Mnyika aanika Siri nzito CHADEMA!!

So mwandishi amefanikiwa kuvuta watu ila kila anaeingia anabaki kucheka tu... maana hiyo said "siri Nzito' haonekani ila ametubamba!

Katubamba hasa, maana mie ndio thread yangu ya kwanza kuisoma.
 
Baba hujasomeka siri nzito au ndo kama vichwa vya habari vya magazeti ya rangi rangi
chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kinatarajia kuzindua matawi katika kila kata nchini, ili kujihakikishia ushindi wa asilimia kubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2014 nchi nzima.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki jijini dar es salaam na mbunge wa ubungo, john mnyika, katika ziara ya ufunguzi wa matawi na msingi 10 ya chama hicho kata ya kimara.

Akizindua tawi la kilungule ‘b’, mnyika aliwaambia viongozi wa matawi hayo kuziona ofisi hizo kama mbadala wa ofisi za serikali za mtaa zinazoongozwa na ccm kwa kuwasaidia wananchi.

Aliwataka viongozi hao kutumia changamoto na matatizo wanayopelekewa na wananchi kuwabana wenyeviti wa serikali za mitaa, ili kuhakikisha hawarudi mwaka 2014.

“ndugu zangu wa kilungule ‘b’ pamoja na changamoto za kisiasa mlizokuwa nazo mmefanikiwa kujenga ofisi za matawi na misingi … zitumieni vizuri, ili tuweze kupata ushindi mkubwa katika chaguzi zinazokuja,” alisema.

Mnyika pia amewakabidhi viongozi wa matawi hayo taarifa za mipango na matumizi ya maendeleo ya jimbo lao ili kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu mambo yanayotekelezwa na yasiyotekelezwa na serikali.

Pamoja na mambo mengine, mnyika alitumia fursa hiyo kutoa mwongozo wa kudai katiba mpya, ili kuhakikisha mwaka 2015 wanapata katiba itakayowaondolea dhuluma nyakati za uchaguzi mkuu.


source: Tanzania daima
 
Molemo

nafiri alidhani Mnyika kapotea kwa kusema uchaguzi 2014 badala ya 2015. La hasha kama alikua anafikiri
si hivyo ni hivyo. uchaguzi wa serikali za mitaa ni 2014 na uchaguzi wa wabunge madiwani na Rais ni 2015.

Kama kuna siri uliyokua unataka kutuaminisha iseme kuliko kukopi na kupaste habari za magazeti

Nadhani siri ni huo mkakati wa kila kata Tz nzima!! Halafu pia ni sanaa ya kiuandishi kuvutia wasomaji.;. Hii sio ripoti kusema heading accuracy counts. Sawa mlema taarifa hujakosea pia umefanikiwa wengi watautembelea uzi huu
 
Nadhani siri ni huo mkakati wa kila kata Tz nzima!! Halafu pia ni sanaa ya kiuandishi kuvutia wasomaji.;. Hii sio ripoti kusema heading accuracy counts. Sawa mlema taarifa hujakosea pia umefanikiwa wengi watautembelea uzi huu

Nakushukuru mkuu kufafanua vizuri sana.Thats why we are GT
 
Siri nzito ndio hiyo? kufungua vijiwe vya vibaka ndio siri? Mi nilishangaa sana kuwa Mnyika anaanika siri nzito wakati hiyo ni kazi ya Slaa aka mzee wa madocuments ya siri.
 
mimi nilijua kajilipua tena kumbe ni ufunguzi wa matawi.................sielewi kiukweli.

Huelewi nini mkuu? Huelewi CDM sasa itakuwa na ofisi kila kata? Huelewi CDM imejiandaa kukamata dola 2015?
 
Back
Top Bottom