Mnyika Akalia Kuti Kavu

nawashangaa sana wana jf ni kwamba chemva auwezi yeye kuiba au kufanya njama za wizi? Mnyika siyo mjinga kuzungumza haya kwenye bunge na akiwa hana ushahidi swala hapa ni sisi kusubiri mnyika alete data na mambo yawe wazi ijulikane nchemba aliihusika vp na wizi wa pesa za epa,
 
Jembe JJ namuamini hawezi kutoa maneno bila ushahidi, nina uhakika ana kitu ambacho kakishika km ushahidi, we subiri uone, nashauri ushahidi uwekwe wazi wasifichwe.

Mhhhhh kazi kweli kweli kusoma hujui hata picha huoni mkuu

Badilikeni vijana wa Kitanzania Mnyika kiukweli kageuka muuza sura ni bora tu atoe single iwe inapigwa kwa Tv watu wamuone ila kiukweli dogo sasa kazidi kukurupuka
 
Huyu jamaa hana adabu ,tunaweza kusema ni mtovu wa nidhamu ,tokea siku ile alivyomwita Raisi kikwete dhaifu na wengine wazembe na juzi akawaita watu machizi nilimuonea huruma sana maana amekosa uadilifu na hana ujuzi wa kuzungumza kwa ufupi hana tofauti na vijana wa vijiweni au wazee wa migahawani.

Vipi utamwita Raisi wa nchi dhaifu tena kwa jina na wengine uwaite wazembe au machizi ndani ya kikao cha bunge ,yaani huyu jamaa anavyosema ni sawa na kelele za jibwa koko tena yule asie na kwao ,anabweka tu utafikiri amekoswakoswa na jiwe.

Kuna haja ya wenziwe kumshauri na asifikirie watu wote wanamtakia wema hata wenziwe wanaweza kuwa na choyo nae na kumwacha akizama katika ujinga.
 
nawashangaa sana wana jf ni kwamba chemva auwezi yeye kuiba au kufanya njama za wizi? Mnyika siyo mjinga kuzungumza haya kwenye bunge na akiwa hana ushahidi swala hapa ni sisi kusubiri mnyika alete data na mambo yawe wazi ijulikane nchemba aliihusika vp na wizi wa pesa za epa,

Uko sawa kabisa mkuu tusubiri ushahidi uletwe kisha tuuchambue kama una ukweli ama laa ili tuweze kufahamu kama Mnyika kageuka muuza sura bungeni kwa kupenda kuonekana kwa Tv ama kweli anauthibitisho Nchemba aliiba fedha za EPA
 
Mnyika ni mtu mzima anae jitambua na ww sijui huruma zako kwake umezitoa wapi na sidhani kama alikuomba Masada.
Unadhani mpaka anazungumza alikua ajitambui! ? Alijua ataambiwa adhibitishe ndo mana akaamua aseme ili akidhibitisha tuzidi kuwafahamu wanafiki wetu .

ACHA KUKURUPUKA WEWE
 
Mnyika nilikushauri tulizana usipende kuropoka hovyo angalia sasa umeingia kichwa kichwa kwenye anga za Mwigulu Nchemba.

Umemtaja kuwa ni mmoja wa watuhumiwa wa EPA, wakati wizi huo umetokea mwaka 2005, wakati Nchemba ameingia BOT mwaka 2006 wakati wizi huo ukitokea alikuwa chuoni.

Haya lete huo uthibitisho wa madai yako.
 
Haraka na mapepe ya nini? Tulizeni munkari enyi vibaraka wa nape mnaokubali kuwa watumwa wa fikra. Huyo Mwigulu mnayemtetea jasho la masaburi linamtoka coz he knows very well who is John Mnyika. Mawaziri wote wanakiri kuwa Mnyika ni makini kuliko mbunge yeyote wa ccm. Mnyika siyo mtu wa kukurupuka hata kidogo.

Cdm kuna majembe ya ukweli. Yule kilaza wa Cuf jana anasimama na kumkashifu Mbowe. hivi huyo msomi prof. Na Mbowe ni nani mwenye mafanikio kiutendaji na Kiuongozi? Shame on you.
 
Jamani shule mmesoma sawasawa.kuna kitu kinaitwa kuwajibika kwa makosa ya wenzako kama hukuchukua tahadhali ya kutoa taarifa mapema.Nchembe hata kama aliajiri baada ya wizi hawezi kukwepa kuwajibika kujibu tuhuma kama aliajiriwa kwenye kitengo cha EPA lazima huyo ni mtuhumiwa kwa kuwa aliendeleza kuhifadhi nyaraka zilizotumika kuiba.Kiutaratibu wewe ukipewa cheo halafu ikagundulika kama kuna wizi ulifanyika na watu waliokalia kiti hicho kabla ya wewe lazima wewe ni mtuhumiwa sheria itakutema mahakamani lakini utakuwa umepewa tag ya MTUHUMIWA.nCHEMBE is not excluded he has a case to answer.
 
Katika hali ya kuchanganyikiwa na sek seke za Nchemba, Mh. Mnyika alijikuta akijiingiza matatani bure kwa kudai kwamba Nchemba naye ni mhusika wa wizi wa EPA pale BOT. Sasa Nchemba laiingia BOT 2006 na tayari wizi ulikwishatokea, na Mnyika amepewa siku 7 kutoa uthibitisho. Atafanya nini masikini kijana huyu ambaye ni kama kachanganyikiwa kabisa sasa.
Nawashauri wabunge wa CDM kuepuka kushindana na Nchemba, watajikuta pabaya sana. Huyu jamaa ni bingwa wa ku provoke watu. .Achaneni naye, mtaumia

Source: Mnyika amhusisha Nchemba na EPA
Usikurupuke kuandika mambo bila kufikiri vyema .Kama una uhakika kuwa walioingia kazini mwaka 2006/2007 hawakuhusika na uwizi wa fedha za EPA una haki ya kuandika hayo unayosema .Unajua fedha za EPA zilianza kuibiwa lini na kukoma lini ?Unauhakika gani kuwa fedha za EPA kuwa ziliibiwa zote mpaka kufikia 2005,uandike kuwa aliyeingia 2006 hakuzikuta?,Unajua nini maana ya Fehda za EPA? Unauhakika gani kuwa a/c ya fedha hizo ilifungwa kufikia 2005 kwa hiyo walioingia 2006 hawakuweza kutoa ama kuweka fedha kwenye a/c hiyo?

Nilichogundua ni kwamba wengi mliomsikia Mwiguli akijijitetea hakuwa mkijua nini maana ya EPA.Jua nini maana ya EPA ndio uanze kumuhukumu Mnyika kwamba alikurupuka ,ila kama hujui uliza na usubiri Mnyika atakapotoa utetezi wake ndio tumuhukumu kuwa J. Mnyika ni mtu wa kukurupuka.
 
Katika hali ya kuchanganyikiwa na sek seke za Nchemba, Mh. Mnyika alijikuta akijiingiza matatani bure kwa kudai kwamba Nchemba naye ni mhusika wa wizi wa EPA pale BOT. Sasa Nchemba laiingia BOT 2006 na tayari wizi ulikwishatokea, na Mnyika amepewa siku 7 kutoa uthibitisho. Atafanya nini masikini kijana huyu ambaye ni kama kachanganyikiwa kabisa sasa.
Nawashauri wabunge wa CDM kuepuka kushindana na Nchemba, watajikuta pabaya sana. Huyu jamaa ni bingwa wa ku provoke watu. .Achaneni naye, mtaumia

Source: Mnyika amhusisha Nchemba na EPA
Mnyika anashangilia baada ya kushinda kesi, hachangii mijadala ya bunge.
 
mleta thread ameekurupuka, na inaonekana yupo kwy payroll ya nchemba, 'etii mnyika akalia kuti kavu' haupaswi kuhukumu kabla ya ushahidi kuletwa. subiri siku saba ndio ulete maoni yako hayo na c kuhukumu kabla ya!
 
mnyika nilikushauri tulizana usipende kuropoka hovyo angalia sasa umeingia kichwa kichwa kwenye anga za mwigulu nchemba.

Umemtaja kuwa ni mmoja wa watuhumiwa wa epa, wakati wizi huo umetokea mwaka 2005, wakati nchemba ameingia bot mwaka 2006 wakati wizi huo ukitokea alikuwa chuoni.

Haya lete huo uthibitisho wa madai yako.
kweli kaingia kichwa kichwa........imekaa vibaya
 
mleta thread ameekurupuka, na inaonekana yupo kwy payroll ya nchemba, 'etii mnyika akalia kuti kavu' haupaswi kuhukumu kabla ya ushahidi kuletwa. Subiri siku saba ndio ulete maoni yako hayo na c kuhukumu kabla ya!
ndiyo maana imeandikwa kakalia kuti kavu... Hajaanguka bado. Anaendelea kujiokoa asianguke. Zingatia kwamba kakalia kuti kavu
 
Kifo chako uwa kinakuwa miguu juu kisha habari yako inakuwa imekwisha! Kamanda Mnyika afundishwi uoga.Hivi Unafikiri adhabu hatakayopewa hata ikidhibitika kuwa kasema uongo(Kitu ambacho siyo kweli) itakuwa kuwa kumvua ubunge?Laaasha!
Mnyika yupo ok kama ni kuchanganyikiwa nafikiri mleta uzi ndiyo anaelekea huko
 
Dogo anatumia porojo za JF kujengea hoja bungeni.
Hii ndo utajua hawa watu ni ujanja ujanja tu hawana umakini wowote.

Mi sikubaliani kabisa na umri wa urais kupunguzwa maana vijana bado wana mihemko wanaitaji kutulia na kujifunza namna ya kuendesha siasa.
 
Hilo ni tatizo lako, mimi naongelea hili tatizo alilonalo Mnyika kabla hajaanza kupashana na Nchemba.

Namuonea huruma huyu kijana na nnatumai watu wazima wenzangu wanaomzunguka (walio karibu nae) wananisoma pia na watafata ushauri japo kwa kumtazama mwenendo wake kwa umakini (ndani na nje ya bunge) wala sileti hizi mada kuhusu Mnyika kwa ajili ya kujibizana kwake Bungeni au hoja zake, la hasha, mimi naongelea afya yake.

Jionee huruma wewe mwenyewe kwa kujaribu kupandisha maji kilimani kwa gunia
 
Kama Chemba aliingia baada ya wizi kufanyika, nae hakusema lolote baada ya kugundua wizi huo(lazima pengo aliliona) basi nae ni mtuhumiwa mmojawapo!! Hivo kinachohitajika ni ushahudi wa kuibwa kwa pesa za EPA na Chemba kufanya kazi BOT!!‏

Rahisi sana kwa Mnyika!! ‎
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom