

Alipoulizwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, January Makamba kilichokuwa kikijadiliwa ndani ya kikao, alisema : " Kikao bado kinaendelea. Tutashauriana na Spika baada ya hapa. Tunatarajia kufanya uamuzi wenye maslahi ya kwa nchi nzima."

Awali jana asubuhi wakizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 , Makamba, Mnyika alipendekeza ufanyike uamuzi mgumu ili kuwezesha mitambo ya Dowans kuwashwa ili kupunguza makali ya mgao.

Kwa mujibu wa Makamba, mitambo ya Dowans inazalisha MW 120 na inaweza kusaidia kupunguza makali ya mgao kwa asilimia 60 mpaka 70. Wote walitambua uwepo wa suala la Dowans mahakamani.

Hata hivyo, Mnyika alipendekeza sheria ya uhujumu uchumi itumike katka suala la Dowans huku akisema kuwa hawezi kwenda ndani zaidi.

Mnyika alimaanisha kuwa mitambo ya Dowans inapaswa kutaifishwa kwa sababu ya ukweli kuwa mkataba wa Dowans/Richmond ni wa kitapeli na huwezi kuwa na mgawo wakati mitambo iko pale imezimwa.

Wakati huo huo, Makamba alipendekeza kuwa usainiwe mkataba wa muda mfupi wa miezi mitatu na hao wenye mitambo ili kuiwezeshwa kuwashwa.
 
Hivi huyo Anna Makinda anaelewa vizuri maana ya BUNGE??
Ni kwanini wambunge watake kuleta hoja bungeni halafu spika akatae????
nini kimejificha hapo?
ni lazima kuna jamabo ndani ya pazia
 
Easy swala hili halitajadiliwa bungeni maana CCM hakina uhakika kama wabunge wake wote wanaweza kuafiki kusaini mkataba sasa imebuniwa njia ya kutumia kamati ambayo itapeleka mapendekezo ya kusaini makataba mfupi na the so called kampuni feki kwa mara ya pili tena na spika atakuwa hana ujanja zaidi ya kukubali.

Anna Makinda = January makamba= Rostam Aziz

Yaani spika na january wamepewa meno na RA so they will not let him down.
 
Mnyika amkaanga Waziri Ngeleja kuhusu umeme Send to a friend
mnyikanow.jpg
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika

Boniface Meena
MBUNGE wa Ubungo (Chadema), John Mnyika amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja atoe maelezo ya kina kuhusu hatua ambayo serikali inataka kuchukua ya kukodi mitambo ya kuzalisha megawati za umeme 260 ili kuziba pengo la takribani megawati 240 ambalo linakabili taifa kwa sasa.

Mnyika alieleza hayo jana akimtaka waziri Ngeleja atoe ufafanuzi wa kutokukamilika kwa mipango ya serikali wakati ambapo dharura ya umeme ilijulikana toka mwaka 2002, serikali ikaijadili kwa kina mwaka 2006, bunge likapitisha maazimio mwaka 2008 na serikali ikaahidi tena mwaka 2009 kuweka utaratibu wa kukabiliana na dharura hiyo.

"Ni muhimu kwa Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo ya kina kuhusu hatua ambayo serikali inataka kuchukua ya kukodi mitambo ya MW 260. Aidha, Waziri atoe ufafanuzi wa kutokukamilika kwa mipango ya serikali,"alisema Mnyika.

Alisema katika muktadha huo ni muhimu kwa bunge likapata fursa ya kujadili kwa kina suala la umeme katika mkutano unaoendelea wa bunge kama jambo la dharura ili kuweza kulinusuru taifa.

Hata hivyo tayari Spika wa Bunge, Anne Makinda ameishatoa msimamo kwamba suala la uhaba wa umeme halitajadiliwa na katika kikao cha bunge kinachoendelea mjini Dodoma na badala yake ameiagiza Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge kuliofanyia kazi suala hilo.

Spika alitoa msimamo huo juzi kufuatia hoja ya dharura ya Mnyika aliyetaka bunge kujadidi suala la umeme mara baada ya Ngeleja kutoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu suala hilo.

Katika maeleo yake bungeni, Ngeleja alitaja orodha ndefu ya miradi ya serikali inayotarajiwa kukamilika katika muda wa kati ya miaka miwili hadi sita, huku akibainisha kuwa ili kulikabili tatizo la sasa kuna mpango wa kukodi mitambo ya kuzalisha megawati 260 za umeme ili kufidia pengo lililopo hivi sasa.

Jana katika taarifa yake, Mnyika alisema ikumbukwe kwamba kampuni ya Dowans ilirithi mkataba toka kampuni ya Richmond ambayo ilithibitishwa kwa maazimio ya bunge kuwa ilipata mkataba katika mazingira ya ukiukwaji wa sheria ikiwemo sheria ya kupambana na rushwa.

Alisema suala zima likitazamwa kwa undani wake yakirejewa yaliyojiri Costa Rica na Tanzania, hata kampuni Dowans kuna utata kuhusu usajili, umiliki na jinsi ilivyorithi mkataba wa kuzalisha umeme kutoka Richmond.

"Kampuni ya Dowans kama inataka kuepusha kutaifishwa basi wamiliki wake popote pale walipo duniani wajitokeze hadharani wakiri kwamba walipotoshwa na Richmond pamoja na vyombo vya kiserikali wakati wa kuhamishwa mkataba, ili wajijengee uhalali wa kufanya majadiliano ikiwemo ya kufuta madai ya fidia inayotaka kutolewa kwa mujibu wa hukumu ya ICC,"alisema Mnyika.

Alisema mtazamo wake ni kwamba ili kupunguza adha ya mgawo wa umeme serikali itumie mamlaka yaliyopo kwenye katiba na sheria ikiwemo sheria ya uhujumu uchumi, sheria ya kupambana na rushwa, sheria ya mali zilizopatikana isivyo halali itaifishe mitambo hiyo haraka iwezekanavyo na kuiwasha kwa maslahi ya umma.

"Nitatoa tamko la kina hivi karibuni kwa nafasi yangu ya uwaziri kivuli kuhusu suala la umeme kwa kuzingatia hali ya mgawo inavyoendelea sanjari na kupanda kwa gharama za nishati hiyo, kunakoongeza ugumu wa maisha kwa Watanzania walio wengi baada ya majadiliano na baraza kivuli na mamlaka nyingine husika,"alisema.

Juzi mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Dowans iliyoibua mjadala mpana katika jamii kutokana na utata wa mkataba wake, ilitangazwa huenda ikawashwa wakati wowote kwa malengo ya kupunguza tatizo la mgawo wa umeme linaloendelea nchini.

Habari zilizopatikana juzi mjini Dodoma na kuthibitishwa na baadhi ya wabunge waliohudhuria kikao cha Kamati ya Nishati na Madini zilieleza kuwa hoja ya kuwashwa kwa mitambo hiyo ilijadiliwa kwa lengo la kupunguza makali ya umeme nchini.

Chanzo chetu cha habari kilisema kwamba wajumbe wa kamati hiyo walikuwa wakijadili ama waitaifishe mitambo hiyo au waingie mkataba wa dharura ili ianze kutoa umeme kwa siku mbili zijazo.

"Suala lililozua mvutano baina ya wabunge ni ama kutaifisha au kuwapo mkataba wa dharura na kampuni inayomiliki mitambo hiyo,"alisema mbunge mmoja aliyekuwapo katika kikao cha kamati hiyo.

Vyanzo hivyo vya habari vilieleza Mwananchi kuwa mpaka juzi usiku kikao kilikuwa kikielendea na kwamba baada ya kumaliza kikao hicho wangeshauriana na Spika wa Bunge kueleza msimamo wao.

Alipoulizwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, January Makamba kilichokuwa kikijadiliwa ndani ya kikao, alisema : " Kikao bado kinaendelea. Tutashauriana na Spika baada ya hapa. Tunatarajia kufanya uamuzi wenye maslahi ya kwa nchi nzima."

Awali jana asubuhi wakizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 , Makamba, Mnyika alipendekeza ufanyike uamuzi mgumu ili kuwezesha mitambo ya Dowans kuwashwa ili kupunguza makali ya mgao.

Kwa mujibu wa Makamba, mitambo ya Dowans inazalisha MW 120 na inaweza kusaidia kupunguza makali ya mgao kwa asilimia 60 mpaka 70. Wote walitambua uwepo wa suala la Dowans mahakamani.

Hata hivyo, Mnyika alipendekeza sheria ya uhujumu uchumi itumike katka suala la Dowans huku akisema kuwa hawezi kwenda ndani zaidi.

Mnyika alimaanisha kuwa mitambo ya Dowans inapaswa kutaifishwa kwa sababu ya ukweli kuwa mkataba wa Dowans/Richmond ni wa kitapeli na huwezi kuwa na mgawo wakati mitambo iko pale imezimwa.

Wakati huo huo, Makamba alipendekeza kuwa usainiwe mkataba wa muda mfupi wa miezi mitatu na hao wenye mitambo ili kuiwezeshwa kuwashwa.

What is the source of this news, paper's name?
 
Mi ningekuwa na uwezo ningehama nchi, make nchi imeparaganyika kama vile hatuna mwelekeo
 
Well suala la ufadhili wa RA kwa CCM linajulikana. Fedha alikuwa anatoa wapi ndo swali la msingi la kujiuliza. RA siyo mbaya kiasi hicho watu wanavyofikiria kwani yeye ni njia tu ya kupitisha huo ulaji. Tumewapa nguvu za kisiasa na kiuchumi wanyonyaji wetu - CCM hivyo acha tukae gizani, acha generali Simbo aendelee kutuua kwa mabomu n.k
 
Sasa kwa mara ya kwanza tz hatuna mhimili wa bunge kwani spika wa bunge badala ya kusimamia taratibu za bnge ameligeuza kuwa sehemu ya kutumia ubabe wake kwa maslahi ya mafisadi......
Kwa nini wat tumelalal kiuasi hiki?
 
anne makinda ........................... anne makinda............................anne makinda ............................... jamani .. tujadiliane - tumchukulie hatua gani??? kumzomea haitoshi............how do we do with this "KIBARAKA" wa mafisadi??? Great thinkers - come out with a plan, suggestion please
la sivyo ATATUMALIZA HUYU MAMA
 
N abado, wanahakikisha kuwa wakati wanatoka walishakamua kila kitu
 
That is another buznez mkuu,
huo ni ulaji tu wa wajanja, wameona kuwa watz wamekuwa ni welevu sana wa mambo hivyo inabidi tucheze tukijua kuwa wale wanaona sio vipofu kama zamani.
Sasa watamtumia huyo Mkamba kumaliza kila kitu.
Wanajua ni moto mklai kama wakilileta bungeni

Back
Top Bottom