Mnyika aanika Siri nzito CHADEMA!!

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kuzindua matawi katika kila kata nchini, ili kujihakikishia ushindi wa asilimia kubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2014 nchi nzima.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, katika ziara ya ufunguzi wa matawi na msingi 10 ya chama hicho kata ya Kimara.

Akizindua tawi la Kilungule ‘B', Mnyika aliwaambia viongozi wa matawi hayo kuziona ofisi hizo kama mbadala wa ofisi za Serikali za Mtaa zinazoongozwa na CCM kwa kuwasaidia wananchi.

Aliwataka viongozi hao kutumia changamoto na matatizo wanayopelekewa na wananchi kuwabana wenyeviti wa serikali za mitaa, ili kuhakikisha hawarudi mwaka 2014.

"Ndugu zangu wa Kilungule ‘B' pamoja na changamoto za kisiasa mlizokuwa nazo mmefanikiwa kujenga ofisi za matawi na misingi … zitumieni vizuri, ili tuweze kupata ushindi mkubwa katika chaguzi zinazokuja," alisema.

Mnyika pia amewakabidhi viongozi wa matawi hayo taarifa za mipango na matumizi ya maendeleo ya jimbo lao ili kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu mambo yanayotekelezwa na yasiyotekelezwa na serikali.

Pamoja na mambo mengine, Mnyika alitumia fursa hiyo kutoa mwongozo wa kudai Katiba mpya, ili kuhakikisha mwaka 2015 wanapata Katiba itakayowaondolea dhuluma nyakati za uchaguzi mkuu.


Source: Tanzania Daima

My Take:
Ni wazi kwa wale waliokuwa hawajui kwanini CDM wanajiamini kuchukua dola mwaka 2015 ni kutokana na mkakati huo ulioanikwa na Mkurugenzi wa habari na uenezi John Mnyika kwamba chama kitazunguka kata zote nchini na kufungua mashina na misingi.Pili ofisi za Kata zitatumika kupokea matatizo ya wananchi ili kuona namna ya kusaidia utatuzi.Watu sasa wanapaswa kumshangaa John Tendwa na mwenzie Benson Bana wanaotaka CDM isifanye mikutano wala kuzindua mashina sasa mpaka nyakati za uchaguzi.Ni wazi mpango wa John Tendwa na Benson Bana ni hila ya kuhakikisha CDM haifiki vijijini kwa wananchi.Ni wazi CDM wamegundua mbinu hii ndiyo maana John Mnyika ameweka hadharani siri/mkakati mzito wa CDM kuingia Ikulu 2015.
 
Ninachoomba ni kimoja hizo ofisi, ziwe ofisi za kweli. Kwanza, majengo yasitawaliwe na ufisadi. Ziwe za ukweli hata kama ndogo.

Maana yale maofisi ya CCM ninayoyakumbuka, sucks!!!
 
naona heading za magazeti zimehamia jf.heading inakuwa kubwa ndani ni matope
 
Ninachoomba ni kimoja hizo ofisi, ziwe ofisi za kweli. Kwanza, majengo yasitawaliwe na ufisadi. Ziwe za ukweli hata kama ndogo.

Maana yale maofisi ya CCM ninayoyakumbuka, sucks!!!
 
Molemo

nafiri alidhani Mnyika kapotea kwa kusema uchaguzi 2014 badala ya 2015. La hasha kama alikua anafikiri
si hivyo ni hivyo. uchaguzi wa serikali za mitaa ni 2014 na uchaguzi wa wabunge madiwani na Rais ni 2015.

Kama kuna siri uliyokua unataka kutuaminisha iseme kuliko kukopi na kupaste habari za magazeti
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom