Maria Roza
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 6,797
- 1,567
Mh huyo cousin wako sasa haoni kama anajidanganya mwenyewe pia?? vipi siku mkewe akiziona hizo pic kwenye laptop inakuwaje sasa!.........Ujue kuna mabinti ni wajinga sana, wanatoa picha zao za kweli kwa wanaume, halafu utakuta mwanaume anamdanganya tu online kumbe kaoa na ana familia yake.
Nina cousin wangu ndio mchezo wake, anawadanganya sana wasichana humu online na ana picha kibao za mabinti kwenye laptop yake. Yaani yeye kafanya kama mchezo anadai anapima akili za wasichana. Halafu yeye wala hawapi picha hao wasichana, lakini wasichana walivyokuwa wajinga wanamtumia picha.
......Enyi wasichana wenzangu wenye tabia hii hebu mjue kujiheshimu, msipende kutuma picha zenu kwa wanaume humu wenzenu wanawachora tu.
Hebu tulieni mtakuja tu kuolewa, mbona wanaume wapo wengi wanaotafuta wasichana wa kuoa.........msijidhalilishe jamaniiiiii!!!