Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Kulikuwa na "mabingwa wa salamu" ambao walikuwa hawakosekani aidha kutuma salamu au kutumiwa salamu kwenye vipindi mbalimbali vya radio. Unayakumbuka majina yao?

Zamani kila vipindi vya salam kwa njia ya simu redioni majina haya yalikua maarufu sana. Charles imalaya kama simba, kung'ombe chacha sukari muhilo obaré, basu basanga basu,baba dula one, chesco mzee wa matunda, imma kulaya, suzy ngodoki, manka mushi, jumane sebarua tingisha. Dah siku hizi majina haya yamefunikwa sana redion.

Unawakumbuka watuma salamu wa zamani RTD kipindi cha salamu? Kuna jamaa mmoja namkumbuka Chidi Chidi Chitanda alikua hakosekani kipindi cha saa sita mchana. Taja wengine.

Tujikumbushie watuma salamu na watumiwa salamu maarufu ktk Radio mbali mabali.
1.Baba Dura one wa Tanga
2.Chesco mzee wa Matunda
3. ...........
4. ..........
 
Hapa MM utakuwa umetukumbusha mbali kweli Huyo WAJADI FUNDI WAJADI alikuwa nae moto kwenye salaam..dah wapo wengi kweli naona hii thread itakuwa balaaa inakumbusha mbaaali kweli wakati hakuna option ya kusikiliza radio nyingine zaidi ya RTD na external service yao!!..nakakumbuka hadi kale kamziki kao ka salamu...afu kulikuwa na kipindi maalum cha mabingwa wa salam..kadi ngapi wametuma ..afu zawadi zenyewe flana au pesa kiduchu enzi hizo
 
Thomas Mushi Kimboka
Issa Hasan Majeshi aka kamanda wa salamu
Kangomba H Kangomba.
.
.
.
Duu, umenikumbusha mbali,
Enzi hizo miaka ya mwanzo ya 90, nilikuwa na rafiki wa karibu, mtangazaji RTD, alinihadithia mambo mengi.
Siku hizo mshahara wa Mtangazaji RTD akianza kazi ilikuwa ni Shilingi,
3,660.65.
Kikombe cha chai ya maziwa canteen yao pale Pugu Rd. ilikuwa Sh. 20, chapati, 20, andazi 10, mayai mawili ya kukaanga 40. Kipande cha kuku wa kukaanga ni sh.60.

Hao mabingwa wa salamu, walikuwa kila ukisoma kadi yake, kuna mahali unapita, anakupiga na Sh. 100. ukimaliza kipindi cha salaam, ukishuka canteen, hiyo 100, unapata chai, chapati 2 na mayai mawili ya kukaanga, kipande cha kuku na soda juu.

Jioni ukipita maeneo fulani, sio vi offer vinafululuza, akina dada ndio usiseme, enzi hizo redio yenyewe ilikuwa moja.

Hawa mabingwa wa salamu, ndio walikuwa wakiongoza kumwaga hizo 100, wakifuatiwa na wanamuziki wanaotaka nyimbo zao zipigwe, hawa walikata fungu kubwa zaidi,

Enzi hizo, Mghanii wetu akiwa 'Mzee Athumani Khalfani' akilipwa Sh.100 kughani kipindi cha nusu saa.

Jameni watu wametoka mbali!. Wee acha tuu!.
Mungu awarehemu watangazaji wote waliotangulia, na walibakia mpaka sasa, wapewe pongezi nyingi, na hata wazuri waliochipukia na wanaoendelea kuchipukia pia pongezi, ukiondoa wale wachache wana vamia fani.
 
mimi nasema wadau hao jamaa walikuwa wanatembeleana tu kwa kufahamiana kwa salamu,mimi namkumbuka baba dulla one.Nasikia kipindi hiko mtuma salamu anatoka tanga anakwenda kumsalimia mwenzake wa mwanza na akifika anapokelewa na anakirimiwa enzi hizo utu na ubinadamu ulikuwepo sio sasa mtu anapata ajali unamsachi kabla ya kumpa huduma.
 
zamani watanzania walikuwa wanapendana,wanajaliana katika raha na shida na ilikuwa ukimsalimia mtu kupitia redio pekee ya taifa,RTD huyo alietumiwa salamu anajisikia na kama watu walisikia jina lake watamtafuta na kumwambia na nikumfata alipo maana simu ya kiganjani ilikuwa bado kipindi hiko .Wewe angalia watu walivyokuwa wastaarabu unaweza ukatuma barua kwa mzee wako labda huko Rombo mkuu kwa kumpa mtu anaesafiri na bus na akipita maeneo hayo anaidondosha huku bus linakwenda itapodondokea inaokotwa na lazima ifike kwa mlengwa salama ,jaribu sasa uone.
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom