Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

1.Jumanne sebarua Tingisha,
2.fambo wa Fambo,
3. International beka wa bengari (IBB)

Pia walikuwa wakiomba nyimbo lazima upigwe.
 
ila ilikua jambo la kufurahisha mabingwa na mangwiji wa salamu wanapotumiana salaam kwenye kipindi kile cha mchana mwema, ama Jambo asubuhi.....maisha hayarudi nyuma, ila kuyakumbuka yanatupa maana kubwa.
miaka 30 ijayo kama Yesu Atakua hajarudi, tutakuwa wazee sana, wajukuu watakuwa wanakumbushana mabingwa wakutuma Post na threads kwenye mitandao....maana ktk kizazi hiki, salaam za radio sio kitu mashuhuri.,.....watakua wanasema kulikua na Mwanakijiji, First lady, Tumaini na wengineo.....maana kila zama na mambo yake.
 
21. Ongeza..... Sura Mbili ( nimesahau jina la kwanza maana hii ni AKA - Huyo alikuwa akituma zile salam za kuunganisha anataja watu kama 10 kama salamu za kwanza, za pili watu kama 30..nk.. alikuwa ana kipaji cha kuongea kama cherehani!

Huyu alikua Sura Mbili Kiango Mamanyi kama sijakosea.
 
Hahaaaaaaa,Mwanakijiji..Umenikumbusha mbali sana ndugu yangu,umenikumbusha vipindi vya Jambo na Mchana Mwema(Pokea Salamu) pale Radio Tanzania bila kusahau kipindi cha usiku cha Kijaruba cha Abdallah Mlawa,hivi vilikuwa ni vipindi maarufu sana vya salamu...Ilikuwa ukisikiliza vipindi hivi ni lazima utakutana na majina haya

1.Issa Hasssan Madjeshi

2.Chidi Chidi Chitenda

3.Chivalavala wa Chivalavala

4.Limonga Justin Limonga

5.Duwa Wajadi

6.Wajadi Fundi

7.Mohammed Kassim Saibaba

8.Jai Sikinde

9.Maalim Shabani Uledi

10.Boko Man Mwana wa Mkongoman

Mzee wangu umenikumbusha wakati niko shule ya Msingi miaka hiyo.. Imebidi nikliki SENKSI..
 
Hahaaaaaaa,Mwanakijiji..Umenikumbusha mbali sana ndugu yangu,umenikumbusha vipindi vya Jambo na Mchana Mwema(Pokea Salamu) pale Radio Tanzania bila kusahau kipindi cha usiku cha Kijaruba cha Abdallah Mlawa,hivi vilikuwa ni vipindi maarufu sana vya salamu...Ilikuwa ukisikiliza vipindi hivi ni lazima utakutana na majina haya

1.Issa Hasssan Madjeshi

2.Chidi Chidi Chitenda

3.Chivalavala wa Chivalavala

4.Limonga Justin Limonga

5.Duwa Wajadi

6.Wajadi Fundi

7.Mohammed Kassim Saibaba

8.Jai Sikinde

9.Maalim Shabani Uledi

10.Boko Man Mwana wa Mkongoman

Nambrieeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee wa Kisalaweee
 
Nambrieeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee wa Kisalaweee
huyo alikuwa Vingunguti kiembe mbuzi, tunaongezea na Medi Kitandawili wa Temeke, pia kulikiwa na ukoo wa Macharanga kuanzia mzee wa macharanga hadi kijukuu cha macharanga
 
Pia walikuwepo wengine ambao ni maarufu sana Radio One na RFA

1.John Zenze
2.Ndilana Mwambi
3.Suleiman Rashid 'Mzee wa Dozi nene'
4.Marehemu Jangala Kilongosi wa Mbuguni Mererani
5.Jumanne 'JB' Ngilisho wa Arusha
6.Stephen Ishengoma
7.Bongo Experience
8.Juma Msurvivor
9.Teddy Big Mama
10.Manka Mushi
11.Bukavu Mwandinda
12.Papaa Osama wa Dodoma
13.Frank Malecela 'Mubosi' wa Kikuyu 5 Stars Dodoma
14.David Beckham Onana wa Dodoma
15.Dismas Chabela wa Chabela Camp Dodoma
16.Juhudi Mr Luvanda wa Tunduma Mbeya
17.Sita Tuma Kubanda 'Sita wa Sita' wa Mwanza
18.James Sinje wa Mbeya
19.Lajii Freedom wa Dodoma
20.Manase R. Muhaha 'Hambako'

we mbona unakumbukumbu sana Balatanda ???
 
Majority ya wana JF ni wa age kati ya late 1960's up to early 1980's.

Mwanakijiji ni wa late 1960's, karibu utapata wajukuu na umri wa kugombea urais karibu utatimia.

Punguza michezo.
 
Wewe kiboko, nilitegemea nione jina lako kwenye kundi!

Hahaaaaaaaaaa,ukweli ni kwamba sijawahi kutuma salamu redioni hata siku moja mkuu,sema nilikuwa nikipenda sana Muziki,na kama unakumbuka zamani wakati wa Idhaa ya Taifa ya RTD Muziki ulikuwa ukipigwa zaidi kwenye vipindi vya Salamu vya Jambo na Mchana mwema/Pokea Salamu(na baadae jioni njema japo kilikuwa kifupi cha nusu saa) na vipindi kama Kijaruba,So ukitaka kusikiliza Muziki ilikuwa sharti usikilize vipindi vya kutakiana salamu....Sana sana kulikuwa na vipindi maalumu(mara moja kwa wiki) vya Muziki kama Misakato,Club Raha Leo Show,Starehe na BP,Disco Show,Chaguo la Msikilizaji,Mambo Mpwitompwito,Kombora n.k..

So sikuwa mtuma salamu mkuu,bali najivunia kwamba nina kumbukumbu ya vitu vingi sana vilivyotokea kipindi cha nyuma hasa katika nyanja za Michezo,burudani na Siasa kwa mbaaaaali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom