MNH hali tete,vyombo vya habari vinapotosha!

Shansila

Senior Member
Jan 28, 2012
189
36
Nimesikiliza vyombo vya habari vya kimataifa kama BBC na Deustch Velle,jamani hali ta Hospitali ya Taifa ni mbaya!Baadhi ya wagonjwa waliohojiwa wameelezea hali katika wodi hospitalini hapo ni mbaya kwani kuna wagonjwa waliofanyiwa upasuaji kabla ya mgomo hawaonwi na waganga.

Huku wengine wakipoteza uhai. Cha ajabu ni kwamba, ukiangalia taarifa za habari katika vyombo vyetu vya ndani ya nchi utasikia 'hali ni nzuri, huduma zinaendelea kutolewa kama kawaida'!

Na baadhi yao vimewanukuu baadhi ya wagonjwa wakithibitisha hilo. Tumwamini nani?
 
Vyombo vya habari vya Tanzania ni Uchwara mtupu kushughulikia habari za kijinga tu hbr zote zenye ukweli na kulihusu Taifa wanazitupa ........................
Tanzania nani ameturoga?
 
Nakumbuka kipindi hakuna mgomo, hospitali ya muhimbili ilikuwa haina madaktari wa kutosha, vitanda vya kutosha manesi wa zamu wa kutosha, vifaa vya kupimia kama pressure, nk wodini.
Baada ya operation ya mgonjwa wangu Dr wake alikuja kumuangalia mara moja baada ya siku mbili, pia eti akiwa hayupo zamu, walio zamu huendeleza tu dawa bila kujali hali ya mgonjwa, walisema tungoje daktari wetu, tukimpigia simu akija, ugomvi na manesi unaanza.
Hospitali ya muhimbili inahitaji
- wafanyakazi wa kutosha wa kada zote wenye motisha
- vifaa vya kutosha
sasa hivi hakuna tufanyeje?
 
Propaganda huwapo wakati wa vita!Sasa naanza kumwamini mwandishi wa Mwanahalisi toleo fulani alipoandika makala isemayo NCHI IKO VITANI.Maana sioni kwa nn vyombo vyetu vya habari vinapotosha habari,tena kwa makusudi,cjui nia ni kuushawishi umma kuwa hakuna mgomo,na kuwapotosha madokta wengine ili waendelee na kazi?Hii nchi ni kama nchi ya Kichaa iliyoongozwa na mfalme Juha!
 
Back
Top Bottom