Mnyika amjia Kikwete na Ikulu yake

Serayamajimbo

Senior Member
Apr 15, 2009
191
38
Mnyika amemjia juu Rais Kikwete na ikulu kuwa ndio chanzo cha mapungufu yote katika serikali. Akichangia bajeti ya hotuba ya ofisi ya rais amesema katiba imempa mamlaka makubwa na watumishi wote wengine wanafanya kazi kwa niaba yake hivyo wanapoharibu wa kuwajibika ni yeye.Mnyika amesema kuwa Rais amelidanganya taifa kuhusu mgawo wa umeme kwa kwa aliahidi mwezi aprili kuwa mwezi julai mitambo ya umeme ya MW 260 ingekuwa imeanza kazi.Amesema Rais anapaswa kuondoa ikulu wote wanaompa ushauri mbaya, pia amerudia tena kauli ya kuwataka Ngeleja na Malima wajiuzulu.Mnyika ametaka bilioni 135 ambazo bunge limejulishwa kuwa zitatumika na Ofisi ya rais kwa ajili ya matumizi ya kitaifa bila matumizi hayo kuelezwa kwa wabunge wala kuweka kwenye vitabu zifafanuliwe.Amesema kwamba fedha hizo ndizo zinazotumiwa na ikulu kufanya matumizi ya anasa ikiwemo safari nyingi za nje.Ameilipua pia ofisi ya rais kwa ufisadi uliofanyika wa malipo ya bilioni 3 kwa kampuni ya Twiga Chemicals kinyume na maamuzi na kutaka TAKUKURU na usalama wa taifa kuchukua hatua ikiwemo kuhusu rushwa katika miradi ya maji na ardhi jimboni Ubungo.Amekosoa mfumo wa bajeti ya Tanzania ambapo wabunge wanapewa vitabu vyenye kurasa chache vikiwa havielezi kwa undani matumizi ya ofisi ikiwemo ya Rais; na kuonyesha likitabu likubwa sana la bajeti ya Zambia.
 
I wish I were able to clone them and get 50 HE John Mnyikas, 100 HE Tundu Lissu, 50 HE Freeman Mbowe and be MPs tol currently CCM-led constituency.
 
Mmmmmh, nikiangalia njia tunayoendea tanzania Sasa hivi ni nzuri, kwani miaka michache iliyopita hivi vitu vilikuwa havitamkwi hadharani, na kwa mwendo huu Wtz, kufunguka katika kujua Hakizetu, na wajibu mbalimbali wa viongozi, ili tujue jinsi ya kuwawajibisha, Keep it up, Mnyika
 
Acha vijana wajijengee ujasili wa kumsema rais hadharani baada ya hapo kitakachofuata ni kumtaka aondoke kabisa ikulu, ni kweli hata roma haikujengwa kwa siku moja.Kwa sasa vijana wana fanya mazoezi ya kufumua siri za kifisadi za ikulu lakini itafika mahala rais atatakiwa kuthibitisha.Kazi ipo
 
Mara zote akisimama mbunge wa upinzani hua najisikia raha sana na kama nipo bar utaona watu wote kimya wanasikiliza kwa makini. akipanda wa ccm utaona watu wanaendelea na shughuli zao. ki ukweli wananchi wamechoshwa na CCM
 
Mnyika leo ametufungua macho yaani bajeti ya ikulu inawekwa bila vipendele ili isjulikane anatumia kiasi gani Raisi wetu kujinoma jamani nchi hii inaliwa kwelikweli
 
Naamini wananchi wanagundua kuwa ni nani anawakilisha wananchi na nani anawasaliti wananchi bungeni. Kwenye kura watafanya kweli na matokeo yakichakachuliwa hasira njema za wananchi zitaendelea vizazi kwa vizazi alafu ndo hapo extra constitution actions zitaanza rasmi.
 
I wish I were able to clone them and get 50 HE John Mnyikas, 100 HE Tundu Lissu, 50 HE Freeman Mbowe and be MPs tol currently CCM-led constituency.
tanga kwenu, umesahau Dr. Slaa, G. Lema na H. Mdee!Otherwise you've cheered my heart.
 
Back
Top Bottom