Mnyika aanika Siri nzito CHADEMA!!

VIVA CDM, na wabunge wengine wafanye hivyo hivyo kwenye majimbo yao wasisubiri mpaka viongozi wa kitaifa wafanye hivyo
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kuzindua matawi katika kila kata nchini, ili kujihakikishia ushindi wa asilimia kubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2014 nchi nzima.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, katika ziara ya ufunguzi wa matawi na msingi 10 ya chama hicho kata ya Kimara.

Akizindua tawi la Kilungule ‘B’, Mnyika aliwaambia viongozi wa matawi hayo kuziona ofisi hizo kama mbadala wa ofisi za Serikali za Mtaa zinazoongozwa na CCM kwa kuwasaidia wananchi.

Aliwataka viongozi hao kutumia changamoto na matatizo wanayopelekewa na wananchi kuwabana wenyeviti wa serikali za mitaa, ili kuhakikisha hawarudi mwaka 2014.

“Ndugu zangu wa Kilungule ‘B’ pamoja na changamoto za kisiasa mlizokuwa nazo mmefanikiwa kujenga ofisi za matawi na misingi … zitumieni vizuri, ili tuweze kupata ushindi mkubwa katika chaguzi zinazokuja,” alisema.

Mnyika pia amewakabidhi viongozi wa matawi hayo taarifa za mipango na matumizi ya maendeleo ya jimbo lao ili kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu mambo yanayotekelezwa na yasiyotekelezwa na serikali.

Pamoja na mambo mengine, Mnyika alitumia fursa hiyo kutoa mwongozo wa kudai Katiba mpya, ili kuhakikisha mwaka 2015 wanapata Katiba itakayowaondolea dhuluma nyakati za uchaguzi mkuu.


Source: Tanzania Daima

My Take:
Ni wazi kwa wale waliokuwa hawajui kwanini CDM wanajiamini kuchukua dola mwaka 2015 ni kutokana na mkakati huo ulioanikwa na Mkurugenzi wa habari na uenezi John Mnyika kwamba chama kitazunguka kata zote nchini na kufungua mashina na misingi.Pili ofisi za Kata zitatumika kupokea matatizo ya wananchi ili kuona namna ya kusaidia utatuzi.Watu sasa wanapaswa kumshangaa John Tendwa na mwenzie Benson Bana wanaotaka CDM isifanye mikutano wala kuzindua mashina sasa mpaka nyakati za uchaguzi.Ni wazi mpango wa John Tendwa na Benson Bana ni hila ya kuhakikisha CDM haifiki vijijini kwa wananchi.Ni wazi CDM wamegundua mbinu hii ndiyo maana John Mnyika ameweka hadharani siri/mkakati mzito wa CDM kuingia Ikulu 2015.

Source yenyewe Tanzania Daima hahahaha
 
Haswaaaaa hiyo ndio kazi ya siasa. Unazichanga karata zako vizuri na kucheza karata dume.
 
VIVA CDM, na wabunge wengine wafanye hivyo hivyo kwenye majimbo yao wasisubiri mpaka viongozi wa kitaifa wafanye hivyo

Umetoa ushauri mzuri sana,nadhani waheshimiwa wote wanapitapita humu na watafanyia kazi.
 
Kwa hii source ya mwenziwe na Uhuru, tutegemee nini?
- Source ni TANZANIA DAIMA- TANZANIA DAIMA ni kwa ajili ya kusoma wapenda maendeleo, Haki, Usawa na wanaotaka ukombozi wa Taifa ili yaani TANZANIA- Wapenda maendeleo, Haki, usawa na ukombozi wa Taifa ili ni CDM- Yaliyoandikwa yanahusu CDM na mkakati wa kupata ushindi wa kishindo 2015 kosa lipo wapi?
 
Kila la heri CDM lakini zisiwe mbwembwe fanyeni kazi mjenge nchi hi. Peoples poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer
 
Hayo ni matope? Mnahofu ya kushindwa 2015. Jiandaeni kisaikolojia kupokea matokeo yatakayowafukuza madarakani CCM. Ufisadi wa CCM mwisho wake ni 2015
naona heading za magazeti zimehamia jf.heading inakuwa kubwa ndani ni matope
 
Hayo ni matope? Mnahofu ya kushindwa 2015. Jiandaeni kisaikolojia kupokea matokeo yatakayowafukuza madarakani CCM. Ufisadi wa CCM mwisho wake ni 2015

Nakushukuru mkuu kwa majibu mazuri sana!
 
mkuu hebu tuache na utani muda mwingine.

Inamana we bado hujaona siri aliyoianika Mnyika?

Mkuu wangu Shardole,watu wengine nashindwa hata kuwajibu kwa sababu nawaheshimu sana lakini hawajaelewa maana yoyote kwenye hii thread.Hawajui kuwa Great Thinker ni lazima ..To think Big.
Thankyou Shardole.
 
mkuu Molemo ahsante sana na Mungu akubariki kwa kutuanikia siri ya kamanda Mnyika kwamba nchi ni yetu 2015 kutokana na siri/ mikakati hiyo.

Mkuu wangu Shardole..watu wanadhani siri nzito ni mpaka kuandika habari za kulipuana.Hata hizi za namna ya kuchukua nchi ni siri nzito tena za maendeleo.Kabla Mnyika hajasema ni nani alijua wananchi wanatakiwa kutumia ofisi za kata za CDM kama mbadala kwa serikali za mitaa zinazoongozwa na CCM? Nani alijua lengo kubwa la kufungua mashina kila kata ni ile ushindi wa serikali za mitaa 2014 uwe mkubwa na wa kishindo? Kuna watu hapa wamefunikwa kwa shuka la Tendwa kwamba CDM isizunguke mikoani mpaka kipindi cha uchaguzi tu..Mkuu Shardole tuko pamoja sana!
 
eti kuchukua nchi? mnaota kweli, 2015 wakristo wote waliompigia kura slaa kwa chuki ya kumchukia kikwete watarudi kupigia kura ccm, kikwete atakuwa anamaliza vipindi vyake.
 
eti kuchukua nchi? mnaota kweli, 2015 wakristo wote waliompigia kura slaa kwa chuki ya kumchukia kikwete watarudi kupigia kura ccm, kikwete atakuwa anamaliza vipindi vyake.

Mtu mjinga usiye na aibu unaandika upumbavu kama mtu aliyejipaka kinyesi.
 
- Source ni TANZANIA DAIMA- TANZANIA DAIMA ni kwa ajili ya kusoma wapenda maendeleo, Haki, Usawa na wanaotaka ukombozi wa Taifa ili yaani TANZANIA- Wapenda maendeleo, Haki, usawa na ukombozi wa Taifa ili ni CDM- Yaliyoandikwa yanahusu CDM na mkakati wa kupata ushindi wa kishindo 2015 kosa lipo wapi?
Mapenzi huwaga matamu!!!
 
Back
Top Bottom