Mnyakyusa wa Kwanza London(utani)

Wadau hii nimehadithiwa juu ya jamaa wawili Mwakipesile na mwenziwe Mwakalobo.
Hawa walipelekwa na chama chao cha ushirika kusoma huko London miaka ya 50's.
Walipofika tu wakahifadhiwa katika hoteli moja ndefu sana ya ghorofa 25 na wao wakaka ghorofa ya 18.
Kwa vile hawakuuona mji wa London kwa vile walifika usiku asubuhi sana Mwakipesile akaamua kudamka na kuuona mji mapema.
Mwenziwe Mwakalobo alipoamka na asimwone Mwakipesile akawa na wasi wasi hivyo akaenda balcony, na chini kabisa akamwona Mwakipesile akifanya window shopping kwa kutazama bidhaa madirishani.
Kwa vile Mwakalobo yeye bado hakuwa ameoga na kunyoa(shave) asubuhi akatafuta wembe asiuone, hivyo katoka tena balcony na ikaw hivi
Mwakalobo akipiga kelele kwa sauti:MWAKIPESILE MBAPO ULWEMBE!!
(Mwakipesile nipe wembe)
Mwakipesile hakusikia na akaendelea na widow shopping, lakini polisi mmoja akaona tukio hilo na aielewe jamaa anasema nini kwa vile helewi kinyakyusa.

Mwakalobo akiendelea kupiga kele:"MALAFYALE MWAKIPESILE MBAPO ULWEMBE!"

Yule polisi akifikiri huyu jamaa nataka kujiua akaenda mbio mpaka ghorofa ya 18 , na alipomkuta Mwakalobo chumbani akamuuliza :"whats wrong sir"

Mwakalobo akamjibu:" Mwakipesile , there, shaving blade, no me"
Polisi akaenda balcony akatoa kiona mbali(binoculars) ambayo Mwakalobo alikuwa hajapata kuiona.
Baada ya kumfocus Mwakipesile, polisi yule akamwonyesha Mwakalobo kama ndiye anayemtafuta.
Mwakalobao alipomwona rafikiye yuko karibu saaana, hata sauti akapunguza kabisa kama anaongea kwa utaratibu sana na mtu aliyekaribu:" Mwakipesile mbapo ulwebe!!"


jubaaa tufwile nyambaya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom